Elections 2015 Kuelekea 2015: Kama CCM Itamsimamisha Edward Lowassa...

Elections 2015 Kuelekea 2015: Kama CCM Itamsimamisha Edward Lowassa...

Kama kweli jamaa alikuwa msafi na anauchungu na wa TZ angewataja wa husika wa richmond ili wamuamini ni mtendaji na mtetezi. Bt jamaa kiukweli bila kuficha hafai tena hafai coz hakuona shida kuwasulubu wezi bali akabeba msalaba huo ambao hatautua kutoka mioyo ya watu up to the death. Namshauri ndoto hizo za mchana asiote tena. Wa TZ si maiti tena.

Kwanza kabisa majimbo ya Jiji la Arusha na Meru yamepotea kwa upinzani kwa sababu CCM imewasimamisha watu waliopandizwa nae. Sasa tunaomba aturudishie majimbo yetu kwanza. Leo Arusha imekuwa kama Syria. La hasha. Soma alama za nyakati. Akisimaishwa basi upinzani unachukua kilaini.
 
Tata nadhani hujanisoma vizuri na kunielewa.
Hakuna mahali nimesema namtaka au simtaki Lowassa ila nimeonyesha uwezekano wa Lowassa kuwa mgombea Urais wa CCM 2015 na uwezekano wa CHADEMA kutushinda kirahisi.

Hoja yangu sio nani anatufaa wanaCCM ili kuwashinda CHADEMA bali nimetoa tahadhari tu kuwa Mgombea wetu wa urais mtarajiwa(Lowassa) ni dhaifu sana kuweza kupambana kisiasa dhidi ya nguvu na kasi ya sasa ya CHADEMA.

Njia bora kwa chama changu kwa sasa ili kupata mgombea bora ni kuruhusu 'siasa safi' zianze kufanyakazi ndani na nje ya CCM. Kwa njia hiyo labda huenda litawaibua watu wema na wazuri kutaka kugombea urais.
Huenda hata mimi au wewe tukawa tunafaa tu!!

Nimekupata TanganyikaTANU labda tungeanza na Lowassa kama kipimo cha wagombea wa CCM na kwa kuwa tayari ni front runner nadhani ni kipimo sahihi. Ni vitu gani hasa ambavyo Mheshimiwa Lowassa hana ambavyo unadhani wengine wanaotafuta uraisi kwa tiketi ya CCM wanavyo? Kwa maana majina ambayo tayari tumeshayasikia mpaka sasa sioni aliye bora kuliko Lowassa. Kuhusu siasa safi nadhani hapa inabidi kuelimishana zaidi. Siasa safi ni zipi hizo unazoziongelea? Kutegemea kuwa CCM inaweza kupata mgombea bila kuwepo kwa makundi, kuchafuana, kutukanana, kutoa na kupokea takrima, kuibiana kura, mizengwe na mambo kama hayo ni sawa na kutarajia winter yenye barafu itokee Dar es salaam. Huo ndio mwelekeo wa kisiasa ambao CCM iliamua kuufuata kuanzia miaka ya mwanzo ya tisini na kwa sasa siyo rahisi kuuacha.
 
2015 lowasa u can go go go lowasa we love u

Binafsi sina tatizo/ugomvi na Komred Lowassa, lakini kuna haja gani ya kumsimamisha candidate ambaye kuna vidolee kadhaa havimzungumzii vizuri? Kwani wasafi kabisa wameisha hadi asimamishwe mtu ambaye usafi wake una maswali?

Sent from my BlackBerry 9380 using JamiiForums
 
Edward ngoyaye lowassa namfananisha na jamaa mmoja aliyekuwa na ukimwi huku akiwa na utajiri wa kutosha. Jamaa huyu baada ya kujijua kuwa ameathirika, alijitahidi kutumia nguvu za kifedha na kuwahonga wanawake wengi huku akiwaambukiza ukimwi. Walipokuja kushtuka walikuwa tayari ameisha waunganisha kwenye mtadao. Ukisha nasa hutoki.
Huu ndiyo utaratibu wa edward lowassa, ametumia fedha zake ambazo sijui anazipata wapi na kuwahonga viongozi wa dini, vijana na makundi mbalimbali ya kijamii. Lengo tinalijua anataka urais, lakini akisha pata kila mtu atatambua kuwa alikuwa ameathirika sasa ni kila mtu kusubiria kifo. Akisha ingia ikulu watanzania mtaelewa hatari ya kukukutana na mbogo aliyejeruhiwa, visasi vitatawala na ufisadi ndipo utakapochanua maua yake na kila mtu atatambua.

mjitu mingne bhana!!Lowassa,Lowassa!naona vijana wa membe mpo kazni,ila tambue kwmba mliko sasahv lowassa alshapita zaman,hata familia ya jk inajuw,hii nchi hatuwez kumpa joka la mdimu hata cik moja,jua liwake,mvua inyeshe,damu imwagike kamwe jk ndo atakuw wa mwisho kwny hyo familia kuw kiongoz,milele yote ci kizaz cha sasa wala kijacho wala cha kesho kutw wala cha mtondo,wala mtondo goo,kamwe imetosha na ukawambie hawa waliokutumaa,wakat mwngne kama huna kaz kajarib hata kuosha vyombo nyumban kwako,halaf eti ukienda nyumbn unaitw baba,nawaonea huruma sna ha wanakuita bab,hv wanatambuw kwli kuw mpaka utume sms jf ndo wale msosi?
 
Team Lowasa inayoongozwa na Pasco.

Sio dhambi kumpigia chapuo ENL

Lakini Mwalimu alisisitiza sifa za kiongozi ni muhimu kuliko jina.

Lowasa kama Pasco anavyotaka tuamini, kweli anaonekana anafaa. Lakini madudu ya Lowasa yameishaigharimu sana nchi hii tunayoiita 'masikini', alipokuwa bosi wa ardhi tulijipata na madudu, alipokuwa bosi wa maji tulijipata na madudu, alipokuwa waziri mkuu kwa muda mfupi tukajipata kwenye madudu ya shule za kata na elimu kushuka mpaka inatisha achilia mbali madudu ya richmond. Pamoja na kupanda kiuongozi Lowasa ni 'dramatic leader' yaani ni aina ya kiongozi anayehusudu maigizo maigizo hivi, hivyo uongozi wake unakuwa na kukurupuka na kuigharimu nchi sana tu. Halafu aina hii ya kiongozi ndio bora kabisa kwa vigezo na sifa za uongozi za Pasco. Aibu (!)
 
Lowasa hawezi kuwa Rais wa nchi hii hata siku moja, hii inalalia kwenye ukweli wa hotuba ya Mwalimu na Press Club.1995, DSM.

*CCM mkimweka mgombea dhaifu hakika hampiti!
*Moja ya sera za chama ni kuweka utaratibu usio na
mizengwe kumpata mgombea wa uraisi katika chama!


Kama kuna nyinyiemu anafikiria Lowasa ni mgombea thabiti basi jiandaeni kukabidhi madaraka!
NGUVU ya UMMA imoto! Itawaunguza hata mifupa.
 
Hadi wagonjwa wanataka urais yule atazikwa kabla 2015
 
wanaomuunga mkono EL wote ni akina NAY WA MITEGO raisi wa manzese
 
NI LOWASA 2015!

Watanzania, sasa, tunahitaji mtu practical zaidi!
Tunahitaji mtu atakayeturudishia utaifa wetu na mapenzi ya nchi yetu wakati huu ambao tofauti ya vipato imetugawa!
Tunahitaji mtu atakayewezesha wawekezaji wa ndani zaidi na kuinua mitaji yao!
Tunahitaji mtu mwenye mtizamo tofauti kabisa na viongozi wa awamu nne za awali kuhusu practical economy!
Tunahitaji mtu serious na atakayeangalia maslahi ya taifa thidi ya watu na nchi zinazoinyemelea nchi yetu na uchu wa ajabu!
Tunahitaji mtu atakayeiwekea nchi yetu misingi madhubuti ya kuinua 'technology' ya nchi kivitendo!
Tunahitaji mtu atakayewatumia wanataaluma wetu wa fani mbalimbali kikamilifu kuleta maendeleo endelevu nchini!
Tunahitaji mtu atakayekiongoza kizazi kipya kuthamini kazi na kujituma kwa bidii na maarifa kuliondoa taifa kwenye ulemavu wa utegemezi na kuinua heshima ya taifa letu kimataifa!
NINA IMANI KABISA EDWARD LOWASA ANAWEZA!
(Wanaopiga politiki endeleeni! lakini mumchague au lah, 'time will tell!)

 
Team Lowasa inayoongozwa na Pasco.

Sio dhambi kumpigia chapuo ENL

Lakini Mwalimu alisisitiza sifa za kiongozi ni muhimu kuliko jina.

Lowasa kama Pasco anavyotaka tuamini, kweli anaonekana anafaa. Lakini madudu ya Lowasa yameishaigharimu sana nchi hii tunayoiita 'masikini', alipokuwa bosi wa ardhi tulijipata na madudu, alipokuwa bosi wa maji tulijipata na madudu, alipokuwa waziri mkuu kwa muda mfupi tukajipata kwenye madudu ya shule za kata na elimu kushuka mpaka inatisha achilia mbali madudu ya richmond. Pamoja na kupanda kiuongozi Lowasa ni 'dramatic leader' yaani ni aina ya kiongozi anayehusudu maigizo maigizo hivi, hivyo uongozi wake unakuwa na kukurupuka na kuigharimu nchi sana tu. Halafu aina hii ya kiongozi ndio bora kabisa kwa vigezo na sifa za uongozi za Pasco. Aibu (!)
Kwanza rekebisha kidogo, sii kweli, na huwezi amini wala siko kwenye Team EL labda kwa jf!.
Jina lako nimelishika!, naomba tukumbushane ifikapo July 2015!, nikisahau nikumbushe, ukisahau nitakukumbusha!.
P.
 
Kwanza rekebisha kidogo, sii kweli, na huwezi amini wala siko kwenye Team EL labda kwa jf!.
Jina lako nimelishika!, naomba tukumbushane ifikapo July 2015!, nikisahau nikumbushe, ukisahau nitakukumbusha!.
P.

ha ha haa Pasco bana.

Kimsingi nimekufuta kwenye Team EL kama ulivyoshauri.

Tuombeane uzima ili tuifikie hiyo July 2015 na baada ya hapo.
 
Mkuu Mjuni Lwambo!, Pasco wa jf, sio mfuasi wa mtu yoyote, hana chama, hana upande na wala sio shabiki, ila anazungumza ukweli daima!. Wengi wanadhani jua linapochomoza Mashariki ile asubuhi, na kuzama Magharibi ile jioni, wengi wanadhani jua ndilo linalozunguka, hivyo huo ndio ukweli wao wanaouamini, ila ukweli halisi, ni jua limesimama hapo lilipo, ni dunia ndio inayozunguka!. Watu wanapenda kuushabikia ukweli wao lakini sio ukweli halisi!. Pasco wa jf, anasimama na ukweli halisi!. Subiria mpaka baada ya 2015 ndipo utawajua wafuasi halisi wa EL, mimi usinihesabu, kwa sababu kazi yangu ni kukupeni tuu ukweli halisi!.
P.
Pasco, kama huo ukweli halisi unaouzungumza una mfeva Lowasa basi wewe tayari ni shabiki wake, kuwa shabiki wake sio lazima uwe mwana CCM, unaweza ukawa mwanaCHADEMA au ukawa sio mwana chama wa chama chochote cha siasa.
 
Binafsi sina tatizo/ugomvi na Komred Lowassa, lakini kuna haja gani ya kumsimamisha candidate ambaye kuna vidolee kadhaa havimzungumzii vizuri? Kwani wasafi kabisa wameisha hadi asimamishwe mtu ambaye usafi wake una maswali?

Sent from my BlackBerry 9380 using JamiiForums

Nani haliyemsafi chini ya jua?
 
Back
Top Bottom