Kuchukua mkopo benki na kujengea nyumba ni jambo jema lakini hasara yake ni kubwa

Kuchukua mkopo benki na kujengea nyumba ni jambo jema lakini hasara yake ni kubwa

Kwa yeyote mzoefu, atapingana kwa kiasi flani na ajenda hii.
Mtu umefanya kazi yenye kukuingizia kipato cha wastani na unajiwekea malengo, lakini hakuna ulichoambulia, bado unaishi pangoni, what do you expect?
Pata hela ya mkupuo jenga, hamia.
Madeni yana msimu yataisha na utabaki na njengo wako.
Kukopa na kufanya biashara yahitaji uzoefu pia, hilo silishauri kwa kuwa sina uzoefu nalo.
Umenena vyema mkuu.
Kuna watu wamejenga nyumba zao kwa pesa zao wenyewe. But wakaona waende bank wakope kwaajili ya biashara na kuweka hati ya nyumba kama dhamana. Biashara imekufa na nyumba imeenda. Maisha hayana formula ni kujpanga na kujua uwezo wako unafika wapi.
 
Jaman tusidanganyane kwa vipato vyetu vya mishahara sisi watumishi wa chini huwezi kusonga Mbele bila kukopa ingawa mikopo ni ya kinyonyaji kutokana na riba kubwa lakini hamna namna ili uwe na nyumba yako lazima ukope ununue Gari au hata kuanzisha biashara lazima ukope halikwepeki maana mshahara ni mdogo hutaweza kufanikisha hayo
 
Ha ha ha umenifurahisha sana,muda mwngine kudaiwa kuna kufanya uongeze juhud zaid ya kutafuta,ila nyumba yako inafaida gan kama unaishi na maisha ya shida na stress... Sio kila aliepanga hawez kujenga,kuna aliejenga ana maisha magumu na stress kuliko aliepanga.. Nyumba ni nzur,kwako ni kuzur na heshima,lakin kuliko nijenge kwa mawazo na kuanza kufikiria maden,ukiangalia nyumba hata haijaisha,madirishan umeweka mabox,chin hata floor haijawekwa eti kisa tu nami nionekane nina nyumba lah siwez,, kujenga ni process inayokwenda taratibu kulingana na kipato chako,kama mfanyakaz kopa,weka biashara,zungusha ukipata faida nunua vifaa kdgo kdgo mwsho unakuta umepiga hatua bila stress wala kuumiza kichwa.. Japo siwez mdhadau yyte mwenye kwake. Naheshim pia mawazo yako
Hili jambo tunaongelea linaendana na watu wenye maisha.
Maana yake uwe na kipato rasmi kisichoyumba. Bussiness ama ajira.
Ninachoshangaa wewe kuogopa kukopa! Hiyo ni kasoro yenye doa. Utakuja kushituka upo kambabu na uwezo wa maamuzi ya kufanyia mijadala pendwa kama hii utakuwa hauna.
Deni ama mkopo halali utaishije kwa stress?
Na hauwezi kukopa hadi kibubu kikakauka, haiwezekani. Unapoanza kuomba mkopo, lazima upewe masharti ya 1/3 na kuambatanisha salary sleep kwenda kupimwa, maana yake uachie hela ya kula na matumizi muhimu.
Chunguza kwa kutafakari, mtu anayekopa, mfano mkopo wa miaka mitatu, akafanya mambo yake makubwa. Je wewe unayeweka akiba, ili usimame mwenyewe, mtalingana nae akiishakumaliza makato yake? Hilo angalizo lifanyie kazi jibu utalipata.
Halafu mikopo ama madeni ni mfumo wa kidunia, hiyo ni fursa.
Wapo watu hata akitaka kukopa hawezi kukopeshwa kwa kuwa hana dhamana.
 
Kusema unadunduliza ela ya kununua Gari au kununua kiwanja ni kitu kigumu kidogo coz utapatwa na mahitaji mengine ambayo utatumia hiyo hiyo ela unayosema unadunduliza

Cha msingi ni kutokuwa na source of income moja tu, ili uweze kufanya mambo yako kwa wakati,pia Saccos ni nzuri maana zina riba ndogo sana

Bank wacha wakopeshane wenyewe tu unaweza kufa siku si zako
 
Hivi unajua akili za kijasiriamali haziko sawa! Hivi unajua kama huna akili ya biashara hata ukipewa mil 200 haiwezi kukusaidia kuongeza kipato Zaid utaingiza hasara tu? Watumishi wengi hawana muda wa kusimamia biashara zao unalijua hilo, nawashaur watumishi kopeni mjenge nyumba na mnunnue magari, mtaishia kupanga kwa huyu jamaa!!!
Umeongea kweli tatizo tunafikiri kila mtu ana nidhamu ya pesa. Kuna mtu akipewa milioni 10 anaweza kuidhalisha kama unavyosema kuna mtu hata akipewa milioni 200 itapotea tu.
 
Kila mtu achukue mkopo afanyie lile analoona linamlipa zaidi... Kwa aliyeamua kununua ardhi kwa hela ya mkopo sawa, kwa aliye na ardhi akaamua kujenga sawa tu, na aliyeamua kuendelea kulipa kodi ya nyumba lak 2 hadi 4 kwa mwezi halafafu mkopo wake akaamua kufanyia biashara badala ya kujenga ni sawa pia.. Usiige kitu usichokijua.
Umeongea point mkuu. Kila mtu anakitu kinachompa furaha na anachoona kwake ni sawa. Unachona ni sahihi kwako sio lazima mwenzako pia aone ni sahihi. Tumeumbwa tofauti.
 
Raha ya maisha sio lazma uwe umejenga nyumba,,raha ya maisha ni kufanikisha mengi ambayo unayataman,na kuyaishi,sio kila mtu ana taman kua na nyumba,mi naamin yyte anaejua kutafuta hela na mwenye maono ya mbali nyumba sio kipaumbele chao.. Nyumba ni kitu cha mwsho kuwa nacho,ila unaweka mikondo ya hela ili hela ianze kukufanyia kaz baada ya wewe kutumia muda mwngi na akili na nguvu zako kuitafuta sasa inafiki kipind hela inakutumikia wewe.. Unaiamuru na inakupa majibu mubashara, mi namtetea mtu ambae anaweza kupanga laki sita kwa mwez kwenye appaintment then chin ana gar ya milion30-40,huyu akiamua kujenga anajenga tu lakin kujenga sio kipambele chake..

Narudia nyumba inakusaidia nn kama umewekeza nguv zako zote kwenye kujenga halaf kula kwako kumekua kwa shida? Nyumba ina maana gan kama umekopa ukajenga na mshahara wako unakatwa unabaki kulalamikia serikali? Kujenga kuna maana gan kama unalala njaa? Wekeza hela akilini ili akili ikujazie hela mfukoni hapo unaweza nunua cchte ukipendacho. Bado nasema siwalaumu wanaokopa kwa ajili ya ujenzi
Gari m40,kodi mwezi laki 4 unalipa kwa baba mwenyenyumba, we huna hata kajumba ka vyumba Vitabu. Labda hizo pesa zitakuwa za mazingaombwe unatimiza masharti.

Nirahisi kumwelewa sana mtu anayeishi nyumba ya kupanga wakati ye amejenga maana huyu anaishi kwa malengo fulani
 
Gari m40,kodi mwezi laki 4 unalipa kwa baba mwenyenyumba, we huna hata kajumba ka vyumba Vitabu. Labda hizo pesa zitakuwa za mazingaombwe unatimiza masharti.

Nirahisi kumwelewa sana mtu anayeishi nyumba ya kupanga wakati ye amejenga maana huyu anaishi kwa malengo fulani
Hajaamua kujenga ila akiamua dakika 0 tu jumba hiloooo
 
Angalau kujenga.Mi nikikopa 3,000,000.Nkaenda kuoa na kulipa mahari.Hua siwezagi kuweka hela.Makato yalikua ya miaka3.Nliishi kwa ugumu ila deni liliisha.
aisee ilikuwa siku baada ya marejesho unatandika dudu kwa wife mpaka anajua deni limepunguzwa. mie nilikopa vikoba nireplace michango ya harusi nilizungusha kwa biashara aisee ctasahau. mikopo inasaidia ila kwa malengo mema
 
h
Kwani Ukikopa na kuanzisha biashara una uhakika kuwa hiyo biashara haitakufa na kukutia hasara?

Kuna mtu alikopa 5m akanunua bajaji, ndani ya wiki moja bajaji ikatekwa na kuibiwa, na haikuwa na comprehensive insurance!!
ahahahahah atakuwa sawa na yule aliyempgia kura raisi wake
 
Si kweli maneno yako maana inategema kama wewe ni mfanya kazi wa umma unaweza kuchukua mkopo according to your salary au ukaenda Wizara ya Ardhi wanatoa mkopo wa interest ya 2% , Private Sector ninaamini pia kuna njia ya kupata mkopo bank .... ukiwa na nia ya kufanya jambo mtu yeyote asikukatishe tamaa! Don't fear anything but FEAR itself,
maelezo zaidi kwenye mkopo wa ardhi wizarani..
 
Kweli mkuu ishi vzuri hata ka kupanga watoto wasome vizuri mambo mengine yatafuata huko ulaya umeona nani anajenga?
Ulaya watu binafsi hawajengi sababu hakuna ardhi isiyomilikiwa. Ardhi zote zimekwisha milikiwa lakini wananunua nyumba kwa mkopo kutoka benki (mortgage) kupitia kampuni ambazo zinajenga nyumba hizo na kuziuza kwa watu. Kama NHC inavyofanya bongo hivyo malengo ni yale yale mkuu. Tofauti ya ulaya mkopo wake wa nyumba kulipa utamchukua mtu mwenye kipato cha kati miaka 20-25 kumaliza kulipa deni.
 
maelezo zaidi kwenye mkopo wa ardhi wizarani..
Nenda Wizara ya Ardhi, gorofa ya 9 utapata maelezo ya kina, mkopo ni 2% interest na ni lazima uwe mfanya kazi wa UMMA, kuna benefits nyingi sana kwa wafanya kazi ! Nakutakia kila la kheri!
 
Kujenga ni kuogopa maisha.Kama unachukuwa Mokopo na kuanzisha biashara/mradi inakuwa jambo but usimamizi lazima uwe mzuri ili Upate tija.
Kama unajenga nyumba ya biashara it's oke sababu nayo inakuwa ni source of come
 
Nenda Wizara ya Ardhi, gorofa ya 9 utapata maelezo ya kina, mkopo ni 2% interest na ni lazima uwe mfanya kazi wa UMMA, kuna benefits nyingi sana kwa wafanya kazi ! Nakutakia kila la kheri!
Hata mikoani ipo? Mm nipo Iringa inapatikana huku?
 
Back
Top Bottom