Kuchukua mkopo benki na kujengea nyumba ni jambo jema lakini hasara yake ni kubwa

Kulipa kodi 400000 kuna reflect kipato chako. Maisha ya sasa vijana tunavipato vidogo. Ukiwa na uwezo wa kulipa hiyo kodi, ni bora ukope ili pesa uliyotakiwa kulipa kodi ifanye marejesho.
Nakubaliana na wewe kabisa, unalipa kodi laki 400,000 kwa mwezi, unashindwa nini kukopa na marejesho yakawa hiyo gharama ya kodi unayolipa kila mwezi?
 
Kama ni mwajiriwa hasa wa serikali, unatake home ya tsh. mil.1.2- 2. na unalipa kodi ya pango ya tsh.250000 - 400000. Nakushauri kopa na hicho kiwango unacholipa kodi kwa mwezi ndo kiwe marejesho ya mkopo bank, utanishukuru baadae. Hata kama unamshahara mkubwa, kundunduliza fedha eti upate ya kutosha kujenga huku tayari unamajukumu mengi ni uongo, utajenga nyumba ukiwa umezeeka na unakaribia kustaafu.
 
Unadhani wanaochukua mikopo hawapendi kujiwea akiba? 😆😆😂.

Huo ujasiri ni wa wachache sana.
 
Mimi Kukopa sijawahi kwanza naogopa mikopo ila ni bingwa wa.ubahili na saving,Huwa nasevu 60% ya kipato change.
 
Kiujumla kama una salary take home ya hicho kiasi Kukopa ni bora maana unaweza pata pesa nyingi ya kufanyia masuala yako kuliko kudunduliza kwa saving.
 
Watu wa Dar mna tabu na maisha magumu Sana yaani kiwanja mil.40? Ni City centre au residential plots za kawaida?
 
Salary ikiweza kukudhamini kupata hizo 50 basi atakuwa na kaposition au ni senior staff..

Lakini salary za Kukopa sijui mil 2-5 kwangu ni useless kama unaishi mjini maana tija yake ni ndogo ila kwa walio Vijijini kwenye kilimo inawatoa fasta.
 
Urahisi wetu unatokana na upatikanaji wa kiwanja,tofauti na Ulaya ardhi ni ishu ila kwenye materials za ujenzi ni simple.

Pia si unajua no regulations tunajenga kiholela na tunajenga vibanda sio nyumba za standards
 
Kudunduliza ni majanga, gharama za maisha zinaongezeka kiasi kwamba huwezi sema natafuta milioni 10 nije kujenga 2025 .
 
Nenda Wizara ya Ardhi gorofa ya 9, utapata maelezo yote, lazima uwe mfanyakazi wa UMMA. Ni 2% interest only, kuna benefits nyingi sana kwa wafanya kazi!
Ukijenga kwa mkopo wa mortgage ni nafuu kuliko mkopo wa commercial banks.
 
Inategemea na taasisi uliko,mimi ni junior staff kwenye taasisi x na uwezo wangu wa kudunduliza kwenye salary na posho unanipa Kati ya mil.8-10 kwa mwaka so naweza ku skip mikopo kwa sababu pia naiogopa..
 
Unatak kujenga hoja gani ? Kuwa mfumo wa mortgage haufai Tz?
 
Wadanganye wenzio nimekopa nimejenga kanyumba kangu na kausafiri kangu navimba tu mjini sidaiwi na mtu zaidi ya benki na Wala sijali na siwazi halafu silingi Wala Nini majirani wananionea tamaa kopa Fanya Mambo ya maana usishinde bar[emoji2957][emoji2957][emoji2957][emoji2957][emoji2957][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]
 
Nyie pigeni kalele tutakutana uzeen maisha ni nyumba.kama uko single endelea kupanga lakin Kama upo double napita miaka 3 unakuja huku unatembea labda huwe hanisi.
Nyumban ni furaha
Nyumba Ni comfortable
Nyumba Ni heshima ya ndoa
Nyumba inaokoa gharama zisizo na lazima.
Kijana wew fuata mkumbo utaamuka jua limeshazama.
Miaka 3 mi nne kitu gani?? Wewe una skill ya kurun biashara itakayotoa faida ya nondo 50@ 27000/= cement alreast mifuko 150@ 16000/= bado kiwanja....
Acha uzembe kopa ujenge upate heshima ya ndoa
 
Kiujumla kama una salary take home ya hicho kiasi Kukopa ni bora maana unaweza pata pesa nyingi ya kufanyia masuala yako kuliko kudunduliza kwa saving.
"...maana unaweza pata pesa nyingi ya kufanyia masuala yako ...." Ss hapo pesa itatoka wap? mana utakua na kaz mbili marejesho + kodi that's means utaendelea kujibana tena sana.

Sijui... Labda mm cjui hesab lakin nachokiona km unaweza kulipa deni la mkopo kwa MSHAHARA WAKO that's means unaweza kujenga bila hata kuhitaji huo MKOPO (kwa kuptia savings / kudunduliza) bila kua na stress za marejesho, cjui naeleweka hapo?!.
 
Utajenga plus biashara afu faida utatumia kufanya marejesho,kula na kukuza biashara.

Tunaamini kwamba biashara yenye mtaji mkubwa/mzunguko mkubwa ina returns kubwa pia.
 
Kuna tofauti kati ya biashara na uwekezaji

Japo zote zinahusu capital na revenues.

I prefer uwekezaji coz ninakuwa huru kufanya michakato mingine ,my money works for me while i ain't around.

Siku za mwanzo uwekezaji una returns ndogo ila kadri siku zinavyozidi kwenda value inaongezeaka na returns pia zinakuwa

Anko wangu mmoja alinunua kiwanja mbezi beach miaka ile ya 90 sidhani hata milioni moja ilifika.

Akajenga nyumba nzur ya kisasa nikikadiria kwa bei wakati upe labda aound 50-60m ila leo nyumba ilipo hapo mbezi beach akitaka aiuze hakosi around 500m

Alichofanya kaivunja vunja na kwa staili ya kupangisha chumba sebule jiko choo cha ndani.

Wapangaji wanapagombea wanalipa advance kabisa anakunja kila unit 600k kwa mwezi ana katoa unit 6 pale maana lilikuwa jumba kubwa na lote limejaa

Yeye kahamia bunju huko alijenga ingine.zamani


Ndani ya miaka 3-4 anakula faida tu akiwa havuji jasho akiwa kalala usingizi au anakunywa wine home kwake

3.6m per month sio ndoho
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…