Ni kuzuri tunapo kwenda kuliko tuliko to. Kwa sasa naona kimetokea chama cha upinzani cha ukweli kinacho fanya chama tawaka jujise usingizi.
Nakubaliana na walio tangulia kuwa uwezekano wa CDM kuchukua nchi uko pale kinacho subiriwa ni muda tu. Tukifikia hapo watanzania tutakuwa tumefikia kiwango kizuri sana kisiasa. Kwani tutakuwa tumefikia,uwezo wa kumpima mtu na kufanya maamu ya kusema huyu anafaa na huyu hafai.
Kwa ufupi kila chama nia yake kubwa, kulongoza dola, wanafanya lolote wawezalo kuongoza dola, wale walio kwenye dola walitakiwa kuwa na nguvu ya kuwamaliza hawa wano taka dola kivitendo, na sio kutumia mabavu au nguvu. Vitendo pekeyake vingewakata kelele wanao wania dola. Lakini kwa wale walio komaaa kisiasa( Tanzania tunapoelekea) Yule aliye kwenye system akikosea huwa anabadilishwa ili basi aingie yule aliye jipanga tayari. Kwani inawezekana tayari aliye kwenye system ameshaishiwa technique. Akae pembeni ajipange ili nae aje na mbinu mpya ya kuendeleza nchi. Hivi ndivyo walio endelea wananyo fanya.
Kwa Tanzania yetu ya leo, kila kona kumeoza, hakufanyi vizuri. Hii maana yake nini, inawezekana mfumo ni mbovu unaoongoza, na hawataki kubadilisha kwani unawapa wale walio kwenye system nafasi ya kuvimbisha matumbo yao. Lakini pia mfumo unaweza ukawa mzuri unakosa usimamizi. Kwani aliye pale ni mtoto wa refikiyangu mkubwa, aliyepale ni class met wangu, aliye pale ni mtoto wa kigogo, ndie aliyenifanya mimi niwe hapa nilipo, hivyo inabidi nilipe fadhira na mambo kama hayo.
Kwa ufupi kila kitu hakiendi kwaajili ya mtandoa. matokeo yake hali ya maisha inazidi kuwa ngumu kwa Mtanzania mmojammoja kadri siku zinavyo kwenda. Badala ya kuboreshwa. Kiasi kikubwa cha National Cake inaliwa na wachache wanao ishi maisha ya kifahari, kunyanyasa watu na kodi za watanzania, kwa ufupi wanaishi maisha ya kifisadi baada ya kufisadi pesa za watanzania.
Msingi wa mabaya yote haya ni kuwapo kwa kuto wajibishwa kwa wale wano haribu,mianya ya rushwa isiyo kemewa hata kidogo na viongozi wa juu kabisa wa serikali. Badala ya kuwa bana wala rushwa wakubwa( big fish) wana kimbiza na wanao toa shilingi elfu kumi kwa polisi. kukosekana kwa maadili ya uongozi na ubinafsi wa viongozi unopelekea kusign mikataba ya kishenzi isiyo na tija kwa watanzania,ila kuvimbisha matumbo yao. Kuwaandam wasema kweli kwa wananchi na kuwauwa( mfano Mwandishi waaabari aliyeuwawa)
Kwa upande wangu kuna kila sababu ya kuwapumzisha hawa walio serikalini kwa sasa na kujaribu wengine ili hawa nao warekebishe makosa yao wakiwa nje ya system. Kuna mazuri waliyo janya lakini kwa sasa wameshindwa kabisa kuiongoza nchi yetu. Tuna shindwa hata na nchi jirani ya Rwanda, ni nchi ndogo sana ukilinganisha na tanzania, lakini ni nchi ambayo tunaweza inuongozi ulio tukuka. Kwani Hauwezi kuzungumzia rushwa Kwannchi kama ya Rwanda. Tofauti ya mwananchi wa kawaida na waziri wa Rwanda ni ndogo sana. Hii ni ndoto kwa serikali ya sisiemu kufanya hayo na sela zake za kuleana na wana mtandao.
nakubaliana kwa asilimia mia kuwa chadema wanatakiwa kuingia kwenye system ili watoe haya matatizo kuliyonayo. Tunataka tufikie kiwango tumeondoka na swala la mafisadi na swala la rushwa, pia mtandao wanao rudisha nyuma maendeleo ya nchi yetu.
Watakapo kosea pia tutaweka wengine wenyenia ya kuongoza nchi yetu tukufu.
Ukweli ni kwamba sisiemu imeshindwa kabisa kuongoza nchi hii. Wameweza toka tulipotoka mpaka sasa, lakini huku tunapokwenda hawawezi, kikilichobaki ni kuanza kuuwa watu wanaofikisha ukweli kwa wananchi. watauwa watu wengi sana kama hawatatoka madarakani. kwani hawana democrasia ila ubabe tu. Kuna profesor mmoja wa chuo kikuu alisema wala tusishangae hili. ukweli ni kwamba nyama vyote vilivyogombea uhuru kwa hali arisi havina democrasia. Ndio maana wakitoka madarakani huwa vinakufa vyote. Mpaka sasa vilivyo baka katika Afrika nzima vinaesabia.
Mkuu Njopy, kwanza nichukue fursa hii kukukaribisha jf, nimekufuatilia tangu ulipojiunga, hii ndio post yako ya pili baada ya ile uliyo post June 21, yaonyesha wewe pia ni great thinker maana bado mgeni halafu unamwaga nondo za kufa mtu!.
Nimeupenda mchango wako na msisitizo nauweka hapo kwenye bold "kuna kila sababu ya kuwapumzisha hawa walio serikalini kwa sasa na kujaribu wengine"!. kumbe issue ni kuichagua Chadema ili kuwapumzisha CCM kufuatia kuichoka, na Chadema yeye tuichague kwa kujaribu!. Yaani tufanye majaribio kupitia Chadema!.
Ukiwa safarini na gari, huku huna kabisa spare tyre, utakapo pata pancha ya busrt ya tairi na ringi kupinda ambapo sasa sio tuu unatakiwa kuziba pancha, bali pia kununua tairi na ringi jipya!. Jee wewe utaondoka mbio kukimbilia dukani kununua tairi na ringi na kuja nalo kwenye gari na kulijaribishia kama litafiti, lisipo fiti unarudi tena dukani unaendelea kujaribishia mpaka upate litakalo fiti?,
Au utalifungua kwanza tairi la zamani, na kuchukua vipimo vyake hivyo kwenda dukani na kipimo cha kununua tairi na ringi lake kwa vipimo sahihi, hivyo ukifika tuu ni kulifunga tuu na kuendelea na Safari!.
Nchi yetu Tanzania ndio hilo gari bovu linakwenda kwa kuchechemea na CCM ndilo lile tairi bovu, Chadema ndilo, dereva ndio sisi wananchi. Kweli CCM tairi bovu ndilo hili na pale kwa mbali tunaliona tairi zima Chadema, jee tutalikimbilia tuu hilo tairi zima kichwa kichwa, na kulileta kujijaribishia ama kwanza tutaondoka na vipimo, na kwenda kulipima kwanza tairi hilo zima ndipo tulinunue tuendelee na safari yetu?!.
Sisi wana nchi lazima kwanza tulipime hili tairi jipya la Chaema kama lina fit vigezo vya gari letu. na sio kujichukulia tuu hilo tairi eti tuu kwa sababu letu la zamani CCM tumelichoka!. Hivyo vipimo ndivyo Chadema inapaswa kutueleza itanyanya nini and how?.
JK alikwisha onekana soft kite alikopita, alishindanishwa na watu makini kina Salim, Prof, Mwandosya, akawapita kwa sababu ana smile vizuri, Watanzania pia tukampa ushindi wa kishindo eti ili kumjaribisha!, matokeo ndio haya!.
Uchaguzi wa 2015, hatujaribishi tena, kama CCM itamsimamisha yule mgombea wangu, huyo uwezo, uimara, uthabiti wake unajulikana japo tatizo kidogo uadilifu wake ambao unarekebishika!.
Sasa Chadema ispokuja na anything new, fresh, practicable, then bora tuendelee na CCM na dereva wetu bingwa kuliko kufanya majaribio ya Ikulu yetu!.
P.