Kuchokonoa pua mbele za watu ni tabia inayochefua

Kuchokonoa pua mbele za watu ni tabia inayochefua

Sky Eclat

JF-Expert Member
Joined
Oct 17, 2012
Posts
57,761
Reaction score
216,011
Huyu ni yule mpenzi wako ambae kila ukiongea nae unamuona kabisa ni yule wa kwashida na raha. Leo amekutaarifu kuwa anakukaribisha chakula kwao.

Umetoa ile nguo ya mwisho kabatini ile uliyolipa kwa instalments ili ikutoe aibu pia unaimani ile nguo inakufanya uonekane mtu wa heshima.

Umekaribishwa vizuri nyumbani na ndugu zake wote. Mdogo wake wa mwisho ana kipaji cha kupiga picha na amekabidhiwa camera ili kumbukumbu ta leo isipotee.

Unayo tabia ya kufokoa pua kutoa mabubu bila mwenywe kujielewa hasa unapokuwa nervous. Baadhi ya picha ziatoka mwenyewe uko busy na pua yako. Unaonyeshwa unatamani ardhi ipasuke, unaziwahi ili uzichane. Mpenzi wako anakujibu baba pia amezipenda hizo na amechukua copy za kwanza amezihifadhi.

Hivi unapofokoa kwa vidole una tumia mikono hiyo kusalimia watu, huoni kuwa unasambaza germs?
Kwakweli hii tabia inakera sana kwa wanaume na wanawake.
 
wengine kuminya pua ni namna ya kuongea..ata nyerere alikuwa akishika pua
 
Nisaidie dawa mkuu, maana nshaivuta imerefuka kuzidi hata ya kagame, najikutaga tu jamani dah comments za humu zimenifanya nijisikie vibaya
 
Inakera,ila ujue kila mtu ana kitu anafanya akiwa peke yake na anachukulia kawaida,
Sasa unapojisahau mbele za watu Ndio kuaibika huko

Na ndio maana wataalamu wa afya wanatuambia tunawe mikono kwa sabuni nyakati muhimu yaani baada ya kutoka kazini, mazoezi. Ukipanda daladala ama kushuka eneo la kazi ama nyumbani cha kwanza ni kunawa maji kwa sabuni achilia mbali wakati wa kula yaani hata ukikutana na karanga ama mahindi

Tatizo linabaki kwa yule anaefanya hadharani na kwa akili ya kibinadamu huwa inachefua haswaaa though kuna mengine machafu zaidi yanafanyika kwa kificho.

Kwa tatizo hili la pua wengi tunadhani chooni ni sehemu ya kwenda haja kubwa na haja ndogo kumbe inaweza ikawa kama umebanwa chafya ambayo unaweza kui-control ama kugusa hizo pua ndani basi unaingia maliwatoni kujiweka safi kwa kupiga chafya za kutosha na mambo mengine mengi
 
Hiki ndio kitu kilinifanya niwe najipikia mwenyewe kile kipindi naanza maisha yangu..

Kila nikitaka kula au kunywa chai nawaza aina ya vitafunwa na tabia ya kuchokonoa pua na masikio kwa vidole.
 
Your absolutely right, it's a very bad habit.
At one time while in Oslo someone asked me if picking nose is African way of life!
But while your wondering with nose picking, unfortunately in Oslo spatting is a common habit,it is really disgusting but nobody care's.
 
Back
Top Bottom