Kucheleweshwa kwa Mkopo World Bank: Tumkemee Zitto Kabwe kwa pamoja

Kucheleweshwa kwa Mkopo World Bank: Tumkemee Zitto Kabwe kwa pamoja

Zitto kweli mwanaume wa shoka. Kibao kinapigwa kila upande juzi Lissu amekuwa kwenye Kikao cha Mabunge akamwaga sumu na leo Zitto kamwaga sumu nyingine. Lazima serikali hii ijue watu siyo wajinga na kuzuia kuminya haki zao naye ataminywa na walimwengu ambao ndio tegemezi kuu. Tuone kama hiyo miradi yake mikubwa itawezekana maana sisi wananchi tumeshakamuliwa maziwa na damu tumebaki mifupa sasa ni kutegemea walimwengu ili kusonga mbele
 
aliyetuloga kasha kufa zitoooo nchiii hatuijengi kwa majungu na fitna maana ukipewa na wewe madaraka wataenda kuchoma halafu hatutaweza kwenda mbali....
ila kwakuwa siasa mtaji n maneno tuendeleee
 
Hawa wahuni tu hii sio barua ya Zitto.
Kwanza Kiingereza kibovu. Kuna mahali anasema In 2020 we will have general elections wakati barua ni ya Jan 22....maboya ya Lumumba tu ndio yanaweA kuandika huo upupu.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Sasa tutamsaidiaje gogo maana hali inazidi kuwa tete na haonekani kuchange inabidi ifanyike namna
 
Nimekuwa nikiangalia tabia ya Zitto tangu alipounda chama chake, akitoka CHADEMA. Hakuwa na la kufanya zaidi ya kujilazimisha kuunga mkono hoja za CHADEMA zikiitwa ni za UKAWA. Tangu Mwanzo yeye hakuwa na wenzake na ndo maana aliwaacha wenzake na kuingia bungeni wakati rais akihutubia Bunge.

Baadaye kapata njia, kupitia kwa Maalim lakini, ana tatizo jipya la uwezekano wa kukosa ubunge. Uwezekano huo ni mkubwa kwamba, hatarudi bungeni kazi aliyoizoea kwa miaka mingi bila umahili wowote kwa kazi nyingine.

Nimuonavyo, sasa anahangaika kupata umaarufu. Naamini anahanigika kupata ajira nje, Kwenye mashirika hayo akiaminia kwa sasa watauona uelewa wake. Nampa hongera kama kweli atapata ajira aina hiyo lakini aelewe hana uzoefu wowote nje ya shughuli za Bunge.
 
images (7).jpeg
 
Akili yako ndogo ya kuajiriwa unadhani kila MTU anafikiri kama wewe!
Kwanza Zitto Kabwe hana mpango na Ubunge kama unavyodhani wewe! Vipindi 3 kwa mtu mwenye akili kama Zitto vimemtosha kujenga Profile yake!
ACT - Wazalendo mwaka huu itakuwa ndani ya Serikali Zanzibar na Wabunge kibao.Zitto kama kiongozi mkuu maisha yataendelea hata bila Ubunge.
 
Hii dunia ina mambo mengi Sana

Mleta uzi una cheti cha taaluma maalumu yaani umethibitishwa na bodi ya taaluma maalum

You are "Certified Fool"

Unamjadili mtu karne ya ishirini na moja badala ya kujadili content ya anachokisema au kuandika

Je? Tanzania watoto wakipata mimba wanaweza rudi shule zile za serikali kusoma

Je? Tanzania kuna uhuru wa habari

Mkuu naweza sema wewe ni "Gifted Idiot"

Sio kila unapowashwa unakimbilia kuandika hapa JF, Tulia fanya utafiti na acha kujadili watu jadili Ideas
Nimekuwa nikiangalia tabia ya Zitto tangu alipounda chama chake, akitoka CHADEMA. Hakuwa na la kufanya zaidi ya kujilazimisha kuunga mkono hoja za CHADEMA zikiitwa ni za UKAWA. Tangu Mwanzo yeye hakuwa na wenzake na ndo maana aliwaacha wenzake na kuingia bungeni wakati rais akihutubia Bunge.

Baadaye kapata njia, kupitia kwa Maalim lakini, ana tatizo jipya la uwezekano wa kukosa ubunge. Uwezekano huo ni mkubwa kwamba, hatarudi bungeni kazi aliyoizoea kwa miaka mingi bila umahili wowote kwa kazi nyingine.

Nimuonavyo, sasa anahangaika kupata umaarufu. Naamini anahanigika kupata ajira nje, Kwenye mashirika hayo akiaminia kwa sasa watauona uelewa wake. Nampa hongera kama kweli atapata ajira aina hiyo lakini aelewe hana uzoefu wowote nje ya shughuli za Bunge.
 
Mwambieni Meko aache ubwege wa kuropokaropoka. Mara ooh, mabeberu hawatutishi, mara ooh, Tanzania yaweza kuwa donner country!

Huyo tajiri leo kaiva macho analilia pesa za mabeberu.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom