Kucheleweshwa kwa Mkopo World Bank: Tumkemee Zitto Kabwe kwa pamoja

Kucheleweshwa kwa Mkopo World Bank: Tumkemee Zitto Kabwe kwa pamoja

Nimeipata Barua ya @zittokabwe aliyoituma kwenda Kwenye Bodi ya Wakurugenzi wa Benki ya Dunia.

Nimekumbuka shambulio la maneno ya @zittokabwe aliyofanya kwa @tundulissutz kwa kumuita Zwazwa baada ya CHADEMA kusema kuwa Wataishitaki Tanzania inyimwe misaada kutoka kwa Wazungu.

@zittokabwe alienda mbali zaidi na kusema kuwa mambo ya Tanzania yanatakiwa yamalizwe na Watanzania wenyewe kwenye ardhi yao.

Sisi wote tunajua kuwa heshima ya Taifa lolote ni Uhuru wa kuamua jambo na kutoka nje ya Mipaka na Lugha moja.
Leo Tanzania tumefika hapa.
Wanasiasa wa Upinzani Tanzania hawana uwezo tena wa kuwashawishi Watanzania wenyewe kushughulika na Serikali yao.

Nchi imevamiwa na Wasioitakia mema Tanzania kwasababu ya Tamaa ya Madaraka,wakiamini kwamba Serikali ya awamu ya 5 inaweza kunyoosha mikono kwa kushindwa kuongoza Nchi.

Ndugu yangu @zittokabwe Mimi ni Mdogo wako,ninaandika haya huku ukiwa bado hai na Afya ya kutosha ukiwa nayo.
Hili ni kosa kubwa kuwahi kufanywa na Mwanasiasa wa Tanzania na wqliofanya hivi maeneo mengine walipata adhabu inayowastahili.

Ulituvuta wengi katika siasa ila katika hili la kusaliti Serikali iliyoshikilia hatma ya Watanzania wenzako Kaka hapa upo pekee yako.

Nina uhakika Yesu aliposema ya Kaisari Mpe kaisari ilikuwa ni ishara tosha ya kuwaeleza watu kuwa Serikali nazo zina kibali maalum kutoka kwa Mungu.

Nikutakie kila la heri katika kusubili mapigo maana naamini katika hili umelifanya ukiwa unajua madhara yake.

Tuendelee kusalitiana kwenye ndoa zetu lakini kwenye Nchi yenu muweke adabu kidogo. Kumbukeni sisi tunapita lakini Tanzania itaendelea kuwepo.

Sina shaka kwasababu ya uzito kwa hiki ulichokifanya ni muhimu ukapata funzo ambalo litarudisha adabu na utii kwa Serikali ya wana wa Jamhuri wa Muungano wa Tanzania.

Ni Mimi Mdogo wako Elia F Michael.
Buyungu Kakonko Tanzania.

#Uzalendo.
#Tanzaniakwanza.

30/01/2020.
FB_IMG_1580413029285.jpeg
FB_IMG_1580413041187.jpeg
FB_IMG_1580413052723.jpeg


Sent using Jamii Forums mobile app
 
Elia F Michael,
Duuh yani kijana umeenda CCM juzi tu na ww umeanza vitisho?

Nilitegemea ungekuja kujibu hiyo barua kwa hoja ili kuonyesha alichoandika ni uongo kumbe unakuja na vitisho vya zitto kushikishwa adabu?? Hivi ni lini barua inajibiwa kwa bunduki?

Kama amepotosha ni jukumu lenu kujibu kwa takwimu ili kuwaconvince hao wafadhili wawape mkopo mnamshambulia whistleblower wa nini??

Kijana umekuja kwenye siasa za CCM juzi tu usijifanye ww ndo una uchungu kuliko kina Nape na January..... Siku ukija kuona rangi zao halisi utajuta kwa muda uliopoteza kutisha vijana wenzako mitandaoni Badala ya kushirikiana nao kuleta maendeleo kigoma.

Ni hivi maadam umeanza siasa jaribu kujenga urafiki na pande zote maana hujui leo na kesho siasa zitakupeleka wapi..... Nape leo anahangaika sababu CHADEMA kwenda hawezi na CCM ameshaharibu!! Choose your enemies wisely.
 
Tangu tu pale Zitto Kabwe alipoleta kashkashi CHADEMA wapinzani wengi waliamini kuwa huyu kijana ni mtumishi wa USALAMA WA TAIFA.\

Pale alipompondea Lissu aliposema kuwa wataishtaki Tanzania kwa wahisani ili Tanzania inyimwe misaada mbalimbali wapinzani wakazidi kuamini kuwa Zito katumwa kazi maalumu ndani ya upinzani. Hoja alizozitoa Tundu Lissu wakati ule kisha Zito akapondea ndizo hoja alizokuja nazo kipindi hichi. Anasahau kuwa technology imehifadhi kila alichoandika na kuongea tangu awe maarufu.

Zitto sio mwanaTISS bali ni kijana mjanja mwenye kujali tumbo lake na mwenye ndoto ya kuwa kiongozi mkubwa nchini, kila leo anatafuta umaarufu kwaajili ya siku za mbele.

Hakuna mwanaTISS akafanya jambo lolote la kukwamisha juhudi za serikali zaidi ya kujifanya yuko kinyume na serikali ili apate wafuasi ambao kesho na keshokutwa atakwenda kuwapeleka serikalini direct or indirect.

Zitto anapoona kuna nafasi kama ya uwaziri iko wazi au kuna teuzi kubwa mbele yake anajifanya kuinga mkono serikali, na asipoteuliwa anarudi tena kwenye upinzani.

Conclusion: Zitto apuuzwe na wanaCCM na watu wa upinzani, maana siasa zake za kishamba hazina tija kwa Watanzania
 
Elia F Michael, Nyie mnafikiri huyu jamaa na Tundu Lisu ni binadam kweli? Mbona wanaonekana kuwa sio wenzetu? Mtanzania gani ambaye amezaliwa kutoka kwenye kizazi kilicho lelewa kwa misingi ya ujamaa ya Julius Kambarage Nyerere anaweza leo akaisaliti nchi iliyo asisiwa na Baba yetu wa Taifa hivi na bado akawa mzimaa! Hii sio Tanzania ninayo ijua mimi.

Na Magufuli au bila Magufuli kwa vitendo vyao vya kuisaliti nchi hii laana kubwa iwapate, na hawa watu wawili Zitto na Lissu hawawezi pata madaraka tena Tanzania. Watanzania hawata wasamehe!

BBC na Zuhra Yunus wako nyuma yao. Wabarikiwe wote kwa kuto watendea haki watanzania.https://youtu.be/0n9gxGe7j6I



Sent using Jamii Forums mobile app
 
Huwa najiuliza Sana Hili swali, hvi Kwa nin Zitto anaitwa Ayatollah??
 
Mleta mada, tofauti yako na Zitto ni moja na ni kubwa sana - Zitto amechukua hatua ya anachoamini na wewe umelalamikia sio Serikali (kumbuka sababu za mkanganyiko wa elimu wa wanafunzi wapatao mimba) wala WB kwa kutotoa mkopo husika.

Zitto kuwa na taswira unayomchorea hakufanyi yako kuwa njema. TISS au sio TISS haihusiani na mkopo wala mimba za watoto wa shule.

Think far away from the box, not just out of it!
 
Augustine Mahiga anajua nini kitatokea kwa jpm Ndio maana yupo kimyaaaa kule Sheria na katiba
 
Back
Top Bottom