Wanabodi,
6. Kwa sasa, angalau Chadema, kupitia M4C, imeshagundua adui halisi anayewakosesha ushindi ni nani!, na sasa imejielekeza kwa wananchi wa grassroots level ambao ndio wenye maamuzi ya mwisho na wamekuwa wakiichagua CCM kwa mazoea tuu, hivyo concentration ikiwekwa kwenye "changing the mindset" ya wenye maamuzi, kuacha kuchagua kwa mazoea tuu, bali kuchagua kwa sababu yaani making informed decisions, Wananchi, watafunguka macho na akili, na hawatakuwa na sababu tena ya kuendelea kuichagua CCM!.
7. Ili hili liwezekane, wapinzani wasiwe ni watu wa kulalamika na kulaumu tuu kuhusu CCM, bali sasa wajikite kueleza where CCM does wrong, lakini wao wakiingia, watafanya nini tofauti na CCM, na ukichagua upinzani kitabadilisha nini, ili wale wanaoichagua CCM kwa mazoea tuu, wapate sababu za msingi za kutoichagua CCM na kuwachagua wapinzani. Yaani Wapinzani wawape Watanzania reasons za not kuchagua CCM na sio kuibadili tuu badala ya kuichagua CCM waichague Chadema for what?.
8. Mara baada ya uchaguzi wa 2010 na mafanikio makubwa upande wa Chadema, kwenye ile mada yangu ya
CCM Imechokwa, CHADEMA Haijajipanga! niliwaeleza Chadema kuwa wao na wapinzani wengine wote bado wako kiuana harakati zaidi, yaani vyama vya kiuana harakati, bado hawajipanga mkao wa kichama tawala tayari kwa kushika dola, lakini kwa kwa sasa kupitia M4C, Chadema wanaonyesha dalili za kujipanga japo bado wanakabiliwa na madhaifu haya na yale, yakiwemo, lile koti la ukanda, udini, ukabila na ubinafsi wa "umimi" etc.
16. Suppose 2015, Watanzania tutakuwa Milioni 50 wenye sifa za kupiga kura ni milioni 30, hawa wote wakihamasishwa kujiandikisha na kujitokeza kupiga kura, mgombea wa CCM atajipatia kura zao zile milioni 5 za wanachama wao kwa mujibu wa tovuti ya CCM, halafu hizo kura milioni 25 zimuangukie mgombea wa upinzani, hata NEC ya CCM, wachakachue vipi, there will be no way out!, hivyo adui yetu mkubwa sio CCM, bali ni Watanzania wanaipigia kura CCM! na Watanzania wengi zaidi ambao hawajiandikishi na hata wakijiandikisha hawajitokezi kupiga kura!. The magic ni uhamasishaji na reaching out kuwafikia!.
17. Sasa ili kuwafikia Watanzania wote -haswa hawa grassroots level na kuwaamsha waliolala, Chadema haiwezi kuwafikia Watanzania wote kwa kutegemea maandamano na mikutano ya hadhara na mass media za wengine. Chadema lazima wawe na mass media yake ambayo ita propagate the message of "changing the mindset" ya Watanzania. Chadema wana all the resource kumiliki media yake lakini very unfortunately they are myopic, hawana vision ya kuona mbali kuangalia nje ya box and see a bigger picture. Hawajui kupanga priorities zao. Bei ya gari moja tuu la M4C linatosha kununua transmitter ya Digital ya redio na TV and convert chumba kimoja pale Ufipa into a modern studio! na kuwa na YouTube Channel yake ya live stream na active interactive social media pages, Chadema bila media yake, ni kutwanga maji kwenye kinu! CCM ina media yake na TV yake ya TBCCM, radio zake na magazeti yake, Chadema bila media yake, ikulu wataendelea kuisikia tuu kwenye bomba, 2015 ni CCM tena! .
Wasalaam.
Paskali
NB. Paskali, sasa ni mwanachama, mfuasi na mshabiki wa chama fulani cha siasa, in fact ni kada!. Lakini ni kada Mzalendo contemporary mwenye kutanguliza mbele utaifa na maslahi ya taifa ndio maana licha ya kuwa kada wa chama kingine bado anawashauri vyama vingine the right thing to do.