Kuchukua pesa za watu benki si kitu cha kawaida, Inawezekana nchi imefilisika!

blogger

JF-Expert Member
Joined
Mar 13, 2012
Posts
12,112
Reaction score
15,060
Kuchukua pesa za watu bank si kitu cha kawaida. Hii nchi RAIA wake huwa tunatabia ya kuzoea mambo hata yasiyozoeleka. Huwa tunasema tunamwachia Mungu. Na, hata hili litapita.

Lakini ni bora hata tuambiwe zinaenda wapi? Kama tunalipa madeni tuambieni na kama zinaenda kwenye miradi tuambieni, kama ndo tunajilipa mishahara semeni pia.

Kukaa kimya kama hamsikii malalamiko ya wananchi ni dharau kubwa. Tunahitaji tuambiwe hizi pesa mnazochukua kwenye Acc za watu bank ZINAKWENDA WAPI!?
 
Sasa hivi kila kitu mnamsingizia Magufuli wakati ata yeye akiwa pale juu alikuwa na analipa na madeni ya mikopo waliyokopa wenzake bila matozo!

Hakuna sehemu umeambiwa tozo zinatumika kulipa madeni, zaidi utasikia Tozo ndo zimeongeza bajeti ya miradi ya Tarura huko mitaani na vijijini, kipindi wanaanza kuchukua tozo walisema zinaenda kujenga madarasa,. Badae wakachuna

Deni la Ujenzi wa Tazara toka China limemalizwa kulipwa kipindi cha Magufuli.
 
Mbona inaeleweka zinakokwenda kufanya kazi tozo na Kodi zetu, kwani huoni vituo vya Afya, zahanati, shule, huduma za umeme na maji vikisogezwa na kupelekwa Hadi vijijini, kwani huoni namna mwananchi alivyo punguziwa adha ya kusafiri umbali mrefu kutafuta huduma,

Tuendelee kumuunga mkono mh Rais wetu kwa kazi kubwa anayoifanya kuijenga nchi yetu,

Pia tutambue kuwa nchi yetu itajengwa kwa mikono yetu wenyewe, hivyo lazima tuchangie kidogo kutoka katika vipato vyetu kuijenga nchi yetu
 
Kuchukua pesa za watu bank si kitu cha kawaida. Hii nchi RAIA wake huwa tunatabia ya kuzoea mambo hata yasiyozoeleka. Huwa tunasema tunamwachia Mungu. Na, hata hili litapita.

Lakini ni bora hata tuambiwe zinaenda wapi? Kama tunalipa madeni tuambieni na kama zinaenda kwenye miradi tuambieni, kama ndo tunajilipa mishahara semeni pia.

Kukaa kimya kama hamsikii malalamiko ya wananchi ni dharau kubwa. Tunahitaji tuambiwe hizi pesa mnazochukua kwenye Acc za watu bank ZINAKWENDA WAPI!?
Rejesho la mikopo
 
Hayati alichukua za Matajiri tu lakini huyu wa Sasa hadi za Walemavu anakomba.
 
Back
Top Bottom