Mikopo tunayokopa benki hapa nchini Tanzania zina riba kubwa sana kitu ambacho hufanya watanzania wengi kutofaidika sana na mikopo hiyo. Kwani kuna benki hutoza riba zenye faida ya asilimia 18%-23%.
Watanzania tulio wengi tukishachukua mikopo hiyo hukimbilia kuninua uwanja na kuanza kujenga nyumba, kisha huishi maisha ya shida sana kwa kipindi cha miaka minne mpk mitano. Wapo wengine hukimbilia kununua gari ili waonekane hapa mjini lakini hata uwanja hawana, mikopo hiyo ya benk ina mambo sana.
Wazo la kukimbilia kujenga nyumba kwa kutumia mkopo ni kujitengenezea maisha ya dhiki sana kwani makato huwa makubwa na kufanya kila siku kukimbizana na madeni yasiyoisha. Ushauri wangu na maoni yangu kama unataka kujenga au kununua gari ni bora ujiwekee mkakati binafsi unaweza amua kila mwezi kujiwekea kiasi fulani ambacho unatumia kwaajiri ya ujenzi, utafanya hivyo bila riba wala hasara yeyote.
Mikopo ya benki ni yakuwekeza katika biashara na ili ziongeze kipato na biashara hiyo irudishe mkopo huo yenyewe bila we kuathiri mapato ya kazi yako.
Kuweka pesa kila mwezi au kila sikunkutokana na maingizo yako inawezekana, kikubwa ni uamuzi thabiti na kujiwekea malengo na kuhakikisha unayafikia malengo yako.
Huu ni ushauri na maoni yangu jinsi ninavyoona namna ya kutumia mkopo wa benk kwa faida, lakini hata kama mtu akajenga nyumba ya biashara ni sahihi lakini nyumba ya kuishi ni safi sana lakini kuna hasara kubwa ndani yake.
Mtoa mada wacha uoga ktk maamuzi.
Mkopo kama mkopo kwa yule anayekopa huwa analengo fulani. Kwa ajili ya kufanikisha kitu fulani.
Sisi watanzania hatujazoea kufanya maamuzi ambayo watakao nufaika ni kizazi chako wala sio wewe.
Lzm ujiulize mkopo unasaidia nini?
Kwa yule aliyechukua mkopo na kujenga nyumba ,faida aliyoipata kutokana na mkopo sio nyumba. Ameokoa muda ktk kufanya maamuzi ya kujenga nyumba.
Ule muda ambao umeusavu ktk kujjijengea nyumba utautumia kufikili kitu kingine cha kufanya ili kukuongezea kipato.
Milioni hamsini unapata kwa siku moja ukichukua mkopo.
Na endapo ungekuwa kila mwezi unaweka laki tano. Itachukua miaka 8 na mwezi moja kutimiza milioni hamsini.
Ndani ya miaka 8 na mwezi mind yako ipo ktk nyumba.
Tuchukulie mwaka huu 2017 ndio umetimiza hiyo pesa baada ya kuichanga kwa kipindi cha miaka 8 na mwezi moja.
Na mimi mwaka 2009 nilichukua mkopo milioni 50 nikajenga nyumba.
Sasa linganisha nyumba yangu niliyoijenga 2009 kwa mkopo .na nyumba yako uliyoijenga kwa kuchanga pesa kwa miaka 8.
Kwanza ili ujenge nyumba utapata plot 20x20 labda kwa milioni 6.
Wakati mimi niliyechukua mkopo 2009 hiyo milioni 6 nina zaidi ya kiwanja cha mpira.
WATU WANASEMA CHEZEA PESA SABABU ZINAKUJA NA KUONDOKA NA KUJA TENA.
USICHEZEE MUDA .
KWA HIYO MKOPO HUOKOA MUDA UKIUTUMIA VIZURI .mfano kujenga nyumba au kujiendeleza kibiashara kama si mfanyakazi