Pascal Mayalla
Platinum Member
- Sep 22, 2008
- 59,804
- 134,593
- Thread starter
-
- #21
Mkuu zimmerman, kwanza nakushukuru sana kwa sababu mpaka sasa, hii thread imeshamkomboa kifkra mtu angalau mmoja ambaye ni wewe!. Kitendo tuu cha kukubali kuwa "Dhana kwamba adui mkubwa wa watanzania si CCM bali ni sisi wenyewe siyo sahihi sana" hii kauli peke yake imenifariji kuwa dhana hii siyo sahihi sana inamaanisha ni sahihi kidogo!, kwangu uelewa kidogo tuu unatosha kuleta ukombozi wa kweli wa pili wa Mtanzania.Pasco, unajua mada zako unazipanga vizuri, unaziandika vizuri na unazifafanua vizuri kwa lugha rahisi kiasi kwamba hata kama kimantiki si kweli watu wengi wanaweza kukubaliana na hoja zako? Ndivyo ilivyo hata kwa hoja yako hii ya leo.
Kiukweli kulekea elfu mbili na kumi na tano adui mkubwa wa Chadema ni ..CCM.
Dhana kwamba adui mkubwa wa watanzania si CCM bali ni sisi wenyewe siyo sahihi sana. Ni kweli kwamba kuna vi element fulani vya utamaduni wa kitanzania vinavyotubakisha sana nyuma lakini adui mkubwa ni yule anayecapitalize kwenye udhaifu wetu ili kuendelea kutunyonya na kutukandamiza. CCM haina huruma, haina tofauti na mkoloni wa kiarabu au kijerumani aliyetumia ukarimu wetu, upole wetu na kukosa elimu kwetu ili kujinufaisha juu ya migongo yetu. Ni kweli, hata hivyo, kwamba njia ya kumshinda adui wa namna hii ni kusambaza elimu ya uraia. Hii inatusaidia sana kuongeza ukali kidogo tunapodai haki zetu za kikatiba na kumpinga hasa pale anapoleta uhuni na ndicho Chadema wanachofanya.
Pasco bahasha zitaua taaluma yako Mkuu!
TUMBIRI (PhD, University of HULL - UK),
tumbiri@jamiiforums.com
Pasco,Mkuu Tumbiri, hizo bahasha zitaiua taaluma yangu ipi kati ya hizi ,
Mimi ni Mwandishi wa habari wa kujitegemea,
Mimi ni Mtangazaji wa kujitegemea
Mimi ni Producer wa kulipwa
Mimi ni Media Consultant wa kulipwa
Mimi ni political Advisor wa kulipwa
na kitaaluma nimesomea LL.B ya UDSM nikiamua nafanya tuu petition na kuwa registered as an advocate.
Sasa hizi bahasha zitakazo iua taaluma yangu ni zipi hazwa na taaluma itakayo uliwa ni ipi kati ya hizo?.
Nimeshawahi kusema humu sio mara moja wala mara mbili kuwa nilipoikuwa mwandishi tuu wa habari, bahasha nimezipokea sana, na sasa kama mshauri wa habari, hizo bahasha mimi ndio nazigawa with clear and honest conscious kuwa bahasha za uwezeshaji is the right thing na ni haki za msingi za waandishi kuwezeshwa ili waweze kutimiza majukumu yao ya kila siku!.
N.B hili la bahasha, nimelifafanua vizuri hapa waandishi-wa-habari-na-bahasha-sio-kila-bahasha-ni-rushwa
Kwa hiyo ukitaka kuuwa nyoka una unapiga risasi kwenye mwili wake au mkia sio?
Pasco,
Bahasha tunazozungumzia ni zile mnazopewa kwa ajili ya kutunga habari ili kutimiza malengo ya mtu au kikundi flani. Sasa hivi unasema wewe ni mshauri wa habari na hizo bahasha wewe ndiye unazigawa. Kwa hizi namaanisha zile unazozigawa kwa maofisa wa Taasisi za Serikali na mashirika ili upatiwe matangazo nk.
TUMBIRI (PhD, Hull University - HULL City, UK),
tumbiri@jamiiforums.com
na kitaaluma nimesomea LL.B ya UDSM nikiamua nafanya tuu petition na kuwa registered as an advocate,
Wanabodi,
Kutokana na kauli hiyo, nimekuwa inspired kuandika kidogo kuhusu adui mkuu wa Tanzania wengi wakidhani ni CCM, kumbe sio, bali adui mkuu wa Watanzania ni ... kwa maoni yangu,
1. Tatizo kubwa .... ni sisi Watanzania tulioiweka CCM madarakani and it plays games on us again and again na sisi
tukiendelea kuiweka madarakani again and again na sitashangaa kama hata 2015, tukairudisha tena!.
Pasco.
NB. Pasco wa jf, sio mwanachama, mfuasi wala mshabiki wa chama chochote cha siasa, bali ni Mtanzania wa
kawaida mwenye kuweka mbele maslahi ya taifa.
Kama umeshang'amua wananchi ndio wamerubiniwa na CCM ili kuichagua, then ili kuiondoa hiyo CCM iliyowarubuni ni kuwafikia hao wananchi na kuwaelkimisha ili wasiendelee kurubuniwa!. Wewe jiulize anayepiga kura kuchagua ni nani?, CCM si ni inachaguliwa?!, unatakiwa kumfuata mchaguaji na sio mchaguliwa!, ukiendelea kumtarget mchaguliwa tuu, mchaguaji ataendelea kumchagua huyo huyo mchaguliwa aliyemzoea, ukimtarget mchaguaji na kumuelimisha asiendelee kuchagua kwa mazoea bali kwa sababu, then, mchaguliwaji wa mazoea, hata chaguliwa tena na atajifia natural death!.Ndo hapo sasa mkuu, huyu jamaa anataka kuharibu mchuzi kwa kujifanya mchambuzi makini, ila anatakiwa akumbuke pia kuchamba kwingi ni kuondoka na kinyesi. TATIZO NI CCM, huwezi kumlaumu mwananchi wa kawaida kule kijijini ambaye kanyimwa hata elimu ya kung'amua mambo. CCM NDO IMEWANYIMA WATANZANIA ELIMU BORA, MATOKEO YAKE UWEZO WA WATANZANIA WENGI KUNG'AMUA MAMNBO HASA VIJIJINI NI MDOGO, MPAKA WANASHAWASHIWA KWA CHUMVI ILI WAMPIGIE MTU KURA. usiwalaumu watanzania, ulemavu walio nao wamelazimishwa makusudi na hili li-ccm. SHULE HAZINA WALIMU BORA, WALIOPO WENYEWE HAWALIPWI STAHIKI ZAO MUDA MUAFAKA, UNATEGEMEA NINI MKUU??? NARUDIA TENA MARA 100 ZAIDI, TATIZO LA TANZANIA NI CCM, MCHAWI WETU TANZANIA NI CCM.
Mkuu Bwa'Nchuchu, hii umeihamishia humu?!, hii ilistahili kule "chit chat", ila kwa vile umeileta humu, nitakujibu tuu kwa sasa na kukuomba ukishasoma hili jibu, jirudie zako kule "chit chat"!.You are a bush-league law graduate. If you were licensed to practice law I wouldn't advise anyone to come to you.
Mkuu Bwa'Nchuchu, hii umeihamishia humu?!, hii ilistahili kule "chit chat", ila kwa vile umeileta humu, nitakujibu tuu kwa sasa na kukuomba ukishasoma hili jibu, jirudie zako kule "chit chat"!.
Kwa uhaba wa ma advocates uliopo nchini, nikiamua ku register as an advocate, belive me, sitahitaji recomendation yako kupata wateja kwa sababu nitaregiter ili kutoa huduma za kisheria bure kwa wasio na uwezo, media consultancy zangu na production company yangu inatosha kabisa kunisustain to my grave, nita register to help the helpless not to make it!.
Mkuu MpendaTZ, nina swali dogo tuu kwako, anayeichagua CCM kupitia ballot box ni nani?, kama CCM inajichagua na kuprint zile kura, then hao members wa opposition waliomo bungeni, wasingekuwemo!.PASCO,
Hakuna cha kujiuliza sana tatizo kubwa Tanzania ni CCM ikiwa imeshikilia Uongozi wa Serikali ya JMT chini ya Katiba ya Chama chenyewe. Kumbuka hatuongozwi au kufuata Katiba ya Tanzania na wala haipo. Bali tunafuata itikadi ya CCM iliyobatizwa na kuitwa Katiba ya Tanzania. Ndiyo maana kila kiongozi nchini anachaguliwa na Mwenyekiti wa CCM na ni lazima awajibike kwake na siyo kwa wananchi.
Du Bwanchu unanitesa!, ngoja kwanza nitafute kamusi ya Kisuaheal ili kulitafasiri hili neno halafu nitakurudia!.Rudi shule ukajifunze tahajia.
Du Bwanchu unanitesa!, ngoja kwanza nitafute kamusi ya Kisuaheal ili kulitafasiri hili neno halafu nitakurudia!.
Haya mawazo niliwahi kuyapigia kelele 2010..kama CHADEMA wanapenda kusikia wanayotaka kuyasikia tu, itakula kwao.Wanabodi,
6. Kwa sasa, angalau Chadema, kupitia M4C, imeshagundua adui halisi anayewakosesha ushindi, na sasa
imejielekeza kwa wananchi ambao ndio wenye maamuzi ya mwisho na wamekuwa wakiichagua CCM
kwa mazoea tuu, hivyo concetration ikiwekwa kwenye "changing mindset ya wenye maamuzi, kuacha kuchagua
kwa mazoea tuu, bali kuchagua kwa sababu. Wananchi, watafunguka macho, na hawatakuwa na sababu tena
ya kuendelea kuichagua CCM!.
7. Mara baada ya uchaguzi wa 2010 na mafanikio makubwa upande wa Chadema, kwenye ile mada yangu ya
"CCM Imechokwa, Chadema Haijajipanga", niliwaeleza kuwa wapinzani bado hawajipanga mkao wa kushika
dola, lakini kwa kwa sasa kupitia M4C, Chadema wanaonyesha dalili za kujipanga japo bado wanakabiliwa na
madhaifu haya na yale, yakiwemo, lile koti la ukanda, udini, ukabila na ubinafsi wa "umimi" etc.
8. Kwa leo naomba nisiingie tena kwenye udini, ukanda na ukabila wa Chadema, bali naomba nijikite kwenye
ubinafsi au "umimi" kwa Chadema kujiamini kupita kiasi kuwa peke yao wataweza!, nilisema peke yao
hawawezi, na leo nasema te na na tena, "Chadema peke yanu hamuwezi Kuiondoa CCM Madarakani" kwa
sababu hili CCM ni dubwana kubwa sana ambalo haliwezi kung'oka bila umoja ambao ni nguvu ya Watanzania
wote wenye kuliutakia mema taifa hili.
10. Chadema na wapinzani wengine wote wa ukweli, ni lazima wa join forces kutafuta the common working
grounds na wenzenu wengine wote mu work together towards a common enemy hata na nyinyi wenyewe kwa
wenyewe lazima mkubali kushirikiana kwa kukubali kutokubaliana kwa hayo madogo madogo lakini lazima
mkubaliane kwenye kubwa la msingi kwa kukubali "umoja ni nguvu" vinginevyo matokeo ya 2015 yatakuwa ni
yale yale ya, vyama vile vile, na watu wale wale!.
12. Hakuna ubishi kuhusu nguvu ya CUF kule Zanzibar na Chadema itake isitake, ipende isipende, ili kujihakikishia
njia nyeupe ya kuwa mpangaji wa magogoni kwa 2015, ni lazima ikubali kuisupport ya CUF kwa upande
Zanzibar ili CUF nao wakubali kuisupport Chadema huku bara!. Chadema wakae chini na CUF, waainishe
maeneo ya strong holds za kila mmoja na kuachiana maeneo hayo ili 2015, kuepuka kumfaidisha kunguru
kwa vita vya panzi!.
Wasalaam.
Pasco.
TATIZO NI CCM, huwezi kumlaumu mwananchi wa kawaida kule kijijini ambaye kanyimwa hata elimu ya kung'amua mambo. CCM NDO IMEWANYIMA WATANZANIA ELIMU BORA, MATOKEO YAKE UWEZO WA WATANZANIA WENGI KUNG'AMUA MAMNBO HASA VIJIJINI NI MDOGO, MPAKA WANASHAWASHIWA KWA CHUMVI ILI WAMPIGIE MTU KURA. usiwalaumu watanzania, ulemavu walio nao wamelazimishwa makusudi na hili li-ccm. SHULE HAZINA WALIMU BORA, WALIOPO WENYEWE HAWALIPWI STAHIKI ZAO MUDA MUAFAKA, UNATEGEMEA NINI MKUU???