Kucheza Mpira V/s Bongo Flava, wapi angalau kuna uhakika wa maokoto ya kuendesha maisha kwa sasa?

Kucheza Mpira V/s Bongo Flava, wapi angalau kuna uhakika wa maokoto ya kuendesha maisha kwa sasa?

sky soldier

JF-Expert Member
Joined
Mar 30, 2020
Posts
5,407
Reaction score
19,264
Diamond naomba tumuwekee exception asiwepo, hata kwa sasa pesa anavuna zaidi kwenye uwekezaji

Binafsi nachoona ni wasanii ni wachache sana wanaoingiza hela kwa mziki pekee, kinachoumiza wasanii wengi ni kulazimika kuishi maisha ya juu kwajili ya brand, mfano kuishi nyumba za milioni 3 kwa mwezi, kuvaa nguo za gharama, n.k. hapa unakuta pesa yote inayopatikana inakaishia kwenye matumizi na mambo yakibana ndio wanaanza kuishi maisha feki na stress ndipo zinapoanza, Hata Vanessa Mdee aligusia hili.

Tukila kwa wachezaji wa mpira wa ligi kuu wapo zaidi ya 300 na wote wana uhakika kuingiza mkwanja kila mwezi ila ni kwamba wanatofautiana mishahara, wanasevu pesa zaidi maana hawana msukumo wa kuishi maisha ya kifahari, Bakhresa anatoa shilingi milioni 50 kila mwezi kwa kila timu ya ligi kuu kwa hio hata mchezaji acheze timu ndogo uhakika upo.

CONCLUSION: Kucheza mpira kuna uhakika zaidi kuliko Muziki ?
 
Mziki una maokoto mengi sana siku hizi, digital platforms zimeleta mageuzi makubwa sana katika vipato vya wasanii na hapo hugusi kabisa maonesho ya jukwaani.

Kiasi kwamba ukiweza kupata nyimbo mbili tatu zikapokelewa vizuri na zikapata viewers na listeners wengi basi una uhakika wa kusogeza kula yako kwa kipindi cha kutosha hata kama hutapata show wala kutoa nyimbo mfulululizo sana.

Mpira pia una maokoto ila sasa unatumia nguvu nyingi halafu mara nyingi inanufaisha wengine kuliko wewe mwenyewe, fedha nyingi zinaenda kwa washika dau na mawakala na klabu we unaishia kupata za maji kunywa unless uwe A class player, kitu ambacho ni adimu
 
bongo flavour.... ukiwa msanii mkubwa hela unazopiga kwenye concert moja sijui huo mshahara wa mcheza mpira wa kibongo utaingia mara ngapi

hapo hatujaongelea hela unazopata kwenye streaming platforms na brand deals
 
Wasanii wanaishi kwa muda mrefu kwenye fani hiyo tofauti na wanamichezo. Kwa hiyo uanamichezo unapesa nyingi ya muda mfupi ila usanii una pesa ya muda mrefu zaidi. Kote huko kunahitaji juhudi na bidii kubwa sana.

Kwangu mimi naona wasanii ndio wenye maokoto zaidi kwa Tanzania
 
Back
Top Bottom