...pia amesema ufisadi siyo hoja ya kuwakomboa watanzania,jambo ambalo sikubaliani naye kabisa.
Mkuu Jmushi1,
Ningependa kuchangia kidogo kuhusu suala hili la rushwa, hasa kwa kujaribu kujengea hoja kwanini rushwa ni hoja ya ukombozi. Naungana na wewe kupinga hoja kwamba Ufisadi sio hoja ya kuwakomboa watanzania. As a matter of fact, vita dhidi ya Ufisadi/Rushwa na ile dhidi ya umasikini lazima viende kwa pamoja, vinginevyo kuendeleza vita dhidi ya umaskini huku vita dhidi ya ufisadi vikilega lega, juhudi za kutokomeza umaskini hazitazaa matunda na tutaishia tu kupoteza resources nyingi sana pamoja na muda mwingi bure kwenye vita dhidi ya umaskini ambavyo havitamalizika.
Mabadiliko yoyote ya kisiasa, kijamii na kiuchumi yenye kulenga kuletea faida wananchi walio wengi hayawezi kufanikiwa bila ya kutokomeza rushwa; Rushwa/Ufisadi ni ‘an infection' kwenye juhudi za Maendeleo ya kisiasa, kijamii na kiuchumi. Ndio maana hata kwenye kwenye international development community, Suala la Rushwa/Ufisadi limeanza kuchukuliwa kama ‘a development issue' & ‘a development imperative';
Kwanini Rushwa ni hoja ya kuwakomboa watanzania?
Rushwa covers a wide spectrum, kuanzia rushwa ndogo ndogo/petty corruption to large scale/grand corruption. Tukianza na Petty corruption, ili mtanzania aweze pata huduma za msingi kabisa zinazosimamiwa na Bureucrats/Administrators kama vile Uhamiaji, Polisi, Ardhi, Elimu n.k, bila ya kutoa ‘kitu kidogo', normal bureaucratic procedures can't be accomplished; Mwalimu Nyerere alipokuja na kauli mbiu ya TANU dhidi ya Rushwa kwamba RUSHWA NI ADUI WA HAKI, SITATOA WALA KUPOKEA RUSHWA, aliliona hili kwani MASKINI HAWEZI KUPATA HAKI katika jamii inayoendeshwa kwa rushwa, na maskini tanzania ni zaidi ya 80% na hawa wanasubiria ukombozi kwa miaka 50 sasa;
Mpaka hapa, hoja kwamba rushwa sio hoja ya kuwakomboa watanzania inajishikilia wapi?
Tukiangalia aina nyingine ya rushwa - Large scale/Grand Corruption, hii inatokea pale ambapo a considerable amount of money inatolewa kama hongo ili kuwapatia watu fulani fulani preferential treatment au access kwa Rasilimali za watanzania ambazo walipewa na Mungu. Nyerere alitueleza kwamba ili kufanikiwa katika Maendeleo, moja ya vitu muhimu tunavyohitaji ni ARDHI, vingine vikiwa ni watu, siasa/sera safi, uongozi bora n.k. Tumeshuhudia jinsi gani wageni wanajinyakulia ardhi kwa kutoa rushwa huko kwa watawala; tunazidi kuona jinsi gani wawekezaji wanawawekea watawala mamilioni ya dola kwenye mabenki huko Uswisi na kupewa miradi ya madini, mafuta, gesi….miradi ambayo ina kila sura ya kijambazi na unyang'anyi kwani
HAKI YA MUNGU aliyopewa mtanzania (rasilimali) inakuwa
HAKI YA MZUNGU.
Pia kwa mfano mwingine huu mdogo tu, hoja kwamba Rushwa sio hoja ya kuwakomboa watanzania inajishikilia wapi.
Mtu anayetoa hoja kwamba rushwa sio hoja ya kumkomboa watanzania ni dhahiri anawatusi mamilioni ya watanzania waliotaka mabadiliko mwaka 1995 wakati wa Augustine Mrema na NCCR Mageuzi kwani nchi ilikuwa inanuka rushwa, jambo ambalo hata Nyerere alilisema sana;
Kama tunaamini katika demokrasia, hasa katika dhana ya nguvu ya umma, umma ule kumuunga mkono Mrema kutokana na msimamo wake dhidi ya Rushwa ni maana kwamba Rushwa ni Hoja ya kumkomboa Mtanzania; Vile vile, katika nyakazi hizi, Chadema imejinyakulia umaarufu na kuungwa mkono na watanzania wengi sana (kwa mamilioni) kwani watanzania wengi wanaona hoja ya rushwa ina mashiko;vile vile the fact kwamba CCM inazidi kupoteza mapenzi mioyoni mwa watanzania wengi ni ushahidi tosha kwamba rushwa ni hoja ya kuwakomboa watanzania;
Nchini Tanzania rushwa imeshaota mizizi, na its ‘negative effects' imesha – multiply kwenye jamii. Katika Tanzania, Rushwa/Ufisadi umepelekea mamilioni ya watanzania kupoteza matumaini na hali zao za maisha, umezaa cynicism, hali ya kutoaminiana kwani watanzania wengi sasa wanaamini kwamba rushwa/ufisadi is a ‘norm'. Ufisadi/rushwa unazidi ku-undermine our social values kwa sababu watu wengi wanaona ni rahisi na inalipa kujiingiza katika shughuli za ufisadi/rushwa kuliko kutafuta shughuli au ajira halali;
Rushwa/ufisadi umeshapelekea mmomonyoko wa uhalali wa serikali ya CCM in the eyes ya watanzania wengi kwani mbali na madhara ya Ufisadi ambayo yanawanyang'anya watanzania ile HAKI YA MUNGU na kugeuzwa kuwa HAKI YA MZUNGU, vile vile petty corruption inapunguza kwa kiasi kikubwa sana ‘effective delivery' ya huduma za kijamii, na ni ahadi juu ya upatikanaji wa huduma za namna hii ndio ilipelekea watanganyika wengi kuiunga mkono TANU miaka ya 1950s na hatimaye kuisaidia TANU kutekeleza malengo yake ya ukombozi wa nchi;
Given all this, mtu anaweza vipi kuja na hoja kwamba Rushwa sio hoja ya kuwakomboa watanzania? Wakati tunazidi kushuhudia madhara ya rushwa/ufisadi katika upatikanaji wa huduma za kijamii kwa watazania walio wengi? Na pia jinsi gani ufisadi/rushwa unapelekea watanzania kuporwa HAKI YAO KUTOKA KWA MUNGU (Rasilimali) na inageuzwa kuwa HAKI YA MZUNGU?
Cha kuzidi kushanganza zaidi ni pale CCM (tofauti na TANU) kinapogeuka kuwa ni chama cha kujiuma uma kuhusu suala la rushwa/ufisadi. Pengine tunapoteza muda kujadili hoja hii kwamba rushwa sio hoja ya kuwakomboa watanzania bila ya kujua kwamba kumbe ina mahusiano na kujiuma uma kwa CCM; I don't know, Lakini yetu macho na masikio.