ISIS
JF-Expert Member
- Apr 20, 2016
- 96,073
- 858,551
Amen Rathanks
Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Amen Rathanks
Ingia kwenye website yao!Hata mikoani ipo? Mm nipo Iringa inapatikana huku?
Au katika vitengo vyao!Hata mikoani ipo? Mm nipo Iringa inapatikana huku?
Naomba link tafadhali.Ingia kwenye website yao!
Hii njia ndio nzuri-juzi kuna jamaa moja friend of mine alikuwa na 400M bank zake mwenyewe lakini alikwenda kukopa 200M NIlishangaa nakuuliza kwa ninj unafanys hivyo siuchukue hela ulizo nazo bank utumie akaniambia hii ndio njia sahihi
Google MINISTRY OF LANDS HOUSING AND URBAN DEVELOPMENTNaomba link tafadhali.
+255 657 685 268 WhatsApp!Mikopo tunayokopa benki hapa nchini Tanzania zina riba kubwa sana kitu ambacho hufanya watanzania wengi kutofaidika sana na mikopo hiyo. Kwani kuna benki hutoza riba zenye faida ya asilimia 18%-23%.
Watanzania tulio wengi tukishachukua mikopo hiyo hukimbilia kuninua uwanja na kuanza kujenga nyumba, kisha huishi maisha ya shida sana kwa kipindi cha miaka minne mpk mitano. Wapo wengine hukimbilia kununua gari ili waonekane hapa mjini lakini hata uwanja hawana, mikopo hiyo ya benk ina mambo sana.
Wazo la kukimbilia kujenga nyumba kwa kutumia mkopo ni kujitengenezea maisha ya dhiki sana kwani makato huwa makubwa na kufanya kila siku kukimbizana na madeni yasiyoisha. Ushauri wangu na maoni yangu kama unataka kujenga au kununua gari ni bora ujiwekee mkakati binafsi unaweza amua kila mwezi kujiwekea kiasi fulani ambacho unatumia kwaajiri ya ujenzi, utafanya hivyo bila riba wala hasara yeyote.
Mikopo ya benki ni yakuwekeza katika biashara na ili ziongeze kipato na biashara hiyo irudishe mkopo huo yenyewe bila we kuathiri mapato ya kazi yako.
Kuweka pesa kila mwezi au kila sikunkutokana na maingizo yako inawezekana, kikubwa ni uamuzi thabiti na kujiwekea malengo na kuhakikisha unayafikia malengo yako.
Huu ni ushauri na maoni yangu jinsi ninavyoona namna ya kutumia mkopo wa benk kwa faida, lakini hata kama mtu akajenga nyumba ya biashara ni sahihi lakini nyumba ya kuishi ni safi sana lakini kuna hasara kubwa ndani yake.
Kinachoongelewa hapa ni maamuzi.Hajaamua kujenga ila akiamua dakika 0 tu jumba hiloooo
Kupanga ni kuchagua,,ungenisoma kuanzia mwanzo nadhan ungenielewa mm ni mtu wa namna gan,,,sio kila mtu nyumba ni kipaumbele chake,,mwngine bila kua na mikondo zaid ya mitano au saba ya fedha bado hawez kufikiria kujenga wala wazo hilo hana,,hiyo kodi anayolipa anauwezo wa kujenga lakin bado sio kipaumbele chake,,wapo watu wana nyumba zaid ya tatu lakin wala hawakai wao na wao wamepangisha vile vile wanaish sehem nyingine kabsa.. Ukiamua kujenga,ni maamuz ya mjengaji na mipango yake,siwez mdharau mtu aliejenga na siwez mdharau mtu mwwnye kipato ambae hajajenga vile vile,,hizo risk unazosema mikondo ya fedha inaweza kugeuka na pia usisahau mikondo mingine haigeuki vile vile.. So usiseme nina dharau maana najua faida na hasara ya kukopa na kati ya wajanja wa kukopa naiman mm ni mmoja wapo...Kinachoongelewa hapa ni maamuzi.
Kuna kanuni nadhani haibadiliki hii. Hii kanuni inafanana sana na kuota ndoto. Unakuta mtu anafunguliwa neema ya kipato kikubwa.
Hawezi kutuliza akili yake na kupanga vipaumbele vyake kwa weledi, matokeo yake ni kufuja pesa ama pato lake kwa starehe za kishamba zisizo kichwa wala miguu ama hasa kugawa ovyo na kutapanya!
Akitaka kufanya jambo lolote la maendeleo, huwa hafanyi, badala yake huishia huulizia tu gharama na kuingiza dharau za uwezo mkubwa wa kumudu gharama, kama ulivyokomenti wewe. Kwamba nyumba, mf: nyumba ya mil.20 anauwezo wa kuinunua siku moja kwa kuwa kipato chake ni zaidi ya kiasi hicho. Haamui, anaendelea na maisha ya pangoni na kutumbua pesa, akiishi kwa matumaini.
Lakini unapita unavuma upepo wa matatizo yasiyo mbele wala nyuma, kipato kinapotea na uwezo wa kufanya uliyokuwa unayaona ni rahisi kuyafanya huwezi kuyafanya tena.
Mdomo unamaringo, waweza kujenga ghorofa bila hata senti tano, inabakia tu hadithi, enzi zetu enzi zetu. Enzi zenu ulifanya nini la maana ili tulifanye "shamba darasa"?
Uwezalo kulifanya leo usingojee kesho kwa kusema utalifanya tu kwa kuwa unazo. Mawazo hayo yamepitwa na wakati.
kweli kabisa.Mikopo tunayokopa benki hapa nchini Tanzania zina riba kubwa sana kitu ambacho hufanya watanzania wengi kutofaidika sana na mikopo hiyo. Kwani kuna benki hutoza riba zenye faida ya asilimia 18%-23%.
Watanzania tulio wengi tukishachukua mikopo hiyo hukimbilia kuninua uwanja na kuanza kujenga nyumba, kisha huishi maisha ya shida sana kwa kipindi cha miaka minne mpk mitano. Wapo wengine hukimbilia kununua gari ili waonekane hapa mjini lakini hata uwanja hawana, mikopo hiyo ya benk ina mambo sana.
Wazo la kukimbilia kujenga nyumba kwa kutumia mkopo ni kujitengenezea maisha ya dhiki sana kwani makato huwa makubwa na kufanya kila siku kukimbizana na madeni yasiyoisha. Ushauri wangu na maoni yangu kama unataka kujenga au kununua gari ni bora ujiwekee mkakati binafsi unaweza amua kila mwezi kujiwekea kiasi fulani ambacho unatumia kwaajiri ya ujenzi, utafanya hivyo bila riba wala hasara yeyote.
Mikopo ya benki ni yakuwekeza katika biashara na ili ziongeze kipato na biashara hiyo irudishe mkopo huo yenyewe bila we kuathiri mapato ya kazi yako.
Kuweka pesa kila mwezi au kila sikunkutokana na maingizo yako inawezekana, kikubwa ni uamuzi thabiti na kujiwekea malengo na kuhakikisha unayafikia malengo yako.
Huu ni ushauri na maoni yangu jinsi ninavyoona namna ya kutumia mkopo wa benk kwa faida, lakini hata kama mtu akajenga nyumba ya biashara ni sahihi lakini nyumba ya kuishi ni safi sana lakini kuna hasara kubwa ndani yake.
Inaelekea anaishi kwenye nyumba ya familia. Hajui hata nyumba ni biashara? Hajui ardhi inaongezeka thamani siku hadi siku? Nimekopa nikajenga, nikakopa tena nikajenga. Naenda kukopa tena nijenge. .Nilikuwa napanga Nyumba nalipa 400000 kwa mezi,nimokopa nikajenga Nyumba nanimehamia sina shida kabisa uache uongo we we,kukopa kunasaidia sana tu
Hili jambo tunaongelea linaendana na watu wenye maisha.
Maana yake uwe na kipato rasmi kisichoyumba. Bussiness ama ajira.
Ninachoshangaa wewe kuogopa kukopa! Hiyo ni kasoro yenye doa. Utakuja kushituka upo kambabu na uwezo wa maamuzi ya kufanyia mijadala pendwa kama hii utakuwa hauna.
Deni ama mkopo halali utaishije kwa stress?
Na hauwezi kukopa hadi kibubu kikakauka, haiwezekani. Unapoanza kuomba mkopo, lazima upewe masharti ya 1/3 na kuambatanisha salary sleep kwenda kupimwa, maana yake uachie hela ya kula na matumizi muhimu.
Chunguza kwa kutafakari, mtu anayekopa, mfano mkopo wa miaka mitatu, akafanya mambo yake makubwa. Je wewe unayeweka akiba, ili usimame mwenyewe, mtalingana nae akiishakumaliza makato yake? Hilo angalizo lifanyie kazi jibu utalipata.
Halafu mikopo ama madeni ni mfumo wa kidunia, hiyo ni fursa.
Wapo watu hata akitaka kukopa hawezi kukopeshwa kwa kuwa hana dhamana.
Hii njia ndio nzuri-juzi kuna jamaa moja friend of mine alikuwa na 400M bank zake mwenyewe lakini alikwenda kukopa 200M NIlishangaa nakuuliza kwa ninj unafanys hivyo siuchukue hela ulizo nazo bank utumie akaniambia hii ndio njia sahihi
Sehem nzur ni zip mkuu
Na mkopo unakatwa shilingi ngapi kwa mwezi?Nilikuwa napanga Nyumba nalipa 400000 kwa mezi,nimokopa nikajenga Nyumba nanimehamia sina shida kabisa uache uongo we we,kukopa kunasaidia sana tu
unaishi maisha ya hofu.. kwa hiyo una react sababu ya hofuuu😀😀.nimejenga nipo kwangu hata nikiishi maisha magumu kwa kipindi cha miaka kadhaa, ila nina amani sidaiwi kodi wala kusumbuliwa, uoga wako ndo umasikini wako utaishi nyumba za kupanga hadi lini!?,
Huyu anajenga nyumba za kupangisha hiyo ni rasilimaliii..Hujamuelewa mtoa mada. Anasema tu nyumba ya kuishi mwenyewe tuu haingizi chochoteKuna jamaa yangu ana nyumba 5 mpaka ss kutokana na mikopo,
Mwanzon alikuwaga anajenga then aksihamaliza boma anakopa na kufanya finishing then anapangisha, mkopo ukiisha anafanya the same. mwaka jana amekopa 50M/5yrs akamaliza ujenzi wa nyumba within 3month na kuipangisha. Anasema kwa kusaidia na nyumba nyingine mkopo wake utaisha after 3/3.5yeras instead ya 5 years
Hivi sasa anajidunduliza atafute eneo kubwa aje kujenga nyumba 3 houses kwa mikopo hiyo hiyo ( kwa dhamana ya one house plus salary yake)
Advantage aliyonayo ni kuwa anakopa kutumia mshahara then makato ya salary plus kodi ya hizo nyumba ndo zinamsaidia kulipa.
Sofar naona yuko vzr, kama anapata 1.2M/month na i think its a good business model
Mkopo wa kurejesha laki tano kwa mwezi hauzidi m 15 ina maana hiyo m15 nyumba ikamilike na ahamie...Hebu piga mahesabu tena vizuri. Otherwise usem tu aezeke na kuhamia bila hata madirisha 😀😀😀Umeeleza vzuri. Ila kuna mtu analpa labda 500,000 kodi ya nyumba kwa mwezi. Kwahyo akpata mkopo wa muda mrefu kwa mrejesho wa 500,000 kwa mwezi huyo kwake ni faida kubwa.