Elections 2015 Kuelekea 2015: Kama CCM Itamsimamisha Edward Lowassa...

Ovyo kabisa ww bila shaka umetoka kujaza utumbo wako wali ng'ombe na gongo maana najua leo wamaasai na walafi wote wanapiga foleni kwenda kula matapishi yao kwa lowassa fisadi mkuu, shame upon you, afadhali fisi maana ni fisi kweli kuliko ww, basi atakuwa rais wa ukoo wako na wenu ili mkalambe miguu yake,ccm ni kundi la wauaji ni wanaotumia miavuli ya umma kufanya uwizi,uaji na ubakaji wa raslimali zetu.
nilimchukia sana alipopata kashfa ya ufisadi mwaka ule, ufisadi uliopelekea ajiuzulu. Baada ya kumfuatilia sana nimegundua kuwa lowasa ndiye mtu sahihi wa kumpa kura yangu ya urais mwaka 2015.
 
Naona unajaribu kuharibu siku yangu!Wewe si ndio mmoja wa wale walioalikwa pilau na soda nyumbani kwake,na baadae mkamuhaidi kwamba mtampigia kampeni nchi nzima?
Mnatuaibisha vijana wenzenu bana!

Njaa zitawaua,yaani mnauza nchi kwa sababu ya pilau soda?
 
Wapenda mababiliko tuombe sana jamaa apitishwe na CCM kuwa raisi. Hii ni turufu kubwa sana kwa upinzani,tulieni.
 
Mgonjwa wa moyo na jambazi la mali za umma lililokubuhu!
Tunakukumbuka Hayati Mwalimu Nyerere..
 
Wanabodi,

Baada ya kumsikiliza kwa makini Waziri Mkuu "Mstaafu", Edward Lowassa katika two- series za kipindi cha Dakika 45 cha ITV, kwanza nimemkubali sana huyu jamaa!, pili kama yeye ndiye angekuwa rais, ile 2005, Tanzania tusingefikia hapa tulipofikishwa sasa na utawala wa JK!, ila kikubwa zaidi, (kama ni kweli afya yake sio mgogoro kama anavyodai mwenyewe kuwa yuko fit, japo he looks sick!), CCM ikimsimamisha yeye kugombea urais kwa tiketi ya Chama cha Mapinduzi, then matokeo ya urais kwa 2015, ni CCM tena!. Mkubali!..., mkatae!.

Hizi ni baadhi tuu ya sababu, kwanini CCM itashinda tena kwa ushindi wa kishindo kikuu, endapo and only if itamsimamisha Edward Lowassa!.

1. Uwezo wa Kusema, Kupanga, Kutenda na Kusimamia!.
Viongozi karibu wote waliopo CCM, wana uwezo mkubwa sana kesema!, tutafanya hiki, tutafanya kile!, ni maneno tuu! na pia wana uwezo mkubwa wa kupanga mipango kwa maneno tuu na sii matendo, au usimamizi, mfano mipanga kamambe kama (Mkukuta, Mkuza, Mkumbita, Mkurabita, na sasa Dira 2025)!. Mipango yote hii ni mizuri kwa maneno tuu, lakini wengi hawana uwezo wa kutenda na kusimamia utekelezaji!. Mipango mingi iliyopangwa, inaishia kwenye maneno na mabuku na makabrasha tuu, lakini utekelezaji kwa vitendo ni sifuri!. Kwa Edward Lowassa, yeye sio msemaji sana, bali ni mtendaji kweli!, yeye sio mtu wa maneno mingi!, ni mtu wa vitendo virefu!, he is an action oriented man!. Mfano hai ni pale alipokutana na madudu ya City Waters!, aliwafurusha there and then!. Hata madudu ya Richmond, alitaka kuwafurusha na kutaifisha kila kitu ila alishindwa!, kutokana na "mwenye mitambo!".

Tulipopata uhuru miaka ya 60, maadui wetu wakuu watatu, walikuwa ni Ujinga, Umasikini na Maradhi, na tulijiwekea misingi yetu mikuu minne ya maendeleo kuwa ili tuendelee, tulihitaji vitu vinne: Watu, Ardhi, Siasa Safi na Uongozi Bora!. Kwenye hiyo misingi, tulisema Pesa sio msingi, pesa ni matokeo!, hili ndilol lililokuwa kosa pekee la Mwalimu, kutofautiana na misingi ya ukweli ya uchumi, kama ilivyofundishwa na Adam Smith (land, labor, capital na interpreneureship)!. Kwenye ile misingi minne tulisahau capital kwa kudai "pesa sii msingi!".

Watu tunao na ardhi ya kutosha, yenye rutuba, vyanzo lukuki vya maji, madini, maliasili etc etc tunazo. Tulikuwa na tatizo kidogo la utekelezaji wa siasa safi ya Ujamaa na Kujitegemea na uongozi bora, ndio maana nchi tulizopata nazo uhuru, ile miaka ya 60, wao wakiwa ni masikini wa kutupwa kuliko sisi, with nothing, kana Tiger nations, leo wako mbali!, sababu pekee iliyowafikisha wenzetu pale walipo, wakati sisi tunaendelea kupiga mark time ni Elimu!. Sisi tulitaja tuu kuwa Ujinga ni adui, lakini we never invested on Elimu because we had no capital!. Nyerere aligombana na maprofesor wa uchumi, Kina Prof. Rweyemamu, wakajitimkia zao, akagombana Edwin Mtei na IMF, WB etc matokeo sote tunayajua!.

Lowassa na timu yake ya Boys II Men, walipoingia tuu madarakani, EL akafanya study tour ya nchi tulizoanza nao wakati wa uhuru!, kwanini wao wamefanikiwa, wako mbali na sisi wametuacha nyuma sana!, akagundua wali invest kwenye elimu!. Akarudi nyumbani, akahamasisha kila kata iwe na shule ya sekondari ili kila Mtanzania apate kwanza elimu, mengine yote, yatafuatia!. Baada ya kujengwa shule, zilikuwa zipatiwe vifaa na waalimu wa kutosha!.

Baada ya kujiuzulu, serikali ya JK ikazi abandon zile shule za EL ili kumkomoa!. Sasa zinaitwa St. Kayumba!. Mpango wa kufundisha waalimu wa ukweli, ukaachwa, nanachukulia wale failures wenye Div IV karibu na zero, na kuwa brush kwa miezi mitatu! (Waalimu wa Voda Faster!). Jana alipozungumzia umuhimu wa kuwaelimisha kwanza watu wetu, amenigusa sana!. Tungekuwa tumeelimika, tusingeibiwa hivi madini yetu!, tunaibiwa madini yetu huku tunaangalia kwa sababu hatuna elimu ya madini!, sasa tumegundua gesi,serikali inakimbilia kugawa vitalu kwa umiliki wa miaka 99 huku Watanzania hatuna hili wala lile kuhusu elimu ya gesi, hatuna sera wala sheria ya gesi!. Kwa kifupi, hutujui lolote wala chochote kuhusiana na gesi!, na tutaishia kuibiwa tena gesi yetu kwa kukosa elimu ya gesi!. Edward Lowassa ameshauri, hiyo gesi tuiache kwanza!, lets invest kwenye elimu kwanza kwa watu wetu, ili kuwa empower hawa watu wetu kielimu ndipo tuingie kwenye ambitious projects kama za kuvuna gesi, au kilimo kwanza etc!.

Kwa hili pekee, CCM ikimsimamisha EL, Tanzania itapata ukombozi wa kweli wa pili wa Mtanzania!.

Nimesema, CCM ikimsimamisha EL, 2015, itakuwa ni CCM tena, kwa sababu katika wapinzani wote, hakuna hata mgombea mmoja anayeweza kusimama na Lowassa kwenye urais wa 2015 na bado akaambulia kura!, there is no one!, none!.

Mwenye masikio na asikie!.

2. Dhambi Kubwa ya Lowassa ni Richmond Tuu!.

Najua wapinzani wa dhana ya ukweli, watakuja na hoja za dhambi kubwa ya Lowassa ni fisadi wa Richmond!, then time will tell, hiyo ni mizigo tuu ya watu, alijitolea kuibeba ili kwa kuteswa kwake, wao waokoke!, wakati muafaka ukifika, hili litawekwa wazi na Watanzania mtawafahamu wenye zigo lao haswa ni kina nani!. Wenye akili wameshang'amua ile metarmophosis process from Richmond -Dowans -Simbion na kwa msio jua, mkae mkijua Tanesco bado inailipa Simbion capacity charge ile ile ya dola 152 kama Richmond na Dowans, hivyo tumeruka majivu na kukanyaga moto, tumeruka maji na kukanyaga tope, na kwa usafi tumeruka nyasi, tukakanyaga ma..!.

3. CCM Haina zaidi ya EL na Upinzani hawana wa Kushindana Nae!.

Wanabodi ni mimi niliwahi kusema, CCM imechokwa na Chadema Haijajipanga, baadae nikasema CCM imechokwa mpaka basi!, Baada ya Chadema kuanza kujipanga nikasema Chadema, Njia Nyeupe Ikulu, lakini sasa baada ya kumsikia Edward Lowassa, kama ni kweli afya yake sii mgogoro kama anavyoonekana!, na CCM ikamsimamisha yeye, come 2015, then, mshindi wa uchaguzi wa 2015, ni CCM tena!, kinyume cha hapo, CCM ikimsimamisha mwingine yeyote, 2015, Chadema inachukuwa nchi kiulaini kama kumsukuma mlevi!.

Mwisho.

Namalizia kwa swali moja tuu, Jee CCM inaujasiri wa kuukubali ukweli huu mchungu wa kumsimamisha Edward Lowassa ili kuweza kujiokoa?! au itaendeleza kiburi uongozi na jeuri ya uchama tawala kusubiria kifo cha mende huki inajiangalia kwa kutegemea itaendeleza uking'ang'anizi wake kwa kuamini this time pia itashinda tena kwa kuutumia uwongo ule ule, na mbinu zile zile za uchakachuaji ule ule, kwa matarajio katiba mpya pia ita provide opportunities za aina ile ile ya miaka ya nyuma, kuwa ita endelea "to fool all the people all the times?!.

Asante.

Pasco.

NB. Japo Pasco wa JF sio mwanachama wa Chama chochote cha siasa, kwa CCM ni Pro Lowassa, kwa Chadema ni Pro ZZK na kwa CUF ni Pro-Jussa!.

Input ya Tanganyika Tanu.

Mkuu Tanganyika Tanu, pole sana, hii kitu yako imeunganishwa kwangu!. Ili kukutendea haki, nimeiweka kule juu kwenye main post.
Pasco.

Ataweza kuoga tope la Nyerere. Maana hilo gamba Baba wa taifa keshalikataa mbona mwalazimisha
 
Lowassa hafai. Hata jk alikuwa kama lowassa 2005,nyoka n nyoka awe mkiyan au kchwan.ccm n wabovu.
 
eti richmund ilikuwa ni mizigo tu ya watu kaibeba..kwahyo aliamua kuwapumcza watz ili kulinda watu flani? je sheria za nchi zinasema je juu ya mtu anaeshiriki ktk kuficha ualifu? je naje sii mualifu pia? tafakari....
 
Pasco,

Mie nimekuwa sikubaliani na Lowassa huko nyuma, lakini hivi sasa nimebadili mawazo nakubaliana na assessment yako. Siyo kwa sababu ulizoweka la hasha ila kutokana na mazingira halisi on the ground. Inafika wakati inatubidi tuwe realists kulingana na political environment tuliyonayo.
Modern day so called "democracy" - mwenye pesa nyingi kamwe hashindwi hata kama ni mbovu.

Angalizo: sijawahi kuwa mwanachama wa chama chochote na wala sio mshabiki wa mtu binafsi.

Nawasilisha.
 
Mnaipigia debe samaki iliyokwisha oza!HAINUNULIKI!

Kama kweli hakushiriki kwenye kashfa hiyo,wenzie walipomwaga mboga yeye angemwaga ugali!
Lakini akakaa kimya mpaka leo hii halafu anajidai anautaka 'urahisi',wakati hajasema ni akina nani ndo wahusika!
HANUNULIKI!
 
Mkuu umeandika maelezo mengi mno! Kwani kuna mwana CCM anaeukataa huo ukweli? Membe anaujua,Sitta analifahamu,Kikwete hata yeye analifaham hilo.
 
Ndugu yangu,

Juzi ulimwengu mzima ulikuwa unaomboleza na kusifu uadilifu wa Mzee Madiba. Wakati Nchi ya SA ilipokuwa inafungua ubalozi wake hapa Nchini, Mzee Madiba alimwambia Mwalimu kuwa, mtazame vizuri Edo, na uhakiki uadilifu wake.

Baada ya kumsikiliza kwa makini Waziri Mkuu "Mstaafu", Edward Lowassa katika two- series za kipindi cha Dakika 45 cha ITV, kwanza nimemkubali sana huyu jamaa!, pili kama yeye ndiye angekuwa rais, ile 2005, Tanzania tusingefikia hapa tulipofikishwa sasa na utawala wa JK!, ila kikubwa zaidi, (kama ni kweli afya yake sio mgogoro kama anavyodai mwenyewe kuwa yuko fit, japo he looks sick!), CCM ikimsimamisha yeye kugombea urais kwa tiketi ya Chama cha Mapinduzi, then matokeo ya urais kwa 2015, ni CCM tena!. Mkubali!..., mkatae!.

Hizi ni baadhi tuu ya sababu, kwanini CCM itashinda tena kwa ushindi wa kishindo kikuu, endapo and only if itamsimamisha Edward Lowassa!.

1. Uwezo wa Kusema, Kupanga, Kutenda na Kusimamia!.
Viongozi karibu wote waliopo CCM, wana uwezo mkubwa sana kesema!, tutafanya hiki, tutafanya kile!, ni maneno tuu! na pia wana uwezo mkubwa wa kupanga mipango kwa maneno tuu na sii matendo, au usimamizi, mfano mipanga kamambe kama (Mkukuta, Mkuza, Mkumbita, Mkurabita, na sasa Dira 2025)!. Mipango yote hii ni mizuri kwa maneno tuu, lakini wengi hawana uwezo wa kutenda na kusimamia utekelezaji!. Mipango mingi iliyopangwa, inaishia kwenye maneno na mabuku na makabrasha tuu, lakini utekelezaji kwa vitendo ni sifuri!. Kwa Edward Lowassa, yeye sio msemaji sana, bali ni mtendaji kweli!, yeye sio mtu wa maneno mingi!, ni mtu wa vitendo virefu!, he is an action oriented man!. Mfano hai ni pale alipokutana na madudu ya City Waters!, aliwafurusha there and then!. Hata madudu ya Richmond, alitaka kuwafurusha na kutaifisha kila kitu ila alishindwa!, kutokana na "mwenye mitambo!".

Tulipopata uhuru miaka ya 60, maadui wetu wakuu watatu, walikuwa ni Ujinga, Umasikini na Maradhi, na tulijiwekea misingi yetu mikuu minne ya maendeleo kuwa ili tuendelee, tulihitaji vitu vinne: Watu, Ardhi, Siasa Safi na Uongozi Bora!. Kwenye hiyo misingi, tulisema Pesa sio msingi, pesa ni matokeo!, hili ndilol lililokuwa kosa pekee la Mwalimu, kutofautiana na misingi ya ukweli ya uchumi, kama ilivyofundishwa na Adam Smith (land, labor, capital na interpreneureship)!. Kwenye ile misingi minne tulisahau capital kwa kudai "pesa sii msingi!".

Watu tunao na ardhi ya kutosha, yenye rutuba, vyanzo lukuki vya maji, madini, maliasili etc etc tunazo. Tulikuwa na tatizo kidogo la utekelezaji wa siasa safi ya Ujamaa na Kujitegemea na uongozi bora, ndio maana nchi tulizopata nazo uhuru, ile miaka ya 60, wao wakiwa ni masikini wa kutupwa kuliko sisi, with nothing, kana Tiger nations, leo wako mbali!, sababu pekee iliyowafikisha wenzetu pale walipo, wakati sisi tunaendelea kupiga mark time ni Elimu!. Sisi tulitaja tuu kuwa Ujinga ni adui, lakini we never invested on Elimu because we had no capital!. Nyerere aligombana na maprofesor wa uchumi, Kina Prof. Rweyemamu, wakajitimkia zao, akagombana Edwin Mtei na IMF, WB etc matokeo sote tunayajua!.

Lowassa na timu yake ya Boys II Men, walipoingia tuu madarakani, EL akafanya study tour ya nchi tulizoanza nao wakati wa uhuru!, kwanini wao wamefanikiwa, wako mbali na sisi wametuacha nyuma sana!, akagundua wali invest kwenye elimu!. Akarudi nyumbani, akahamasisha kila kata iwe na shule ya sekondari ili kila Mtanzania apate kwanza elimu, mengine yote, yatafuatia!. Baada ya kujengwa shule, zilikuwa zipatiwe vifaa na waalimu wa kutosha!.

Baada ya kujiuzulu, serikali ya JK ikazi abandon zile shule za EL ili kumkomoa!. Sasa zinaitwa St. Kayumba!. Mpango wa kufundisha waalimu wa ukweli, ukaachwa, nanachukulia wale failures wenye Div IV karibu na zero, na kuwa brush kwa miezi mitatu! (Waalimu wa Voda Faster!). Jana alipozungumzia umuhimu wa kuwaelimisha kwanza watu wetu, amenigusa sana!. Tungekuwa tumeelimika, tusingeibiwa hivi madini yetu!, tunaibiwa madini yetu huku tunaangalia kwa sababu hatuna elimu ya madini!, sasa tumegundua gesi,serikali inakimbilia kugawa vitalu kwa umiliki wa miaka 99 huku Watanzania hatuna hili wala lile kuhusu elimu ya gesi, hatuna sera wala sheria ya gesi!. Kwa kifupi, hutujui lolote wala chochote kuhusiana na gesi!, na tutaishia kuibiwa tena gesi yetu kwa kukosa elimu ya gesi!. Edward Lowassa ameshauri, hiyo gesi tuiache kwanza!, lets invest kwenye elimu kwanza kwa watu wetu, ili kuwa empower hawa watu wetu kielimu ndipo tuingie kwenye ambitious projects kama za kuvuna gesi, au kilimo kwanza etc!.

Kwa hili pekee, CCM ikimsimamisha EL, Tanzania itapata ukombozi wa kweli wa pili wa Mtanzania!.

Nimesema, CCM ikimsimamisha EL, 2015, itakuwa ni CCM tena, kwa sababu katika wapinzani wote, hakuna hata mgombea mmoja anayeweza kusimama na Lowassa kwenye urais wa 2015 na bado akaambulia kura!, there is no one!, none!.

Mwenye masikio na asikie!.

2. Dhambi Kubwa ya Lowassa ni Richmond Tuu!.

Najua wapinzani wa dhana ya ukweli, watakuja na hoja za dhambi kubwa ya Lowassa ni fisadi wa Richmond!, then time will tell, hiyo ni mizigo tuu ya watu, alijitolea kuibeba ili kwa kuteswa kwake, wao waokoke!, wakati muafaka ukifika, hili litawekwa wazi na Watanzania mtawafahamu wenye zigo lao haswa ni kina nani!. Wenye akili wameshang'amua ile metarmophosis process from Richmond -Dowans -Simbion na kwa msio jua, mkae mkijua Tanesco bado inailipa Simbion capacity charge ile ile ya dola 152 kama Richmond na Dowans, hivyo tumeruka majivu na kukanyaga moto, tumeruka maji na kukanyaga tope, na kwa usafi tumeruka nyasi, tukakanyaga ma..!.

3. CCM Haina zaidi ya EL na Upinzani hawana wa Kushindana Nae!.

Wanabodi ni mimi niliwahi kusema, CCM imechokwa na Chadema Haijajipanga, baadae nikasema CCM imechokwa mpaka basi!, Baada ya Chadema kuanza kujipanga nikasema Chadema, Njia Nyeupe Ikulu, lakini sasa baada ya kumsikia Edward Lowassa, kama ni kweli afya yake sii mgogoro kama anavyoonekana!, na CCM ikamsimamisha yeye, come 2015, then, mshindi wa uchaguzi wa 2015, ni CCM tena!, kinyume cha hapo, CCM ikimsimamisha mwingine yeyote, 2015, Chadema inachukuwa nchi kiulaini kama kumsukuma mlevi!.

Mwisho.

Namalizia kwa swali moja tuu, Jee CCM inaujasiri wa kuukubali ukweli huu mchungu wa kumsimamisha Edward Lowassa ili kuweza kujiokoa?! au itaendeleza kiburi uongozi na jeuri ya uchama tawala kusubiria kifo cha mende huki inajiangalia kwa kutegemea itaendeleza uking'ang'anizi wake kwa kuamini this time pia itashinda tena kwa kuutumia uwongo ule ule, na mbinu zile zile za uchakachuaji ule ule, kwa matarajio katiba mpya pia ita provide opportunities za aina ile ile ya miaka ya nyuma, kuwa ita endelea "to fool all the people all the times?!.

Asante.

Pasco.

NB. Japo Pasco wa JF sio mwanachama wa Chama chochote cha siasa, kwa CCM ni Pro Lowassa, kwa Chadema ni Pro ZZK na kwa CUF ni Pro-Jussa!.

Input ya Tanganyika Tanu.

Mkuu Tanganyika Tanu, pole sana, hii kitu yako imeunganishwa kwangu!. Ili kukutendea haki, nimeiweka kule juu kwenye main post.
Pasco.

[/QUOTE]
 
Mbona yeye hajasema. Anautaka? Na mimi nitakupa kura yangu sema kama unautaka mh. El.
 
Back
Top Bottom