Robert Heriel Mtibeli
JF-Expert Member
- Mar 24, 2018
- 28,297
- 68,017
KUCHELEWA KUOA HAKUKUFANYI UFANIKIWE AU UWE NA UNAFUU WA MAISHA!
Anaandika Robert Heriel.
Kwa kijana isipungue miaka 25 wala isizidi 33. OA mapema. Usikawie. Hakuna kitu kizuri kwenye maisha Kama Familia yako. Wewe, Mkeo na watoto.
Chelewa kupata yote usichelewe kuoa au kuolewa. Lazima itakusumbua sehemu Fulani Huko mbele.
Miaka 28-30 ndio miaka mizuri ya kupata Mke na kupata mtoto.
Usije jifanganya kuwa utaoa mambo yakiwa MAZURI, hakuna mambo mazuri kwenye maisha Kama kufanya Jambo Kwa wakati.
Kuna wakati wa kuoa
Kuna wakati wa Kulea.
Kuna wakati wa Kula pension
Hatimaye wakati wa Kifo.
Wengi unaowaona waliowafanikiwa kwenye maisha ya sasa hivi hawakuchelewa kuoa, walioa wakiwa na hali ngumu, lakini hawakujali.
Hakuna Jambo zuri Kama kumhudumia Mkeo na watoto ukiwa kijana mwenye NGUVU.
Sio unasubiri uzee ambao kimsingi unaanzia miaka 40 ndio Uoe.
Madhara ya kuchelewa kuoa utayaona kwenye malezi ya watoto wako.
Utayaona Kwa Mkeo kushindwa kummudu,
Na Kama ukishindwa kabisa kimaisha ndio utakuwaa kwenye hatari kubwa Sana na kubaki kuwalaumu wanawake na watoto wako.
OA hata Kama umepanga chumba kimoja
OA hata Kama unashindwa kulipa Kodi
OA hata Kama hujui kesho utakula nini.
Ilimradi uoe mwanamke unayefanana naye.
Usioe mwanamke mwenye ndoto kubwa ambayo anataka itimie hivi karibuni. Utashindwa, muache aolewe na waliokwisha kufikia ndoto hizo.
Usiyaogope maisha ingawaje yanaogopesha.
Usioe Kwa sababu unaona unauwezo wa kumhudumia Mwanamke na mtoto.
OA umri ukifika, OA ukiwa na nguvu, umri wa miaka 25-33 uwe umeoa.
Umri wa 20-30 uwe na walau mtoto mmoja au wawili.
Maisha hatahitaji kusubiri.
Usijilaumu Kwa lolote sio kosa lako wala la wazazi wako. Ndio mfumo wa maisha upo hivyo.
OA mapema bila kujali mazingira yanaruhusu au laa.
Usiige familia Tajiri, HAO wanachelewa kuoa na pengine kupata watoto Kwa sababu wanaurithi Kwa watoto wao.
Sasa wewe usiwaige.
OA mapema!
Robert Heriel
Taikon wa Fasihi
DAR ES SALAAM