Kuchukua mkopo benki na kujengea nyumba ni jambo jema lakini hasara yake ni kubwa

Kuchukua mkopo benki na kujengea nyumba ni jambo jema lakini hasara yake ni kubwa

Nilikuwa napanga Nyumba nalipa 400000 kwa mezi,nimokopa nikajenga Nyumba nanimehamia sina shida kabisa uache uongo we we,kukopa kunasaidia sana tu
mshahara wako ulikuwa kiasi gani per month, sema tu hakuna amayekufahamu humu
 
Wewe kweli unakula panya. Usisifie uwozo kama chakula chako. Mikopo inayotolewa na hizi bank zetu ndio inaumiza sana kwa riba kuwa kubwa lkn upande mwengine huwapa nafuu watu wengi kwa kuwapatia makaazi mazuri na kuondosha usumbufu wa kuhamia kila mitaa.
tumia lugha ya ustaarabu. Huyu kaleta uzi fikirishi wewe unamtukana na panya, Mungu akupige kofi
 
Si kweli maneno yako maana inategema kama wewe ni mfanya kazi wa umma unaweza kuchukua mkopo according to your salary au ukaenda Wizara ya Ardhi wanatoa mkopo wa interest ya 2% , Private Sector ninaamini pia kuna njia ya kupata mkopo bank .... ukiwa na nia ya kufanya jambo mtu yeyote asikukatishe tamaa! Don't fear anything but FEAR itself,
Mkuu utaratibu wa kupata mkopo Wizara ya Ardhi upoje huu? I become interested.
 
Nenda Wizara ya Ardhi gorofa ya 9, utapata maelezo yote, lazima uwe mfanyakazi wa UMMA. Ni 2% interest only, kuna benefits nyingi sana kwa wafanya kazi!
Nimeipenda ngoja na Mimi nifuatilie
 
Wazo lako zuri lakini ktk uhalisia wachache wanaweza,biashara pia ni risk taking kama kununua gari.
Yaani kwa mtumishi aliyebanwa na mazingira hayamruhusu kufanya biashara hamna jinsi,lazima akope ili awe na nyumba. Kuwa na nyumba kutamsaidia asipange au kupangisha hiyo nyumba apate kodi. Lasivyo atastaafuu bado amepanga kama hakujenga.
Mkopo mbaya ni wa gari ya kutembelea hatari,kama umekopa naamini hata kuilipia bima comprehasive na mikopo ya gari imewaingiza loss vijana sana maintanance si mchezo.
Nimeongelea hasa watumishi. Kutunza fedha nayo ni kipaji,maana fedha ni shetani ikiingia inataka kutoka.[emoji28] [emoji28]

Umenena Vyema! Mkopo wa Nyumba na hasa kwa maana halisi mkopo ulioko kwenye mifumo ya kitaifa mahsusi kwa ajili ya kuwezesha wananchi kupata makazi stahili ni njia mbadala ya uwekezaji katika maisha yako. Penda usipende kama huna nyumba utakodisha. Kodi utakayodaiwa au unayodaiwa unaimudu walau kwa sasa. Ila matakwa ya Baba Mwenye Nyumba na jinsi atakavyokudai na kukupandishia ukijuisha yote hayo utaona ni bora ungekuwa umetafuta nyumba ya kununua kwa njia ya mkopo. Mikopo iliyo rasmi katika mifumo ya mikopo ya nyumba ni ya muda mrefu - yaani miaka 10, 15, 20 au 25. Marejesho yanaweza yakazidiana kwa kiwango kikubwa na kodi ambayo unatakiwa ulipe leo. Lakini fikiria Ndugu Njughu kama ulivyoeleza hapo juu, kuanzia marejesho ya mwezi wa kwanza hadi mwaka wa 20 yanahesabiwa kama ni hisa zako ndani ya nyumba ile. Maana yake nini? Ukilipa kodi ya pango, pesa ile inatumbukiwa kwenye shimo ambamo huwezi kamwe kuiona, lakini marejesho ya mkopo unajiwekea akiba uzeeni.

Mara nyingi wengi wetu hatuoni mikopo kama aina ya uwekezaji, tunaiona kama ni kimbilio la mwisho la kutokea tunapokuwa kwenye mahitaji. Tungeiona kama njia mbadala ya kutumia raslimali zetu yumkini tungechochea uchumi kwa namna nyingi. Ukichukua mkopo kuna ambaye atashawishika kujenga na ujenzi maana yake unafahamu tena....

Ila tukumbuke thamani ya pango (kodi ya nyumba) inakwea siku zote, marejesho ya mkopo ni sawia kwa kawaida, basi utaona aliyekopa nyumba 2014 akawa analipia 700,000 kwa mwezi kwa nyumba ambayo angepanga angelipa 500,000, mwaka huu kodi inaweza imekuwa 700,000 na hivyo kulingana na marejesho, na pengine miaka 3 ijayo itakuwa 1,000,000 lakini mkopaji ataendelea na laki saba yake na tayari akiwa ameshajimbilikia hisa za kutosha kabisa.
 
Kweli mkuu ishi vzuri hata ka kupanga watoto wasome vizuri mambo mengine yatafuata huko ulaya umeona nani anajenga?
Acha uoga wa maisha..Ulaya Watu wanakopa sana kuliko uku..Unaogopa Kudaiwa?Marekani ni nchi Tajiri ila bado ina daiwa deni kubwa tu.

Vijana tuache kuogopa kukopa..Matajiri asilimia kubwa wana Mikopo bank.

Binafsi nina mifano ya watu wengi waliotajirika kupitia mikopo najifunza kupitia kwao
 
inategemeana na kazi ufanyayo sasa km ww ni mwl unakopa m 15 manake utaishi kwa dhiki ila km ni jaji unakopa m15 ni sawa na mshahara wa miez 2 maelezo yako hayana maana tena ungesema wafuatao wasikope kwa kujengea manesi,askari,walimu,watendaji wa vijj/kata/tarafa ,afisa kilimo na mifugo wa kata,ustawi wa jamii,hapo ungeeleweka lakin sio mbunge,waziri,jaji,hakimu,maelezo hawawez kueleweka kwa watu hao m 20 kwake ni miez 2 tu
 
Nilikuwa napanga Nyumba nalipa 400000 kwa mezi,nimokopa nikajenga Nyumba nanimehamia sina shida kabisa uache uongo we we,kukopa kunasaidia sana tu
Take home ya watumishi wengi wa serikali ni 450000/=,wewe siyo wa mchezo.
 
Tulilima ruaha mbuyuni ukipata sehemu ambayo ni karibu na maji utafanya vyema usiogope kuthubutu mkuu Mungu akutangulie hakuna ambacho hakina changamoto
Nashukuru sna dadaake,,naweza kukujia pm ndugu
 
Tena uwongo iv biashara ni risk ikifa si bora nijenge tena naishi kwa amani ya moyo
Tetemeko la aridhi likipiga nyumba. Nalo ni swala muhimu sana la kuzingatia kwa iyo asara aikwepeki katika maisha ndugu yangu
 
Afrika watu wanatamani kuwa na nyumba zao wenyewe-sijui kwa nini???? Kila mtu utasikia nataka kuwa na kwangu!
Uwezo wetu waafrika wa kufikiria ni mdogo ukilinganisha na watu weupe na ndio maana waindi na Waarabu wengi wanakaaa katika nyumba za kupanga na wanaishi maisha mazuri kuliko sisi waafrika. Maana wao wapo makini na mzunguko wa pesa. Awawezi kukopa pesa ya kununua Gari au kujenga nyumba ya kuishi. Na akikopa pesa ujue ya biashara kama ni kujenga ni nyumba za biashara, petroleum station [emoji618], mahotel, magodown na kama ni magari ni kufanyia kazi kama mashine za kuchimba barabara, mitaro na Gari kama za kubeba abiria na magari ya mizigo
 
Umeeleza vzuri. Ila kuna mtu analpa labda 500,000 kodi ya nyumba kwa mwezi. Kwahyo akpata mkopo wa muda mrefu kwa mrejesho wa 500,000 kwa mwezi huyo kwake ni faida kubwa.
 
Back
Top Bottom