Kucheleweshwa kwa Mkopo World Bank: Tumkemee Zitto Kabwe kwa pamoja

Kucheleweshwa kwa Mkopo World Bank: Tumkemee Zitto Kabwe kwa pamoja

Zitto ni chuma jiwe likijisogeza linapasuka


Sent from my iPhone using JamiiForums
 
Ninachojua gaidi na mpigania uhuru ni yuleyule. Ni kama ambavyo mzalendo na msaliti anaweza kuwa ni mtu yuleyule. Inategemea unamwangalia kwa mrengo gani. Mandela alikuwa ni gaidi kwa makaburu na nchi za magharibi ikiwemo marekani. Mpaka anaapishwa kuwa rais wa SA alikuwa kwenye orodha ya magaidi wasiotakiwa kuingia USA. Kwetu waafrika na nchi nyingine zilizokuwa zikiunga mkono mapambano ya uhuru wa mtu mweusi Mandela alikuwa ni mpigania uhuru na haki za mwafrika.

Lakini baada ya kuwa rais SA nchi zilizokuwa zikimuita gaidi zilishindana kumualika ili akatoe mihadhara kwenye mabunge yao huko ulaya na marekani kama kiongozi anayeheshimiwa duniani.
 
mmh! naona kama kuna mtego hapa kati ya serikali na upinzani.
ccm ni wajanja sana, hata hii barua unawezakuta ni ya vitna ili kuendelea kubaki madarakani.
na ndo akili ya mchezo, liwe goli la mkono au la halali end of the day inabaki UMESHINDA TU.
refer ile ya Zanzibar(2015), kati ya Maalimu seif vs Ccm.
(yangu macho tu, mimi sipigi kura na wala sina time na masiasa yao)
 
Rais hakikisha Zitto harudi bungeni aende kulima viazi maana hafai hata kwa mboga, anajikomba kwa wazungu
Rais hana jurisdiction yoyote juu ya Zitto kurudi bungeni au kutokurudi. Hilo suala lipo mikononi mwa wapiga kura. Hivi hata hizi siasa mnazielewa au ndio fata mkumbo?

Au unaamaanisha rais awatume wale 'gente desconocida'?
 
hivi Zitto ni nani?

kama ni uongo au uzushi.

Hoja hupingwa kwa hoja na sio marungu na bunduki.


Je ni kweli tunawazuia watoto wajawazito kusoma?

Je ni kweli hakuna uhuru wa kujieleza?

Je ni kweli vyama vya upinzani vinaonewa na kuwaacha kina Polepole na Dr Bashiru.

Je ni kweli Lipumba alikuwa kwenye mkutano wa ndani alikamatwa?

Je ni kweli Mwanasiasa Tundu Lissu alipigwa risasi zaidi ya 16 na mpaka sasa hakuna aliyekamatwa wala kushitakiwa?

kama majibu ya maswali hayo yote ni NDIYO!


Basi tusimlaumu zitto bali ni nafasi yetu kujicheki na kurekebisha mambo.
 
Rais hakikisha Zitto harudi bungeni aende kulima viazi maana hafai hata kwa mboga, anajikomba kwa wazungu
Niliwaeleza hapa tabia chafu za Zitto Kabwe kuwa siyo nzuri kwa Jamii ya Watanzania. Anatuletea vitabia ambavyo siyo asili wala Jadi yetu Watanzania. Huyu Jamaa kule anaitwa Akafanywe.
Mimi nawashauri Followers wa Zitto wa ACT Wazalendo wajue wanaongozwa na anayefanywa 😆😆😆😆😆
 
Kila mara tunaona maandamano ya wananchi wao mabeberu yanapojipanga kwenda kuzivamia nchi zenye mafuta, tunaona madhara ya vita kwa raia wanaovamiwa na political instability ya hizo nchi baada ya vita.

Sasa aina maana hao viongozi hawafikirii na wao what will happen na sio kwamba wanapenda kuzivamia hizo nchi. Ndio maana nchi za EU majeshi yao yakipiga bomu kwenye civilians area unaona jeshi linapewa wakati mgumu sana.

Lakini kwanini wanavamia kama wanajua madhara, sababu watakwambia ni national security interest.

Bila ya uhakika wa energy supply ni kuweka rehani uchumi wao na kuhatarisha maisha ya raia wao.

Hapo ndio wanaona kuna ‘moral obligation’ (this notion is very important in western politics when it comes to political decision making) na kwa mtazamo supply ya kupata mafuta ni muhimu kwenye kulinda interest zao hilo lina justify madhara ya vita.

Sasa ni upumbavu wa hali ya juu kwa nchi ambayo makusanyo yake ni $500m kwa mwezi tena serikari inajivunia hii aijawahi tokea tangia uhuru. Tena kufikia hapo ndio wamechukua na pesa za halmashauri, basically we are very poor maana hiyo ni hela ambayo some middle income countries inakusanya kwa siku tu, let alone mataifa makubwa.

Halafu anatokea mtu kwenda kupambana huko kuona serikari inakosa kiwango cha hiyo hela, ni upumbavu uliopindukia regardless of the motive you just can’t do that to a poor country, now this justifies any drastic measures against those involved; sio upuuzi wa kuangaika na watu kama akina Kabendera na Lissu.
 
View attachment 1340204
View attachment 1340206
View attachment 1340205

Nimesoma kwa ufasaha Taarifa zilizoandikwa na Mwandishi Tom Wilson kwenye Gazeti la FINANCIAL TIMES akiwa Uingereza kuwa baadhi ya viongozi wa Jamii ya Tanzania wakiongozwa na Mbunge wa Kigoma Mjini Ndugu yangu Zitto Kabwe kuiomba Benki Kuu ya Dunia kuahirisha kuipa Tanzania Dollar Milion 500 za mkopo kwa kile kilichoelezwa kuwa kufanya hivyo ni kuwapiga kofi la uso wanawake ambao wamezuiliwa kusoma huku wakiwa na ujauzito kwenye shule za Tanzania.

Kupitia Barua iliyoandikwa na kutumwa kwenda Benki ya Dunia na Zitto Kabwe wiki iliyopita na kupokelewa na Bodi ya Benki hiyo, Zitto ameandika taarifa za uongo kuwa Serikali inayoongozwa na Rais Magufuli imewanyima haki wanafunzi Wajawazito kusoma na badala yake inawahamasisha wanawake kuzaa kwa kadri ya uwezo wao ili kuongeza idadi ya Watu wa Tanzania. Nitanukuu "Excluded pregnant Girls from School and encourage women to free their ovaries to boost the country's population"

Ndugu Zitto Kabwe na washirika wake wanaamua kupotosha Hotuba za Rais kwenye maeneo tofauti tofauti kwa makusudi ili kukidhi matarajio yao.

Kuunganisha Hotuba za Mh. Rais za maeneo tofauti tofauti ili kuleta maana isiyo sahihi ili kukidhi matarajio yako ni makosa lakini pia ni dhambi.

Kupitia Barua yake Zitto Kabwe ya kushinikiza Tanzania kunyimwa fedha na Benki ya Dunia ameandika pia kuhusu fedha za kupunguza umasikini dola Milioni 450 ambazo ziliidhinishwa mwezi Septemba na benki hiyo kwa kujiridhisha kuwa Tanzania inafuata matakwa ya masharti ya fedha hizo, Zitto ameenda mbali zaidi na kuandika kuwa hakuna kilichobadilika!

Mkoa wa Kigoma ni miongoni mwa Mikoa ambayo Mwanafunzi wa Kike anakabiliwa na Changamoto Mbalimbali katika Masomo yake na Kwa kutambua hilo Serikali ya Tanzania kupitia mpango wa Elimu Bila malipo haukumtenga mwanafunzi wa Kike.

1. Mpango wa Elimu Bila malipo hauna Ubaguzi

Fedha za Ruzuku ya Elimu bila malipo Chini ya mwongozo uliotolewa Tar 28 Decemba 2015 umeelekeza fedha za Ruzuku kwa kila mwanafunzi wa Shule ya Msingi kuwa ni Tsh 6,000 na Sekondari Tsh 25,000 kwa kila Mwanafunzi kwa mwaka bila kujali kuwa ni wa Kiume ama wa Kike na fedha hizo zinatumwa Shuleni Moja kwa moja na kufanya kwa mwaka Serikali kutumia Tsh 12,329,791,183 kwa mwaka. Je, wasichana wetu wamenyimwa haki ya Kusoma?

2. Serikali imekuwa ikifuatilia kesi zinazohusiana na Wanafunzi wanaobebeshwa mimba na Wahusika wamekuwa wakiwajibishwa kwa Mjibu wa Sheria

Kwetu sisi ambao tumekuwa viongozi wa wananchi na kushughulika na matatizo ya wananchi wetu moja kwa moja tumekuwa tukikimbizana na watu wanaowapa mimba wanafunzi wetu na watu wanaokutwa na hatia hiyo wamekuwa wakiwajibishwa.

Kwahiyo maneno ya Zitto kuwa wasichana wenye mimba wamekuwa hawaruhusiwi kusoma na badala yake wanahamasishwa kuongeza jitihada katika kuongeza idadi ya watu Tanzania si za kweli kwani nchi inayowahamasisha wasichana kubeba mimba haiwezi kuweka sheria Kali za kuwaadhibu wanaowabebesha mimba wanafunzi wakati lengo ni kuongeza watu wa Tanzania.

3. Mfumo wa Elimu Nchini umewezeshwa kuwasaidia watu walioacha masomo kwa sababu mbalimbali ili kutimiza ndoto zao

Vituo mbalimbali vya Mitihani na Program za muda mfupi (miaka 2) inatambuliwa na Serikali ya Tanzania kwa miaka kadhaa sasa ili kuendeleza dhana ya Elimu kutokuwa na mwisho.

Ni dhahiri kwamba kama Tanzania ingekuwa inapinga mwanafunzi aliyebeba mimba kukosa haki ya kujielimisha isingetambua mifumo hii inayowarudisha watu hawa kupata haki hii ya Elimu na bado matokeo ya Mitihani yao inawawezesha kujiunga na Elimu ya Juu. Kwa hiyo si kweli kwamba wananyimwa haki ya Elimu.

4. Waziri wa Elimu ni Mwanamke.

Hili nalo pia linaweza kuwa chachu ya kuonyesha ni jinsi gani Serikali ya awamu ya 5 inadhamini mtoto wa kike kwenda shule. Mimi nimeona hivyo sijui nyie mnaonaje. Siamini kama Prof Ndalichako, mama huyu wa Kigoma anaweza kusimamia Wizara ambayo inachimbia handaki jinsia yake. Siamini pia kama Rais Magufuli anaweza kumteua mwanamke kwa lengo la kuzika matumaini ya wanawake kupata Elimu. Inahitaji kuwa na akili ya kichaa kuelewa lengo la Zitto katika kuamusha hisia za jinsia fulani kutengwa kielimu.

Mikopo na misaada inayotulazimisha kuchanganya wajawazito na wasio wajawazito hiyo inatakiwa kuangaliwa kwa macho na akili.

Mkuu wa nchi kukemea tabia za kubebesha na kubebeshwa mimba wanafunzi hapo anakuwa anatimiza wajibu wake. Tafsiri ya maneno ya Rais inayobebwa na mtu kupeleka sehemu fulani kwa lengo la kupotosha huko ni kukosa uzalendo.

Kuandika barua kwa siri kwenda kwenye taasisi ya fedha duniani kwa lengo la kudhuru nchi yako huku ukijua hauna nchi nyingine ya ahadi pia ni kiwango cha juu cha usaliti wa Utanzania wako. Ishitaki Serikali ya Tanzania kwa Watanzania wenzako na siyo kwa Mabeberu pamoja na mawakala wa Ukoloni mamboleo ambao hata hivyo uhusiano wetu na wao unatakiwa uwe wa kutumia akili sana.

Hata hivyo nimeona mrejesho wa Msemaji wa Benki ya Dunia akisema kuwa "Kutakuwa ni kutokomaa ikitokea yeye akazungumza chochote wakati Bodi ya Benki kuu ikiwa haijalitathmini jambo hilo "

Natambua matamanio ya mwanasiasa yoyote kama Zitto ni kuona Kunatokea Agenda yoyote inayoweza kusaidia Chama chake kukua na kutimiza malengo lakini napenda nimueleze kuwa Urais hautafutwi hivyo.

Siku ukiona unasaidiwa na Mataifa ya Nje kutawala Nchi ambayo mwanzoni mlipambana kwa hali zote muachwe ili muwe huru ujue ndio utakuwa mwanzo wa kuwakaribisha Wakoloni tena.

Upinzani wenye nia njema na Tanzania unajishughulisha na Watanzania wenyewe kwenye nchi yao, nenda Kusini, kasikazini Magharibi na Mashariki na kila kona zote za Tanzania, wakikuelewa watakupa Nchi. Urais wa Tanzania haupo mkononi mwa Benki kuu ya Dunia wala Ulaya.

Umewaacha Watanzania kwenye ardhi yao wakiwa wanafaidi mema ya Magufuli itakuwa ni ngumu kwao kukuelewa.

Mwambieni Zitto Serikali ya Magufuli anayoitumu vitu vingi vibaya inaendelea kumlipa Mshahara wake wa Mwezi na hajawahi kukataa hata siku moja Mshahara huo.

Najua atasema ni haki yake kulipwa lakini pia akumbuke kuwa haki hiyo inakumbukwa na Serikali ile ile anayoituhumu kwamba inavunja haki za Binadamu.

Ninasikitika sana kwamba Serikali ya awamu ya nne ilikuwa na mfumo wa kufanya kazi na Zitto lakini hii ya awamu 5 kidogo imejitenga nae kwa kiasi fulani na hivi ndivyo ameamua kuishi na Serikali hii.

Ni matumaini yangu kuwa sasa umefungua ukurasa rasmi wa kuachana na wewe kwenye vyombo vya uwakilishi.

Nchi haitafutwi hivyo.

#KigomaVoteWisely2020 #ourleaderisourproblem

Elia Fredrick Michael
Buyungu, Kakonko Kigoma

Aksante kwa kutujulsha Zitto ni mzalendo wa kweli na mpiganiaji haki za Wanawake !
 
Mkuu ongeza hii hapo mbele ili watu wajue tatizo linalotunyekelea

Hii ni ku-supplement tu why ZZK was so bitter about MKIRU!
Cha msingi tu kila mtu ashinde mechi zake..
 
Kwanza barua inaonekana ni feki.. Zitto hana kingereza kibovu hivyo..
Hata kama ni kweli sijaona uongo wowote alioandika hapo.. alichokiandika kila mtu TZ anafahamu na sio siri hata kidogo.
 
Back
Top Bottom