Mkuu Richard, kwanza nakubaliana na wewe kuhusu msimamo wa Mwalimu Nyerere kwa EL, kiukweli Nyerere alikuwa mjamaa halisi kwa maneno na matendo!, alimdisqualify EL kwa kosa la utajiri, enzi za Mwalimu, utajiri ulikuwa dhambi!.
Baada ya Nyerere, alipofuata Mwinyi, CCM waliliua Azimio la Arusha na kulibakisha vitabuni tuu, waka li replace na Azimio la Zanzibar, sasa utajiri sio dhambi tena!. Kwa heshima ya Mzee Rukhsa, naomba nisiutaje ufisadi wake hapa, wala nisiutaje ufisadi wa Mkapa jinsi alivyofanya biashara Ikulu, na wala sitaji ufisadi wa JK, ndio maana aliyasamehe yale majizi ya EPA na ndiye mmiliki wa "lile zigo" hivyo CCM yote imeoza kwa mijizi, mifisadi na kwa rushwa, na kwa taarifa yako, mwenye afadhali ndio EL!. amini nawaambieni EL ndie safi, mkiujua uchafu wa hao mnaowadhania ndio agadhali, mtashindwa kuamini!.`
Maadam unajiapiza na kamwe, then, nakushauri pia jianfae kutaguta nchi ya kuhamia baada 2015!.
P.