Mystery
JF-Expert Member
- Mar 8, 2012
- 15,843
- 31,057
Nimemsikiliza kwa makini Sana, Rais Samia Suluhu Hassan, Katika hotuba yake kwa Baraza la vyama, akijibu hoja aliyopewa na Kiongozi mkuu wa ACT Wazalendo, Zitto Kabwe, aliyeomba Mwenyekiti wa Chadema Mbowe afutiwe kesi ya ugaidi inayomkabili.
Alijibu hoja hiyo kuwa kusamehe kupo, lakini Mbowe inabidi aheshimu sheria!
Nimejiuliza maswali kadhaa, hivi kumbe Rais Samia, ndiye aliyeamuru Mbowe akamatwe,na kufunguliwa mashitaka ya ugaidi, kwa madai ya kuwa anavunja sheria kwa kudai Katiba mpya?
Hivi ina maana gani kuwa kiongozi wa chama cha upinzani nchini?
Maana yake ni kukosoa yale yanayofanyika na serikali kwa nia ya kuliletea maendeleo makubwa zaidi nchi yetu.
Tumeshuhudia ushahidi ukitolewa kwa watuhumiwa wakidai kuwa maelezo yanayodaiwa kuwa waliyatoa wao Katika kituo cha Central, wakikana kuwa kamwe hawakuyatoa kwa hiyari yao, kwani waliteswa Sana na maelezo hayo yaliandikwa na mapolisi Katika kituo cha Mbweni na wao kulazimishwa kuyassini, ambapo ni kinyume cha Haki za mtuhumiwa.
Kwa namna Rais Samia, alivyoielezea Kesi hiyo, nimebaini kuwa hata kama Mbowe atatoka kwa msamaha wa Rais, itabidi aipiganie Katiba mpya kwa kasi zaidi na ari zaidi, kwa manufaa ya kizazi kijacho, kwa kuwa kwa mfumo uliopo sasa, ambao Katiba imempa mamlaka ya ki-mungu mtu, Rais wa nchi, ndiyo tatizo kubwa linafanya mfumo wa kiuongozi, umpe kiburi cha kupitiliza Rais wa nchi hii.