KWELI Kuchoma mifuko ya plastic na ndala kunaweza kumfukuza Nyoka ndani ya nyumba kwa muda mfupi ambao harufu itakuwepo

KWELI Kuchoma mifuko ya plastic na ndala kunaweza kumfukuza Nyoka ndani ya nyumba kwa muda mfupi ambao harufu itakuwepo

Taarifa hii imethibitika kuwa ya kweli baada ya kufanya tathmini ya kina
Nimepata kusikia kuwa endapo nyoka akiingia ndani ya makazi ya mtu au nyumba basi njia bora zaidi ya kumtoa bila kumdhuru ni kuchoma kitu cha plastic kama mifuko au ndala na ile harufu inamfanya atoke ndani. Je ni kweli dhana hii?
1722328060558.png
Je, ni kuchoma mifuko ya plastic au bidhaa iliyotengenezwa na plastic kunaweza kumfanya nyoka atoke ndani ya nyumba?
 
Tunachokijua
Nyoka ni reptilia wasio na miguu. Kuna takriban spishi 3,000 duniani, wako kwenye mabara yote nje ya Antaktiki na Aktiki.

Kama ilivyo reptilia wengine nyoka nao wana damu baridi na ngozi ya magamba. Wote ni wala nyama na spishi mbalimbali hutumia sumu kwa kuwinda lakini nyoka walio wengi hawana sumu wanashika windo kwa miili yao au kwa mdomo tu.

Snake_Nina-B_Shutterstock.jpg
Zimekuwepo hoja mbalimbali zinazosema kuwa nyoka akiingia ndani ukachoma mifuko au vitu vya plastiki basi nyoka aliyepo humo ndani akipata harufu hiyo atakimbia ndani ya nyumba hiyo.

Baada ya Mdau wetu kutaka kufahamu pia kuhusu ukweli wa Hoja hii Jamiicheck imefatilia suala hili kwa kuzungumza na Mkufunzi wa Chuo cha Usimamizi wa Wanyamapori Mweka, Tito Lanoy ambaye ameeleza kuwa hoja hiyo ina ukweli japo ina mafanikio kwa muda mfupi kwa kuwa mara tu harufu inapokwisha nyoka huweza kurudi tena eneo hilo kwa kuwa kinachomkimbiza ni hiyo harufu tu kwa kuwa inamuathiri kiafya.

"Hiyo hoja inakuwa na mafanikio kwa muda mfupi, kwa sababu hiyo harufu ikiishaisha nyoka atarudi tena alipokuwa na ni aina zote za nyoka huathiriwa na harufu.

Kinachosababisha nyoka kuondoka au kukimbia ni ile harufu, nyoka akisikia harufu ya vitu vya plastiki huwa anapata karaha, kwa kuwa nyoka ananapata athari/ karaha kiafya akisikia harufu, harufu za aina nyingi tofauti tofauti kama madawa ya kuulia wadudu, mfano wa dawa zinazopulizwa kwenye pamba kahawa kuua wadudu, ile sumu, harufu huwa inawakimbiza au kuwaua nyoka, na harufu nyingine zinawaathiri kiafya.

Kwa hiyo ili kujilinda ni kuweka mazingira ya nyumba kuwa masafi ili kuzuia nyoka kuingia. Milango iwe inashika vizuri chini, mara nyingi sehemu za chini ya mlango ukiwa haushikamani na sakafu nyoka huweza kupenya na kuingia ndani. pia na Madirisha yawe yanashika vizuri na yawe na wavu ili kuzuia wadudu kuingia ndani.

Pia, Ndani maji kama yapo kwenye ndoo yawe yanafunikwa kwa sababu nyoka anaweza kulazimisha kuingia ndani kutafuta maji.


images
Pia vyakula kama unga, nafaka kama mchele, mahindi viwe vinafunikwa kwenye vyombo yenye mfuniko kwa sababu vitavutia panya, japo nyoka hali unga, mchele wala mahindi ila anakula panya, hivyo nafaka zikiwa wazi zitavutia panya na nyoka anakula panya hivyo atalazimisha kuingia kutafuta panya iwapo nyumba ina panya.

Pia mazingira ya nje kusiwe na vichaka karibu na nyumba, mashimo yafukiwe karibu na nyumba ili kusiwe na uwezekano wa nyoka kuvutiwa"
Kwa hiyo, nichome hizo plastiki mfululizo ili kila akija anaishia njiani. Mimi nitavaa barakoa kuzuia sumu ya plastiki.
 
Shukrani sana kwa mrejesho
 
Back
Top Bottom