Kucheleweshwa kwa Mkopo World Bank: Tumkemee Zitto Kabwe kwa pamoja

Kalamu1,

Habari za mwaka mpya?
Zito hajasema ukweli, tangu enzi ya Mwl Nyerere hakuna mwanafunzi aliyepata mimba akaendelea kusoma, ni upotoshaji wa hali ya juu. Watanzania lazima wafahamu kwamba hata nchi kubwa kama USA au UK huwa hawakubaliani kwenye mikakati yao ya ndani lakini linapokuja swala la kitaifa wote huwa kitu kimoja.

Anayekomolewa hapa sio JPM pamoja na baraza lake la Mawaziri etc bali ni wale ambao pesa hizo za mkopo zingewasaidia. Zito pamoja na wanaharakati wenzake wasisahau kitu kimoja. Whether they exist or not Tanzania will be there. Shame on them. BTW WB wameahirisha tu uamuzi wakati wowote ule wakiona Tanzania ina-secure mkopo kutoka nchi rafiki watapiga magoti kwa JPM achukue mkopo.

(I can bet you my last nickel, hivi sasa watu wapo kazini na utasikia kuna nchi watatukopesha pesa kwa bei nafuu zaidi au hata AfDB).
 
WE MLETA MADA NI NANI ALIWAAMBIA WATZ WAFYATUE WATOTO NAYE ATAWASOMESHA? HAYA HAYANA TOFAUTI NA MAUNO YA LUGOLA MWISHOWE KUTUMBULIWA
 
Hapa na Mimi ndo namshangaa huyu jamaa,sijui anawashwa?.
Kauli ya kufyatua watoto atawasomesha bure ilishatolewa Leo anawatetea?
 
Nashangaa Sana waafrika,Hawa wazungu hamwapendi na mnawaita mabeberu,Kama hatuwapendi na tunawachukia kwa Nini pesa zao tunazitaka?.
Kama wao Ni wabaya na pesa zao tuzione pia mbaya .
 
Mkuu Ole, ningependa sana nikujibu kwa moyo mtulivu ili unielewe ninachosema, lakini wakati huenda ukanivuruga na kukupa andiko ambalo halikunyooka kama nilivyotaka liwe.

1. Ninakubaliana nawe moja kwa moja kwamba hata enzi za Mwalimu na hadi awamu nyingine zote wasichana waliopata mimba hawakuendelea na shule. Hili ni kweli na liko wazi kwa kila mmoja wetu.

Lakini jambo hili halikuwahi kuwa kikwazo kwa wafadhiri kutoa msaada.
Hii sio kwa sababu Mh Zitto hakuwepo kuwashtaki hao viongozi wake toka enzi za Mwalimu , Mwinyi, Mkapa hadi Kikwete. Kikwete alilizungumzia hili "Kiuswahili swahili", na hakuna aliyelichukulia kwa uzito mkubwa likaishia hapo.

Sasa tofauti usiyotaka kuikubali kati ya huyu aliyepo na hao wengine ndilo tatizo. Tatizo sio Zitto.
Alivyolichukua na kulitangaza, na huku kwa upande mwingine akihimiza wanawake 'wafyatue,', 'contrast' ya ajabu sana.
Staili ya "Uwasilishaji" wa jambo, ukiambatana na hali nyingine iliyopo katika serikali yake, wewe bado huoni tofauti hiyo kubwa kati ya yeye na watangulizi wake?

Anavuta 'hisia' na 'attention' sehemu nyeti kabisa inayohitaji uangalifu mkubwa sana kuishughulikia. Hilo ni tatizo si katika jambo hili pekee, bali tumeona hata katika mambo mengine, kama ile mikataba ya madini. Mambo mazuri tunayotamani, lakini utekelezaji wake unatia ukakasi mkubwa.

Swala la hizo nchi kubwa, sikubaliani kabisa nawe hasa kwenye swala kama hili la ndani kwa ndani. Nadhani unachanganya au huna uelewa na maswala ya watu hao.
Hata hivyo, tofautisha kabisa hizo nchi na hizi zetu. Wao hawalilii misaada kama hiyo ya Benki kuu kuwasomesha watoto wao.
Usijifanye kutotambua sababu inayowafanya akina Zito waende huko kuomba msaada kama huo wa kuzuia. Ni kwa sababu hapa nyumbani hata wakilia machozi ya damu hawawezi kusikilizwa, sana sana wataishia gerezani au ya akina Lissu yanawapata. Hayo huyaoni huko uliko wewe, na bado unatoa mfano kama huo?

Unajiliwaza eti Benki wameahirisha tu, baadae watazitoa hela. Tunaomba iwe hivyo, kwa sababu funzo tayari litakuwa limewasilishwa kwenu. Kama nyinyi ni watu wenye akili kichwani hamuwezi kutojifunza chochote tokana na funzo hili.

Hata dunia itakuwa imewawashia mwanga kufahamu mapungufu yenu.

"Nchi marafiki watapiga magoti"
Hapa ndipo ninapokudharau kabisa.
Huko mwanzo tulipoanza kujibishana, kuhusi ile thamani ya shilingi ya Tanzania na dollar ya Kimarekani na kuhusu Waziri Mkuu Edward Sokoine, kidogo nilidhani wewe unao upeo kiasi fulani.
Sasa angalia mistari kama hiyo niliyoi-'quote' hapo juu!

Nadhani inanibidi nikupe pole sana.
 
Huwa hatuna tabia ya kuwasikiliza malaya wa siasa huweza uza vyote bila mipaka.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Nani anaeathirika na kunyimwa huo mkopo?.. Zito sio mzalendo ni mnafiki
 
Wanabodi za jioni!

Tangu naanza kufuatilia siasa zetu!nimekuwa nikimfuatilia huyu zitto kama mjenga hoja mzuri na mwanasiasa machachari hapa nchini!

Lakini kuna baadhi ya watu wamekuwa wakimhusisha na kitengo yaani usalama wa taifa!Swali la kujiuliza kama ni mwana usalama kwanini aivue nguo serikali inayomlipa mshahara??Lengo lake ni nini?Kwenye sakata la kunyimwa mkopo nchi yetu na Benki ya Dunia zitto ana mkono!kwenye sakata la kupinga kukua kwa uchumi wetu zitto yumo!kwenye lile sakata la Richmond alikuwemo!Karibia kila jambo ambalo linaipa kibano serekali ye yumo!sasa najiuliza anakuwaje mtu wa kitengo?

Hadi sasa ndio kiongozi pekee wa upinzani ambae hana kesi mahakamani japo anaongoza kwa kutoa hoja za kupinga na kuhujumu taarifa za serikali!Je serekali inampuuza?Je hana madhara kama Lema,Mbowe?Je serekali ina furahia hoja zake?Au ameshindikana wamemshindwa?Au ana nguvu za kipekee ambazo zinamlinda kuliko mwanasiasa mwingine wa upinzani?

Ana nini huyu zitto ambacho wenzake hawana? Yeye ni nani hadi ameshiriki Benki ya Dunia isitishe mkopo wake halafu bado anadunda tu? Mbona Tundu lissu alionywa kwa maneno hadi yakamkuta makubwa?

Anaemjua Zitto ni nani atuambie maana anaonekana sio wa kawaida huyu!au ni mzimu unaoogopwa??Angekuwa Lema je? ambae aliota tu miezi minne ndani!

Wanabodi naombeni mnisaidie kumwelewa Zitto Zuberi Kabwe!!!
 
Zito ni mwanasiasa tu ni mtu wakucheza na maslahi yake akiyakosa hubuni mbinu nyingi kuhakikisha anaogopwa
Alicheza na Makapuni ya madini kisha Richmond akacheza na mabilion yalipo uswis hasa kuwatishatisha
Alijipenyeza vizuri kwa baadhi ya viongozi enzi za Jk. Sasa huyu JPM kamtema anahasira sana


Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kitengo uwatumia watu waliowekwa upande mwingine ili kupush agenda fulani au kuzuia dili fulani kama halina maslahi kwa taifa.

Ili kisionekane kama kimefanya kazi direct ufanya kazi indirect.

Usalama wa taifa kiufupi ndio kazi yao kubwa kuzuia wakifeli kuzuia wanavujisha dili lilivyofanyika.

pande zote hizo Zitto anaonekana.

What if zile 500$ zilitaka kutumika vibaya? kinyume na tunavyoaminishwa?
 
Sawa mbona hana kesi hata moja mahakamani?
 
Zitto Ni Mwanasiasa pekee aliyekosana na mungu Mbowe lakini ameshindikana kupotea, aidha kufa au kufa kisiasa .

Na Kibaya Zaidi Wafuasi Wa Mbowe Wakiwemo Wachagga na Wapare Hawajakata Tamaa Ya Kupambana Naye.

Yaani huwezi kuwakuta wanamponda Lowassa Wala Sumaye Na Kuwaita Wanatumika Na CCM.

Na Kibaya Zaidi Jamaa Anavyozidi Kufanikiwa Ndio Kabisa Wanaumia Sana Roho.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…