Hili bado sio suluhisho la kudumu. Muda si mrefu wakati wa distribution itaibiwa tena tu. Labda tuwaite waingereza watusambazie na kusimamia katika mashule. KInachohitajika ni hatua ya haraka ya kubaini nini hasa chanzo cha kuibiwa mitihani hiyo na kuwachukulia hatua kali waliohusika. Hilo likitushinda basi tumekwisha.
Ndio kusema, tangu mitihani ianze kuvuja miaka kadhaa iliyopita, hakuna yeyote aliyenaswa kuhusika? Na hapa nazungumzia kiongozi. Mtiririko mzima wa utungaji, uchapishaji, usambazaji na usimamiaji una viongozi. Hawa wote lazima wawajibike maana wanatakiwa kujua nini kinachoendelea kwenye section zao. Sio kwa maneno bali kwa vitendo. Kama kiongozi mkuu wao hawezi kusema na akatenda, watu wa chini yake watacheka cheka na wataendeleza mambo yao maana wanajua hakuna jipya la kuwatisha.
Kuna kitu wanaita root cause analysis (msingi wa tatizo). Je ni njaa? wanaiba mitihani wauze wapate hela ya kula? Je ni kwa sababu ya msemo kila mtu hula kazini kwake kwa hiyo kama hawana nafasi kwenye madini au TRL, TANESCO, EPA au TICTS basi nafasi yao ni kwenye mitihani? Je hii ndio nafasi yao ya kujipatia kama ambavyo traffic hujipatia rushwa yake kwa madereva? Au ni kwamba tatizo linaanzia kwa wanafunzi kwamba hawaelewi au hawazingatii masomo ilhali wanataka kufaulu?
Chanzo cha tatizo kikishafahamika, basi viongozi wawe strict kutoa adhabu stahili kwa wakati na bila upendeleo. Na wananchi wajulishwe ili yeyote mwingine aliyekuwa anafikiria mkakati kama huo ajue kitakachomkuta. Tofauti na hapo ni yaleyale. Je huyo kiongozi yupo?