Mimmi Adams
New Member
- Jul 24, 2022
- 2
- 0
Kama ilivyo kwa sehemu kubwa duniani, Afrika pia ni sehemu ambayo inajengwa na nguvu kazi ya vijana kwa asilimia kubwa na kama inavyojulikana kwamba vijana ni watu wenye nguvu, akili na uwezo wa kutenda mambo mengi kwa sababu bado wapo imara. Lakini ni ukweli pia kwa miaka mingi sasa nchi nyingi za kiafrika ndio zimekuwa nafasi ya chini kwenye sekta ya maendeleo licha ya nguvu kazi yake kwa asilimia kubwa kuwa vijana.
Kumekuwa na maoni mbalimbali kutoka kwa wanajamii, wasomi na hata vijana wenyewe juu ya sababu zinazopelekea matokeo ya namna hii na sababu nyingi ni zile zinazogusa mambo kadhaa ambayo hayazungumzii vijana wenyewe moja kwa moja, sababu nyingi zimekuwa zikigusia makosa yanayofanywa na serikali na sababu zingine zinazoendana na hizo. Lakini leo ningependa tutazame hili suala kwa namna tofauti, tuwatazame vijana wenyewe kwa kutazamia sifa au vigezo walivyonavyo kama visababishi pekee vya kuwawezesha kufika mahala fulani na kuwa na tija kama wanavyopaswa kuwa. Swali ni je, vijana wetu wengi, wa kiafrika wana vigezo vinavyohitajika kwenye soko la kimaendeleo la dunia?
Tunaishi kwenye ulimwengu uliojaa mabadiliko ya kila namna na kila siku bado kuna maboresho yanazidi kufanyika katika kila nyanja ya maisha. Afrika pia haijatengwa katika hilo, sisi sio kijiji, sisi ni sehemu ya dunia hii inayokua ambayo ni jamii kubwa na sote tunawajibika nayo. Hivyo sote tunahitajika kuwa na hamu ya kutaka kuwepo mahali fulani duniani, sote kama taifa na hakuna njia nyingine nzuri ya kuwezesha hili zaidi ya kuwafanya vijana,ambao ndio tegemeo kubwa la taifa, kuwa na uwezo wa kupambana kulifikisha taifa mahala bora zaidi na hatimaye iwe ni ushindi kwa Afrika kiujumla katika nyanja ya maendeleo.
Katika nchi nyingi za Afrika, elimu imekuwa kati ya sekta zinazopewa kipaumbele cha hali ya juu sana na hii ni kutokana na kwamba tumekuwa tupo nyuma kwa miaka mingi na kiwango cha upatikanaji wa elimu kwa watu wengi bado hakishawishi sana ukilinganisha na nchi nyingi hasa kwenye ulimwengu huu uliojaa ushindani mkubwa wa kimaendeleo. Kutoa elimu ni jambo moja, lakini kutengeneza utayari mahususi kwa wanaopokea hiyo elimu ni jambo lingine. Itakuwa ni hasara kubwa kama jitihada na rasilimali nyingi zitatumika kuhakikisha elimu inatolewa halafu wanaopokea elimu hiyo hawako na sifa za kuitumia hiyo elimu ili iwe ina manufaa sio kwao peke yao lakini kwa taifa kiujumla. Ni kweli kwamba, leo hii inaweza kuonekana kama vile “ah, maisha si yao bwana” lakini kiukweli hali hii ni hasara endelevu na kubwa kwa taifa la kesho ukizingatia vijana ndio watakaoshikilia nchi kwa vizazi vijavyo kwa hivyo kunahitajika kuwepo na msingi imara sana.
Ukifuatilia vijana wengi kwa ukaribu utagundua kwamba, vijana wengi wanakosa hali ya kujiamini (self-confidence), katika kutenda mambo. Neno “kujiamini” lina maana ya kuwa na uthubutu binafsi juu ya mambo pasipo kuwa na hofu wala woga na bila kutegemea msukumo kutoka kwa watu wengine. Utakutana na kijana ana uwezo mkubwa wa kufanya kitu fulani ama anayo talanta fulani lakini hana ujasiri wa kukiwasilisha kile alichonacho kwa ufasaha mbele za watu. Hili ni tatizo kubwa sana na ni changamoto hasa kwa asilimia kubwa ya vijana wadogo ambao bado wanakua na kama watapata kukua huku wakiwatazamia wao kama mfano wa kuigwa.
Mchoro rahisi unaoeleza taswira kubwa ya andiko hili
Hii asilimia ya sasa ya vijana ambao wanaonekana kufanya mambo makubwa yanayogusa taifa kwa namna mbalimbali ni ndogo kulinganisha na asilimia kubwa inayobaki bila kusikika kutokana na kushindwa kupaza sauti zao na wakasikika kwenye jamii na hatimae kuwa na manufaa kwa taifa.
Chanzo kikuu cha tatizo hili ni malezi ya hawa vijana, kutoka kwenye familia zao walizokulia na pengine walezi na walimu ambao wanapata nafasi kubwa ya kuwajenga hawa vijana pindi ni watoto. Ni muhimu kwa wazazi na walezi kuwajengea watoto wao mazingira mazuri ya kuweza kuwapa uwezo wa kujiamini wao binafsi kama watu ambao dunia ipo tayari kusikiliza maoni na mawazo yao pindi watakapofanya hivyo, kama mtu mwingine yule duniani. Uwezo wa kuamini kwamba unaweza kuwa chochote, sehemu yoyote na mawazo yako ni muhimu na yanaweza kupewa sikio kama wengine ni nguvu kubwa sana. Vijana wengi wamekuwa wanakua huku wakisikia nchi zetu za kiafrika ni masikini na hiyo imekuwa na athari ya moja kwa moja hata katika utendaji wao kama watu wenye jukumu kubwa kwenye taifa, wanahisi kwamba watu wa mataifa mengine ndio wana vipaumbele zaidi na ndio wana uwezo wa kufanya vitu fulani kulinganisha na wao, jambo ambalo linahuzunisha sana.
Sio ajabu kwa sasa kukutana na kijana ambae amehitimu kabisa mpaka elimu ya juu ya Chuo Kikuu lakini kijana huyohuyo hawezi kujielezea binafsi au kuelezea kwa kina jambo alilosomea ama kuielezea taaluma yake mbele za watu kwa ufasaha. Ni ukweli kwamba sio wote tutaweza kusimama kwenye jukwaa la mamilioni ya watu na kuhutubia jambo fulani, lakini suala la muhimu hapa tunalosisitiza ni kuwa na uwezo binafsi wa kuamini kilicho ndani yako na kuaminisha wengine ili waamini kilichomo ndani yako na kuweza kufanya mambo kwa ufanisi kama mtu yoyote yule duniani.
Kwa kuhitimisha, yote kwa yote, mtu atapata kujiamini kutokana na uzoefu wake binafsi na uamuzi. Hakuna hotuba au mazungumzo yanaweza kuleta mabadiliko ya mara moja. Ni mchakato wa taratibu lakini wa kila mara na ni lazima sote tushiriki.
Itachukua muda lakini ukishaufanikisha, hakuna kinachoweza kukuzuia kushinda kila urefu wa maisha. Na lengo kubwa ni kuitumia vizuri elimu waliyonayo vijana isibaki tu kuwa elimu bali ikawape ujasiri wa kuweza kuchochea maendeleo endelevu kwenye nchi zao za kiafrika.
Vijana wajue wana jukumu zito la kuendeleza rasilimali za nchi, kwa hivyo wanatakiwa kuwa na uwezo na sifa ili wafae katika kutumika kwenye kizazi cha sasa na cha badae ambacho kinawategemea kama kioo. Hivyo kipaumbele kiwe ni kuwaandaa vijana ili waweze kukabiliana na uhalisia wa maisha na hali nzima ya kujitegemea na kujiamini mapema ili wakawe mabalozi bora wa Afrika ulimwenguni.

Upvote
0