Hahaha aisee hapa mmenikumbusha mbali sana aisee, mie nadhani glands zangu za hacra zimekufa aisee. Kuna mmoja wetu humu kazungumzia suala la low self esteem.... yaani unasema uwongo kwa kuwa unajua huwezisema ukweli mbele ya mwandani wako kwa kuwa hujiamini na ulilolifanya. Mmenikumbusha one of the vituko vya ex wangu ambaye aliniitroduce kwa mdada ambaye alisema walisoma wote (I trusted him na yule mdada nikamfanya one of my telephone buddies) only to find that hawajawahisoma wote pamoja na ni wapenzi kwa muda mrefu tu. Ilinichukua muda wa wiki tatu kuumeza uongo huo ikiwemo kumwuliza kila mara naye alikuja na jibu lake alokremu la kushikilia pale pale kuwa walisoma wote. Siku nilipomshukia na facts, bahati mbaya nilisema kwa tone ya dharau kiasi cha kumfanya asiamini kuwa ni mie kondoo wake.
Hii inaturudisha kwa Babu DC na Mbu. Babu DC nafikiri ni vema tukatofautisha kati ya uwongo/danganya wenye nia ya kunusuru, kuokoa au kuongeza dakika za mahusiano, ambao huwa unaruhusiwa mara moja tu yaani unausemea mara moja kisha huurudii tena (either kwa kutokifanya kile kilichokufanya udanganya au kukifanya kwa teknologia mpya ili usishikwe)
Ila uwongo ambao unajirudia, kwa mwenzi yule yule eh, ni bora mtendaji ukaanza kujiuliza uzito wa penzi lako kwa umpendaye kabla hujaanza kutengeneza uwongo mwingine kwa kosa linalojirudia aisee