PreGE2025 Kudukuliwa kwetu imekuwa kituko Kenya, wanasema polisi wameweza kuzuia akina Martha udukuzi umewashindaje?

PreGE2025 Kudukuliwa kwetu imekuwa kituko Kenya, wanasema polisi wameweza kuzuia akina Martha udukuzi umewashindaje?

Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla)

Cute Wife

Platinum Member
Joined
Nov 17, 2023
Posts
3,054
Reaction score
8,449
Wakuu,

Majirani wanapata burudani tu huko, wanasema sasa mtu unaweka password "Zuchu" au "Diamond" unategemea nini? :BearLaugh: :KEKLaugh::KEKLaugh: majirani wanajua kutusuta😂.



Ila tukisema ukweli kutoka moyoni, si ni kama majirani wametusadia Watanzania kulipiza hata robo kwa madhila tunapitia?

Comments za wananchi kwenye udukuzi wa leo ni funzo tosha kwa serikali yoyote inayojielewa kurudi nyuma na kubadilisha nyendo zake, maana imeonesha bila chenga jinsi wananchi walivyoichoka serikali yao. Chance yoyote watakayoipata kuhahakisha serikali inataabika vilivyo wataichukua, hii sio hatua nzuri

Lakini si mnajua tena wanazengo wetu walivyokuwa sikio la kufa? Wameenda kule kule walipokuwa wanategemewa kutoa vitisho na kichambo ndani yake, wengine mpaka wamefanya tuonekane weupe, eti wamefungua account mpya wakati dunia imeona tulivyodukuliwa.... nakusalimu sana Mkuu Gerson Msigwa.

Anyhu, kwakuwa Rais Samia na wapambe wake wanapita humu, kuna madini mengi humu ya kujifunza kujiweka sawa upande wa digitali, na hata JamiiForums wanaweza kuwasaidia kabisa kuwapiga msasa tusiaibike tena wakati mwingine.... ila dawa itakayomaliza haya kabisa kabisa ni utawala bora, uwajibikaji na kufanya maboresho kama mama alivyosema kwa kizaramo 'reforms' sehemu zote tunazoona hazina tija kwa sasa.

Alamsik!
 
😂😂😂😂😂😂
 
Swala la cyber attack, si la kwanza kutokea duniani, udukuzi unafanyika kila iitwapo leo!
Nchi zote kubwa dunian zmepitia cyber attack!

NA HIYO SIYO MBINU YA KUMTOA LISU KOROKORONI!

SEMA NINI "LEO WATZ TUMEPIGWA TUKIO"
tanzania haiwezi kulala, na bado hakuna cha kuirudisha tz nyuma kuwashughulikia wahuni wa kisiasa.
 
Naona sasa kuingia mtandao wa X lazima utumie VPN kama mtandao wa Telegram
 
Swala la cyber attack, si la kwanza kutokea duniani, udukuzi unafanyika kila iitwapo leo!
Nchi zote kubwa dunian zmepitia cyber attack!

NA HIYO SIYO MBINU YA KUMTOA LISU KOROKORONI!

SEMA NINI "LEO WATZ TUMEPIGWA TUKIO"
tanzania haiwezi kulala, na bado hakuna cha kuirudisha tz nyuma kuwashughulikia wahuni wa kisiasa.
Nasikia police wamepost porno kwenye ukurasa wao wa X
 
Kwahy hao akina Martha walivyokuja hawakuzuiliwa?
Kweli Afrika ni bara la giza mana hata ukweli hauonekani.
 
Back
Top Bottom