Elections 2015 Kuelekea 2015: CHADEMA, Don't Miss the Target, Adui Mkubwa sio CCM Bali ni ...


Mkuu makundi4619, ndio maana nasisitiza "reaching out" Wapinzani waachane kabisa na CCM, concentration ielekezwe kwenye reaching out strategy to change the mindset ya wapiga kura, ili kwanza kuwahamasisha kujitokeza kwa wingi kujiandikisha, kisha wajitokeze kwa wingi kupiga kura!.

Uchaguzi uliopita JK amechaguliwa kwa kura milioni 5!, waliojiandikisha ni milioni 20, waliojitokeza kupiga kura ni milioni 8, hii inamaana kuna watu milioni 12, walijiandikisha lakini hawakujitokeza kupiga kura kwa sababu zozote zile, ile wengi wao hawakujitokeza kutokana na kukata tamaa kuwa hata wapige vipi kura, itakuwa ni kujisumbua tuu, matokeo yatakuwa ni yale yale!. Hawa watu sasa ndio upinzani unatakiwa kuhangaika nao!.
 
Ni hoja ya kitoto na kijinga umeandika halafu ukairemba.Sichangii huu ujinga...
 
Pasco umeongea kitu cha maana ingawa najua wengi watakupinga.Wachina wanamsemo wao kama nyinyi mna mko wanne na mnapingana na adui mmoja ni bora mkaungana mkamshinda adui halafu mkaja kupingana wenyewe.Inawezekana nimezungumza lugha ambayo wengi hawataweza kuielewa kwa urahisi lakini kitendo cha cdm kujiona wao pekee wanaweza kuing'oa ccm na vyama vingine ni wasaliti kinawasaidia ccm zaidi kuliko cdm.Vyama vyote vya upinzani vinapaswa kuungana bila kujali tofauti zao ili kuing'oa ccm.kitu kikubwa kinachoisaidia ccm kuwa madarakani mpaka sasa ni kuwa na makada waliosomea mambo ya siasa na propaganda tofauti na vyama vingine ambavyo vinategemea nguvu ya wananchi.Ndio maana ni rahisi ccm kupandikiza mamluki kwenye vyama,kurubuni viongozi na wanachama wa vyama vya upinzani.Wanaposema cuf ni chama cha kidini ina maana wanachukua watanzania wa dini nyingine na wale wasiopenda udini na hivyo hivyo wanaposema cdm ni chama cha udini au ukanda lakini hivi vyama vikiwa na msimamo mmoja ccm watashindwa na propaganda zao za udini na ukanda ambazo kwa kiasi kikubwa zimewasaidia kukaa madarakani.
 

Point zako namba 10 na 12 zina mantiki kubwa. Lakini kwanza niseme kwamba sikubaliani nawewe kuwa adui yetu watanzania siyo CCM. Adui yetu huyu anapigana kwa mbinu zote kubaki madarakani ikiwa hata ni kugawa nchi lakini aendelee kutawala. Kila chama kinachojitokeza kinaundiwa zengwe la kulimaliza hata kama zengwe hilo ni hatari kwa mustakabali wa taifa letu. CUF waliundiwa la chama cha waislamu. Ilikuwa ni rahisi hili kufanya kazi kwa sababu viongozi wa CUF walikuwa waislam waliojinasibisha na watu wa pwani ambao wengi wao ni waislamu. Ilipokuja CDM ikauziwa zengwe la chama cha wakristo. Kwa CUF imefanya kazi zaidi na hii ni kwa kuwa wenzetu waislamu huwa hawafichi hisia zao hata wakiwa kwenye nyumba zao za ibada. Yaani siasa na dini hazitenganishwi sana. Hivo CUF kuwa na wafuasi waislamu kulizidi kuizamisha CUF huko pasipo pingamizi kubwa. Hili la waislamu kutotenganisha dini na siasa inaonekana kuwaathiri hata CDM kwani CDM ilipoundiwa zengwe la chama cha wakristo kwa waislamu wengi inawafanya kwa kiasi kikubwa kuigeuzia CDM mgongo kwa kuogopa chama cha wakristo. Si kwamba wakristo hawanaswi katika mtego huu wa ccm. Wananaswa kwelikweli, ni wengi tu wanaoichukia CUF kwa kudhani ni chama cha waislamu kama propaganda za CCM zinavohubiri. Huu ni mchezo wa ccm ambao kusema kweli CUF wanaelekea kabisa kushindwa kujinasua na CDM inapata wakati mgumu kukabiliana nao.
Kwa mantiki hiyo njia ya pekee ya kumkomesha adui yetu CCM ni kwa CDM na CUF kuungana. Amini usiamini tatizo hili ni rahisi kweli kulitatua na kumwacha adui yetu CCM akichuchumaa kwa aibu ya kujificha. Mimi naamini Prof Lipumba ni kiongozi above cheap mudslides zinazorushwa na wafuasi wa CUF wasiokuwa na busara kwa CDM. Vilevile naamini Mhe. Mbowe na Dr. Slaa ni above cheap propaganda politics zinazoitikiwa na wafuasi wa CDM dhidi ya CUF. KUIOKOMBOA NCHI YETU DHIDI YA MAKUCHA YA CCM NI JAMBO KUBWA KULIKO SIASA NYEPESI ZA TAKA KATI YA CDM NA CUF.
Japokuwa si yote nakubaliana nawewe Pasco; lakini katika hili nakubaliana nawe na kusema ni vyema vyama hivi viungane ili kuikomboa nchi yetu.
 
Ni hoja ya kitoto na kijinga umeandika halafu ukairemba.Sichangii huu ujinga...
Mkuu Molemo, hoja za kitoto na kijinga, hujibiwa kwa hoja za kikubwa na zenye akili na sio kwa kususiwa!. Wanaosusa huwa hawasemi, huwa wanapotezea jumla na kujibu pia sio lazima ndio maana kuna wengi hujisomea na kujipitia zao bila kuchangia kitu!.
 
Ninakuhakikishia wanaoichagua CCM ni wana-CCM wachache na kura zao japo chache zinazidishwa maradufu na hao hao waliochaguliwa na Mwenyekiti as a result of CONFLICT OF INTEREST!
 

Mkuu Thesi, hata baada ya kukuwekea data, waliojiandikisha kupiga kura ni milioni 20, waliojitokeza ni milioni 8 na kati ya hao, CCM imechaguliwa kwa kura milioni 5 tuu, hii inamaana kama 2010 wapinzani wangetarget wananchi wapiga kura, hizo kura milioni 12 ambazo hazikupigwa kabisa, zingedondokea upinzani, CCM wangetokea wapi?!.

Lets be genuine and realistic hivi mwenye kosa ni aliyechaguliwa, au aliyechagua?. Kwa vile CCM inachaguliwa na watu, lets concentrate na reaching out strategy kuwafikia hawa watu na kuwaelimisha ili ku change mind set zao kuwa determinant ni wao and no one else!.
 
Mkuu Molemo, hoja za kitoto na kijinga, hujibiwa kwa hoja za kikubwa na zenye akili na sio kwa kususiwa!. Wanaosusa huwa hawasemi, huwa wanapotezea jumla na kujibu pia sio lazima ndio maana kuna wengi hujisomea na kujipitia zao bila kuchangia kitu!.

Pointi yako namba 7 ndiyo imeondoa nguvu ya hoja yako "unasema CDM bado wanakabiliwa na koti la udini,ukanda na ukabila" nikisema huu ni ujinga umeandika bado nitakuwa sikutendei haki? Kwanini unapenda kuwa mdomo wa CCM kuimba propaganda za kishenzi?
 

Mkuu si ndo maana kuna M4C??? tumeona hata elimu ya uraia iliyokusudiwa kuwafikia wananchi, inachakachuliwa. matokeo yake mtanzania hana kabisa ufahamu wa nani anayemfanya asijikwamue. kwa kifupi ni kwamba, tumeamua kujichimbia kwa wananchi ili tuwaamshe wananchi wajue kuwa hawa MAJAMBAZI a.k.a MAFISADI a.k.a CCM hawana tena nafasi ya kuendelea kutuburuza.
 
Ninakuhakikishia wanaoichagua CCM ni wana-CCM wachache na kura zao japo chache zinazidishwa maradufu na hao hao waliochaguliwa na Mwenyekiti as a result of CONFLICT OF INTEREST!
Mkuu Mpenda TZ, kwa mujibu wa website ya Chama cha Mapinduzi, wanajitapa CCM ina wanachama zaidi ya milioni 6!, japo mimi najui kiukweli huu ni uwongo na CCM wenyewe pia wanaujua ukweli kuwa hizo ni data za uongo!.

JK amechaguliwa kwa kura milioni 5 !, hii inamaana amechaguliwa na wana CCM pekee, wakiwemo wana CCM wengine milioni moja ambao hawamchagua JK!. Kama waliojiandikisha ni milioni 20, why bother na hivyo vikura milioni 5 vya wanachama wa CCM?, lets deal na kura zile milioni 15 zilizobakia ambazo hazikupigwa!.
 
Pointi yako namba 7 ndiyo imeondoa nguvu ya hoja yako "unasema CDM bado wanakabiliwa na koti la udini,ukanda na ukabila" nikisema huu ni ujinga umeandika bado nitakuwa sikutendei haki? Kwanini unapenda kuwa mdomo wa CCM kuimba propaganda za kishenzi?
.

Mkuu Molemo, mimi ni mzoefu wa kutosha humu jf, na naelewa fika, ukileta ukosoaji wowote wa Chadema, nini kinakufika. Nafahamu fika jinsi viongozi, wanachama, wafuasi, mashabiki na manazi wa Chadema walivyotamalaki humu jf kiasi kwamba wengine wao wenye akili fupi, wanaamini Chadema ni chama malaika, perfect party, hakina makosa au madhaifu yoyote!. Kwao kukiimbia nyimbo za sifa na mapambio kwao ndio kukijenga chama!, they are very wrong!.

Kwa kawaida yangu mimi niko frank, simuogopi mtu, chama, siogopi lolote wala chochote wakati nikitoa mawazo yangu ambayo naamini niko genuine!. Japo mimi sina chama, lakini unaweza kukuta sisi tunaoleta ukosoaji wa Chadema hadharani, ndio tunaisaidia zaidi Chadema kuliko nyie ambao kazi yenu ni kuisifia tuu kwa nyimbo za shangwe na mapambio!.

Nimesha post thread kibao humu kuikosoa CCM, CUF na CHADEMA, ni ukosoaji tuu wa Chadema hupokelewa kwa negativity za hali ya juu sana humu jf, lakini sisi wengine tuko bold, kwenye sifa tutasifu, kwenye makosa tutakosoa.

Tatizo la udini, ukanda, ukabila na umimi wa Chadema, sikulisemea leo, tatizo hilo lilikuwepo, lipo na litaendelea kuwepo!. Hii sio thread ya matatizo ya Chadema, ni thread ya adui number 1 wa taifa letu sio CCM bali ni wapiga kura wanaoiweka CCM madarakani!.
 
Pasco,
Kwangu tatizo ni ccm na Kikwete kwa wakati huu,
Ungelifuatilia ukweli halisia ccm imechangia au ina mchango mkubwa wa kuwafanya watu 8 millioni wasipige kura kwa kutumia tume ya uchaguzi. Shame on tume ya uchaguzi. Ningelikuwa na uwezo ningeliwatafuta wale watendaji wote wa tume ya uchaguzi waliostaafu nikawaua mara moja maana hawa ndio adui yetu mkuu sie powerless tanzanians.
Hawa ndio wabaya wetu kwani hata damu ingemwagika ingemwagika kwa sababu ya hawa.
 
Mkuu, Mimi kusema " si yote nakubaliana na wewe" haina maana kwamba katika hili sikubaliani na wewe. Moja ya tatizo ni wananchi kutokuwa na uelewa na kutohamasika ndiyo, lakini haina maana kwamba CCM si adui. Katika hoja zote hoja ya kuunganisha vyama imenikuna zaidi na nikaifafanua.
 
Cha muhimu nilichoona hapa ni chadema wahakikishe wanajikita kwenye uhamasishaji wa kupiga kura.Hao 12 millions wengi wao maybe walikuwa cdm ama walikuwa undecided.Ni vizuri kufanya tathmini ya ni kwanini hawakupiga kura,je ni uchache wa vituo vya kupiga kura,usafiri ama ni vitu gani?Je inaruhusiwa kubeba wananchi kuwapatia uasafiri kwenda kupiga kura?ni mambo gani yanayo wadiscourage waliojiandikisha kutokukwenda kupiga kura?
 
Mku Pasco, Hapa ndipo kwenye tatizo lenyewe. Au watu watatishiwa wasipige kura au kura zao kununuliwa na kuwa destroyed au zisihesabiwe na kuvurugwa vurugwa tuu! Chame cha kibabe!
Tujiulize nini kilisababisha kuchelewesha kutangaza matokeo kiasi kile? Nini maana ya kuchelewesha matokeo? Afadhali wenzetu jirani zetu walipochelewesha wahusika walikiri kilichokuwa kinatokea angalau ikasaidia kuunda serikali ya mseto. Na kwa hatua hiyo wamefanikiwa kuongeza kupiga hatua kubwa sana katika demokrasia yao. Mojawapo la muhimu sana ni kuweza kupata Chief Justice aliyechaguliwa kupitia Public vetting! CCM ikiwa imeshika dola hiyo ni ndoto Mkuu!
 
Almanusura nikubaliane na Pasco ila alipochangia sikonge nikakumbuka mchakato na matokeo ya uchaguzi uliopita. Sasa sio ccm tena bali ni serikali ya ccm, maana ccm ni chama tu. Bila vyombo vya serikali wala ccm isingefika hapo. Kwanza tume ya uchaguzi, pili polisi, tatu mahakama, kisha wananchi
 
Mkuu Kaa la Moto, waliojiandikisha ni milioni 20, waliopiga kura ndio milioni 8, ambao hawakupiga kura ni milioni 12!!.

Kama JK amechaguliwa na kura milioni 5 tuu, hii inamaana kwenye uchaguzi wa 2010, kama concetration ya upinzani ingekuwa kwa wapigakura, zile kura milioni 15, zingedondokea upinzani!. Hapo ujue kuna wengi wenye uwezo wa kupiga kura never even bothered kujiandikisha!.

Naamini kati ya zile kura milioni 5 za CCM 2010, asilimia kubwa ni vile vizee visiojua lolote kuhusu upinzani ambapo kwa 2015, vingi vitakuwa either too old to vote, or wameshatangulia mbele ya haki!. Hivyo kura za CCM zinatazidi kupungua!.

2015, idadi kubwa ya watakaongezeka kwenye daftari la kudumu ni vijana wa kuanzia wale wote waliokuwa miaka 12 ile 2010, watakuwa 18, 2015!, hawa ni vijana walielimika kupitia shule za kata, ukijumlisha na mwamko wa M4C, hawa watakuwa sio watu wa kupelekwa pelekwa, au kuuza utu wao na kura zao kwa t-shirt na kofia na ile shibe ya siku moja!. Hivyo wapinzani wakijikita kuwekeza kwenye watu, watu wataamka na kuchagua kwa sababu na sio kwa mazoea!.
 
Mkuu Jmushi, Ukienda maeneo ambayo CDM inashikiia majimbo ukaulizia kazi waliyoifanya wapenzi wa CDM ili kulinda kura utaelewa maana yake na utaelewa sababu zinazopelekea sehemu nyingine zisiweze kulinda kura zao. Huwa kuna mizengwe ya kushangaza. Hawa jamaa huwa na hata masanduku ya ziada yenye kura. Wawakilishi wa vyama wasipokuwa makini tu wakasinzia kidogo wanakuwa wameliwa. Iko sehemu gari lililobeba masanduku ya kura liliharibiwa kiaina porini mahali yalipokuwa yamefichwa mengine na katika harakati za kujifanya gari inatengenezwa kwa muda, yale masanduku yakabadilishwa. Mwananchi maskini hali ya maisha ngumu anafanyiwa mizengwe mpaka anakubali kuachia mambo yatokee. Ndiyo maana unaona wanapoona CDM wanajiimarisha kimapato wanashtuka na kuanza kuunguruma. CCM mtaji wao ni udhaifu wa wananchi, kielimu na kiuchumi.
 
Pasco Take into consideration zile hujuma zinazofanywa na ccm yenyewe ili watu wasipige kura. Hizo zinachangia kuliko maelezo mengine.
Lakini usisahau hujuma za tume ya uchaguzi. Hizi pia zimechangia sana. Ukichanganya na haya yote inaweza kuwepo historia ya kuitoa ccm kwa nguvu madarakani..
 
Last edited by a moderator:
Kwahiyo chadema inaweza kunufaika vipi na hali mbaya ya uchumi na ya kielimu ya wananchi ili waweze kuipiku ccm kwa wingi wa kura?kuwalipa zaidi ya wanavyolipwa na ccm?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…