Elections 2015 Kuelekea 2015: CHADEMA Kuchukua Nchi Kwa Kishindo!... Only If...!

Duh! Naona ndiyo unazidi kujikoroga kuhusiana na maana ya neno "Ridhaa"...Haya Mkuu Pasco huu ni ushahidi mwingine wa kuonyesha wewe ni gamba la kutupa. Mtanzania yeyote yule mwenye mapenzi mema kwa nchi yetu kamwe hawezi kuita ushindi kupitia uchakachuaji wa matokeo, udanganyifu, utoaji rushwa ya aina yeyote ile, wizi na mbinu zozote zile ambazo ni haramu wakati wa uchaguzi, yaliyotangazwa na tume ya uchaguzi wa magamba ni matokeo halali.

Mkuu BAK, lengo la tendo la ndoa kwa mujibu wa mafundisho yote ya dini zote na jamii zote, was ment lifanywe ndani ya ndoa!. Lakini kabla tendo hilo halijafanyika, lazima kwanza umtafute umpendae, umpende, umpose, ndoa ifungwe ndipo ufaidi matunda ya ndoa!.

Hivyo hata kama CCM, walichakachua, walidanganya, walihonga, waliiba na kufanya kila mbinu, anayetangazwa na tume kuwa ndiye mshindi, anakuwa ni "mshindi halali"
.
 
Last edited by a moderator:
Wakuu zangu Mkandara na Pasco,

Ni wazi kuwa JF ya siku hizi imepoteza mvuto kwa watu serious! Kwa kweli Pasco ameleta bandiko linalogusa epicenter ya ushindi wa CDM 2015! Surely ningetamani CDM wawemo humu, kama ZZK, JJM, TL na wengineo ambao naamnini wana uwezo kuchangia growth ya CDM!

Ni wazi kuwa kama CDM watabadili na kufanyia kazi kero chache chache zinazoelekezwa kwao, 2015 itakuwa huree kwao. Hata kama CCM watamsimamisha EL, CDM wana nafasi nzuri sana ya kubadili dola 2015! Waache mambo ya kubweteka na nyomi ya sasa, muda bado sana, sijui kama kuna strategies zozote serikali za mitaa, hapa ndipo wanapotakiwa kutumia uchaguzi huo kama "mtihani wa moko" kuelekea 2015!!

Pasco dont loose tamper, tutashindwa kumjua nani ni nani!!!

Sikupingi ndugu yangu:Lazima ipoteze mvuto kwa watu fulani1 ambao wapo very serious katika mambo fulani. baada ya kuingia watu fulani2

hembu replace hizo red na haya maneno:

watu fulani1:Fraudsters.
mambo fulani: Purchases.
watu fulani2:Auditors.

Pia unaweza cheza na maneno mengine kwa style hii.
usisahau soma hizi habari za CCM,ambazo zinaendela huku wewe ukiwa busy kusema lingine.
https://www.jamiiforums.com/jukwaa-...-na-vijana-wa-uvccm-huko-bububu-zanzibar.html
 
Sikupingi ndugu yangu:Lazima ipoteze mvuto kwa watu fulani1 ambao wapo very serious katika mambo fulani. baada ya kuingia watu fulani2

hembu replace hizo red na haya maneno:

watu fulani1:Fraudsters.
mambo fulani: Purchases.
watu fulani2:Auditors.

Pia unaweza cheza na maneno mengine kwa style hii.
Mkuu Nicholas, japo jf is meant to be the home of great thinkers, ili kiukweli sisi tuliopo sio wote ni ma great thinkers hivyo ukipost nondo kama hizi, muwege mtatufikiriaga na sisi!. Kama kwenye hii post mimi nimetoka kapa kabisa!, nil!, sijaelewa kitu!.
P.
 
Duh! Naona ndiyo unazidi kujikoroga kuhusiana na maana ya neno "Ridhaa"...Haya Mkuu Pasco huu ni ushahidi mwingine wa kuonyesha wewe ni gamba la kutupa. Mtanzania yeyote yule mwenye mapenzi mema kwa nchi yetu kamwe hawezi kuita ushindi kupitia uchakachuaji wa matokeo, udanganyifu, utoaji rushwa ya aina yeyote ile, wizi na mbinu zozote zile ambazo ni haramu wakati wa uchaguzi, yaliyotangazwa na tume ya uchaguzi wa magamba ni matokeo halali.
Mkuu BAK, issues za uhalali ni issues zinazofuata "sheria", "taratibu" na "kanuni"!. Kwenye "uhalali" wa ushindi wa JK kama rais halali wa JMT, tutaishia kubishana mpaka basi!. Nakuomba sana usiniletee maubishi kama ya Mzee Mwanakijiji kuhusu "uhalali wa Muungano.
 
Last edited by a moderator:
..Usiyakimbie maneno yako yanayoonyesha umagamba wako. Hayo maneno hayajaandikwa na BAK hivyo usitake kujibaraguza huku na kule kukimbia yale uliyoyaandika ambayo yanaonyesha dhahiri jinsi ulivyo karibu mno na magamba.

Hivyo hata kama CCM, walichakachua, walidanganya, walihonga, waliiba na kufanya kila mbinu, anayetangazwa na tume kuwa ndiye mshindi, anakuwa ni "mshindi halali"
 
Mkuu Nicholas, japo jf is meant to be the home of great thinkers, ili kiukweli sisi tuliopo sio wote ni ma great thinkers hivyo ukipost nondo kama hizi, muwege mtatufikiriaga na sisi!. Kama kwenye hii post mimi nimetoka kapa kabisa!, nil!, sijaelewa kitu!.
P.
Sidhani nini huelewi hapa.Naamini kama umesoma basic maths primary school unaelewa.Au hata kama umetumia M-Pesa utakuwa unafahamu wapi uweke nini.
Well,kila mtu anapitia stage fulani za kumfanya awe thinker then great thinker.Na wote hujifunza toka kwa wengine kwa njia nyingi ila si kwa kuwakwaza wengine.Kwa hiyo ni vyema kujifunza kwa wengine bila kujifanya mjuaji na kadiri mua unaenda utajikuta michango yako inaleta tija hata kama utakuwa tofauti na wengine.Uhalisia wa wa uchambuzi wako ndio utawashawishi wengine kukubalina nao.Na si mtu kujipitia njia na kujiita great thinker.By far wengi wetu si that great thinkers but honest people in discussions while allowing ourselves to learn new things.
 
Kwako wewe Pasco hata kukiwa na ushahidi wa kutosha kwamba mbinu haramu ambazo haziruhusiwi wakati wa kampeni kuelekea kwenye uchaguzi Mkuu zimefanywa na magamba basi Tume ya uchaguzi ya magamba ikitangaza kwamba magamba wameshinda basi hayo ni matokeo halali!!!! halafu unataka kutuzuga hapa jamvini, "Mimi Mtanzania sina chama najali maslahi ya nchi yangu."

Mtanzania yeyote anayejali maslahi ya nchi yake kamwe hawezi kuyaita matokeo ya uchaguzi ambao taratibu zake mbali mbali zilikiukwa kwamba ni matokeo halali.
 
Last edited by a moderator:
mkuu pasco wasiliana na invisible afunge huu mjadala naona tunaelekea kutoana macho sasa. Mwenye kusikia na asikie full stop. vp ile list ya fedha za uswiss ipoje mkuu? kama vp ni PM
 
mbona tulishafunga longtime..ni nyie tuu na side discussions zenu tuu.Happy nayi mmeshakuwa bored.
 
tupo pamoja nicholas ( sisi sote ni ndugu tatizo ni ccm). nitumie ile list ya uswiss kwa pm kama ulifanikiwa kuiona, hapa mtaani napata tabu sana naambiwa sie chadema sio lolote kwamba ndani ya ile list zito kabwe naye yumo. Nabishana nao hadi sasa sijashinda mkuu naona wananielemea.
 
...Mie niliamini ile list haitaondolewa hivyo sikuona umuhimu wa kuyarekodi yale majina, ila niliyaona yale majina mahali kwenye thread yenye kichwa cha habari "Hawa wamefanya nini?" Ngoja niyaangalie kama bado hayajafutwa nikiyaona basi nitakutumia ukiona kimya ujue ndio hivyo tena.

nitashukuru mkuu, hapa nilikuwa kwenye mchakato wa kuwashawishi hawa watu mtaani kwangu tufungue tawi la chadema. wamenibana sana hakijaeleweka.
 
Siku iona ila kama Zitto atakuwemo basi sidhani kama litashtua watu sana.Ila asipokuwepo pia halitashtua sana.Ila litammaliza zaidi yeye binafsi kisiasa kwani wapenda siasa wengi wana taabu kumuelezea.
 
Nguruvi3,heshma mbele,unaweza kuja hapa kuchangia mkuu ili tuelewane?nimeshindwa kuelewa naomba uje hapa utoe msaada.Ni ombi mkuu maana inaonyesha mnakubaliana na ndugu Pasco.

Tafadhali sana mkuu ningependa uje hapa,na ndugu Mchambuzi ambaye ulilizungumzia suala la things right vs right things,unaweza kuja hapa mkuu?maana ndugu Pasco amelitumia bandiko lako kwenye hoja yake,kama umemwelewa,naomba uje hapa kuelewesha wengine ambao tuna maswali. Wale ambao bado hawajawaelewa nyie ma great thinkers,ni ombi mkuu.
Mzee Mwanakijiji pia na wewe kwa mara nyingine,nakuomba uje hapa ili tuweze kueleweshana.Nilimwomba ndugu Pasco aniwekee link ya thread ili niweze kuona context ulyoitumia kuyasema maneno ambayo Pasco ameyatumia kama mojawapo ya kauli za kuiback up hoja yake.Ni muhimu mkaja na kutuelewesha.Natanguliza shukran!
Mkuu jmushi1, kwanza nimecheka sana kwa sentensi yako 'uje hapa tuelewane' it's well written. Heshima mbele mkuu.
Mimi nipo hapa na tuendelee na mnakasha.
 
Tunakusikiliza kwa makini mkuu,usibaki tu kule great thinkers,tunakuhitaji sana hapa mkuu kuliko unavyodhani.Mimi ushauri utakaoutoa,nitausikiliza bila wasi wasi wowote,kwasababu najuwa utakuwa ni ushauri genuine.Pengine kuna namna wengi wetu wanaweza kukubaliana na dhana ya chadema kujirekebisha,ila sidhani kama mleta mada ameiweka inavyotakiwa.This is the right time to do so.Pia hata thread unaweza kuanzisha huku.Ujumbe huu pia ni kwa wengineo ambao nilishawataja.Tuende straight kwenye point ili tutoe msaada sahihi wa mawazo kwa wapenda mabadiliko waliko ground kuwaelewesha wananchi.Nashukuru sana kwa kuelewa umuhimu wa uwepo wako humu.Sasa ni zamu yangu kusoma kwanza busara zako.
Thanks a lot.
 
...pia amesema ufisadi siyo hoja ya kuwakomboa watanzania,jambo ambalo sikubaliani naye kabisa.

Mkuu Jmushi1,

Ningependa kuchangia kidogo kuhusu suala hili la rushwa, hasa kwa kujaribu kujengea hoja kwanini rushwa ni hoja ya ukombozi. Naungana na wewe kupinga hoja kwamba Ufisadi sio hoja ya kuwakomboa watanzania. As a matter of fact, vita dhidi ya Ufisadi/Rushwa na ile dhidi ya umasikini lazima viende kwa pamoja, vinginevyo kuendeleza vita dhidi ya umaskini huku vita dhidi ya ufisadi vikilega lega, juhudi za kutokomeza umaskini hazitazaa matunda na tutaishia tu kupoteza resources nyingi sana pamoja na muda mwingi bure kwenye vita dhidi ya umaskini ambavyo havitamalizika.

Mabadiliko yoyote ya kisiasa, kijamii na kiuchumi yenye kulenga kuletea faida wananchi walio wengi hayawezi kufanikiwa bila ya kutokomeza rushwa; Rushwa/Ufisadi ni ‘an infection' kwenye juhudi za Maendeleo ya kisiasa, kijamii na kiuchumi. Ndio maana hata kwenye kwenye international development community, Suala la Rushwa/Ufisadi limeanza kuchukuliwa kama ‘a development issue' & ‘a development imperative';

Kwanini Rushwa ni hoja ya kuwakomboa watanzania?

Rushwa covers a wide spectrum, kuanzia rushwa ndogo ndogo/petty corruption to large scale/grand corruption. Tukianza na Petty corruption, ili mtanzania aweze pata huduma za msingi kabisa zinazosimamiwa na Bureucrats/Administrators kama vile Uhamiaji, Polisi, Ardhi, Elimu n.k, bila ya kutoa ‘kitu kidogo', normal bureaucratic procedures can't be accomplished; Mwalimu Nyerere alipokuja na kauli mbiu ya TANU dhidi ya Rushwa kwamba RUSHWA NI ADUI WA HAKI, SITATOA WALA KUPOKEA RUSHWA, aliliona hili kwani MASKINI HAWEZI KUPATA HAKI katika jamii inayoendeshwa kwa rushwa, na maskini tanzania ni zaidi ya 80% na hawa wanasubiria ukombozi kwa miaka 50 sasa;
Mpaka hapa, hoja kwamba rushwa sio hoja ya kuwakomboa watanzania inajishikilia wapi?

Tukiangalia aina nyingine ya rushwa - Large scale/Grand Corruption, hii inatokea pale ambapo a considerable amount of money inatolewa kama hongo ili kuwapatia watu fulani fulani preferential treatment au access kwa Rasilimali za watanzania ambazo walipewa na Mungu. Nyerere alitueleza kwamba ili kufanikiwa katika Maendeleo, moja ya vitu muhimu tunavyohitaji ni ARDHI, vingine vikiwa ni watu, siasa/sera safi, uongozi bora n.k. Tumeshuhudia jinsi gani wageni wanajinyakulia ardhi kwa kutoa rushwa huko kwa watawala; tunazidi kuona jinsi gani wawekezaji wanawawekea watawala mamilioni ya dola kwenye mabenki huko Uswisi na kupewa miradi ya madini, mafuta, gesi….miradi ambayo ina kila sura ya kijambazi na unyang'anyi kwani HAKI YA MUNGU aliyopewa mtanzania (rasilimali) inakuwa HAKI YA MZUNGU.
Pia kwa mfano mwingine huu mdogo tu, hoja kwamba Rushwa sio hoja ya kuwakomboa watanzania inajishikilia wapi.

Mtu anayetoa hoja kwamba rushwa sio hoja ya kumkomboa watanzania ni dhahiri anawatusi mamilioni ya watanzania waliotaka mabadiliko mwaka 1995 wakati wa Augustine Mrema na NCCR Mageuzi kwani nchi ilikuwa inanuka rushwa, jambo ambalo hata Nyerere alilisema sana; Kama tunaamini katika demokrasia, hasa katika dhana ya nguvu ya umma, umma ule kumuunga mkono Mrema kutokana na msimamo wake dhidi ya Rushwa ni maana kwamba Rushwa ni Hoja ya kumkomboa Mtanzania; Vile vile, katika nyakazi hizi, Chadema imejinyakulia umaarufu na kuungwa mkono na watanzania wengi sana (kwa mamilioni) kwani watanzania wengi wanaona hoja ya rushwa ina mashiko;vile vile the fact kwamba CCM inazidi kupoteza mapenzi mioyoni mwa watanzania wengi ni ushahidi tosha kwamba rushwa ni hoja ya kuwakomboa watanzania;

Nchini Tanzania rushwa imeshaota mizizi, na its ‘negative effects' imesha – multiply kwenye jamii. Katika Tanzania, Rushwa/Ufisadi umepelekea mamilioni ya watanzania kupoteza matumaini na hali zao za maisha, umezaa cynicism, hali ya kutoaminiana kwani watanzania wengi sasa wanaamini kwamba rushwa/ufisadi is a ‘norm'. Ufisadi/rushwa unazidi ku-undermine our social values kwa sababu watu wengi wanaona ni rahisi na inalipa kujiingiza katika shughuli za ufisadi/rushwa kuliko kutafuta shughuli au ajira halali;

Rushwa/ufisadi umeshapelekea mmomonyoko wa uhalali wa serikali ya CCM in the eyes ya watanzania wengi kwani mbali na madhara ya Ufisadi ambayo yanawanyang'anya watanzania ile HAKI YA MUNGU na kugeuzwa kuwa HAKI YA MZUNGU, vile vile petty corruption inapunguza kwa kiasi kikubwa sana ‘effective delivery' ya huduma za kijamii, na ni ahadi juu ya upatikanaji wa huduma za namna hii ndio ilipelekea watanganyika wengi kuiunga mkono TANU miaka ya 1950s na hatimaye kuisaidia TANU kutekeleza malengo yake ya ukombozi wa nchi;

Given all this, mtu anaweza vipi kuja na hoja kwamba Rushwa sio hoja ya kuwakomboa watanzania? Wakati tunazidi kushuhudia madhara ya rushwa/ufisadi katika upatikanaji wa huduma za kijamii kwa watazania walio wengi? Na pia jinsi gani ufisadi/rushwa unapelekea watanzania kuporwa HAKI YAO KUTOKA KWA MUNGU (Rasilimali) na inageuzwa kuwa HAKI YA MZUNGU?

Cha kuzidi kushanganza zaidi ni pale CCM (tofauti na TANU) kinapogeuka kuwa ni chama cha kujiuma uma kuhusu suala la rushwa/ufisadi. Pengine tunapoteza muda kujadili hoja hii kwamba rushwa sio hoja ya kuwakomboa watanzania bila ya kujua kwamba kumbe ina mahusiano na kujiuma uma kwa CCM; I don't know, Lakini yetu macho na masikio.
 
...Mkuu nayo imeshaondolewa....Siku hizi hapa jamvini ukiona habari nyeti basi inabidi kuipakua haraka sana kabla haijafutwa.

Mkuu Mchambuzi, asante kuibuka humu, nimenyofoa nondo yako ya utayari wa Chadema kushika dola 2015, naandaa closing remarks nifunge mjadala, kama una lolote la kuongezea, nitashukuru.
P.
 
Back
Top Bottom