Msanii
Platinum Member
- Jul 4, 2007
- 25,252
- 36,513
Kuna maswali wanajiuliza wananchi kuhusiana na kucharuka kwa wabuge wa Bunge la CCM kwenye kikao kinachoendelea huko Dodoma.
Napenda kuwakumbusha kwamba tusiwe wasahaulifu sana tukidhani wanaongea kwa maslahi ya nchi. Tujikite kwenye msingi wa hoja zao hasa kuchunguza vyanzo vya hizo hasira feki wanazozionesha leo.
TUJIULIZE
Tutegemee drama nyingi sana kwa sababu waliotengeneza matatizo na mkwamo mkubwa tunaoupitia ndiyo hao hao wanaojifaragua kuwa wana majibu ya matatizo hayo.
Drama za kiinterehamwe
Napenda kuwakumbusha kwamba tusiwe wasahaulifu sana tukidhani wanaongea kwa maslahi ya nchi. Tujikite kwenye msingi wa hoja zao hasa kuchunguza vyanzo vya hizo hasira feki wanazozionesha leo.
TUJIULIZE
- Ni Bunge lipi lilipitisha Bajeti 2022/2023 yenye miiba yote ya kuwachoma wananchi na walipakodi?
- Ni Bunge lipi walipitisha sheria wanazozilalamikia leo kuwa ni kandamizi?
- Ni Bunge lipi limekuwa linapokea ripoti za CAG na kukwepa eneo la uwajibishaji?
- Bunge linalalamikia ongezeko la deni la Taifa wwkati huohuo lilisimama kumuwajibisha Spika Ndugai aliyehoji kasi ya ukopaji uaipzingatia uhalisia wa uwezo wa kulipa?
- Tunavuna gesi ambayo hatuna haki ya kuipangia bei ya ugavi, leo tunawalaumu vipi wananchi wanaotumia nishati mbadala nje ya gesi huku tukiwapandishia bei hata kama soko la dunia bei imeporomoka?
- Tumewaondoa vijana kwenye ujasiriamali kwa kuwapiga marufuku wasifanye uchuuzi kupitia vitambulisho vya ujasiriamali huku wakiambiwa watapangiwa maeneo yao (hewa). Wengi wameshindwa na wakaingia makundi ya kihalifu na wanauawa kabla hakimu hajasoma hukumu...
- Mikopo ya 10% za Halmashauri imekuwa haitolewi lakini CAG anaelezea katika ripoti yake kuwa pesa inaenda kwenye vikundi visivyoeleweka na haijarudishwa
- Serikali ambayo kimsingi hupaswa kuendeshwa kwa mujibu wa sheria, inasimamia uvunjwaji wa sheria ya vyama vingi kwa kuzuia mikutano yote huku ikiwahadaa kwa kifurushi cha muafaka kuhusu haki zao kikatiba
- Malalamiko ya watumiaji wa huduma za bando kuhusu wizi na uonevu unaofanywa na makampuni ya simu hayapatiwi ufumbuzi badala yake mamlaka ya mawasiliano imewekeza kununua mitambo ya kufuatilia wananchi wanaoikosoa serikali na viongozi wake.
Tutegemee drama nyingi sana kwa sababu waliotengeneza matatizo na mkwamo mkubwa tunaoupitia ndiyo hao hao wanaojifaragua kuwa wana majibu ya matatizo hayo.
Drama za kiinterehamwe