Nimekuwa nikiangalia tabia ya Zitto tangu alipounda chama chake, akitoka CHADEMA. Hakuwa na la kufanya zaidi ya kujilazimisha kuunga mkono hoja za CHADEMA zikiitwa ni za UKAWA. Tangu Mwanzo yeye hakuwa na wenzake na ndo maana aliwaacha wenzake na kuingia bungeni wakati rais akihutubia Bunge.
Baadaye kapata njia, kupitia kwa Maalim lakini, ana tatizo jipya la uwezekano wa kukosa ubunge. Uwezekano huo ni mkubwa kwamba, hatarudi bungeni kazi aliyoizoea kwa miaka mingi bila umahili wowote kwa kazi nyingine.
Nimuonavyo, sasa anahangaika kupata umaarufu. Naamini anahanigika kupata ajira nje, Kwenye mashirika hayo akiaminia kwa sasa watauona uelewa wake. Nampa hongera kama kweli atapata ajira aina hiyo lakini aelewe hana uzoefu wowote nje ya shughuli za Bunge.