brazaj wengine hatuuchukulii uchaguzi wa CHADEMA mwaka huu kama tu ni ishara ya demokrasia ndani ya chama, bali kama ni kipimo pia Cha uimara wetu.
Hofu ya watanzania kuhusu "kusambaratika" kwa chama kama Mbowe na Lissu wote wakigombea nafasi ya Uenyekiti Taifa, ni ishara ya ndani kabisa ya kuzoea utawala wa kisultani.
Kipimo kimojawapo cha demokrasia, ni kuheshimu Katiba ya taasisi husika. Mkutano Mkuu wa CHADEMA ndicho chombo cha juu kabisa cha maamuzi ndani ya chama.
Mwaka 2006 mkutano Mkuu wa CHADEMA uliamua kuondoa ukomo wa uongozi ndani ya nafasi zote za kiuongozi ndani ya CHADEMA.
Maana yake ni kuwa wenyewe CHADEMA waliamua mtu yeyote anayetaka nafasi yoyote ndani ya CHADEMA, anaweza kugombea mara nyingi awezavyo, bila ya kizuizi.
Mkutano Mkuu ukawekwa ukomo wa kugombea kwenye mikono ya wanachama wa CHADEMA. Yaani kikomo cha mtu kuwa kiongozi ni wapiga kura ndani ya CHADEMA kumkataa akigombea.
Na hili si jambo la ajabu Sana. Uongozi ndani ya chama si kama uongozi wa dola, lakini hata dola kuna nchi hazina ukomo wa mtu kuwa kiongozi wa nchi hizo.
Ujerumani ni mojawapo wa nchi hizo, Helmut Kohl na Angela Merkel waliongoza Kwa zaidi ya miaka 15 mpaka walipoondoka madarakani.
Ninachomaanisha ni nini. Wapiga kura wa CHADEMA wasifanywe hawana uwezo wa kufikiri jambo lipi ni bora kwa chama chao. Hata Sasa kuna minyukano ya hoja ndani ya chama kati ya wafuasi wa Mbowe na wafuasi wa Lissu.
Kitu pekee watu wanatakiwa kuhimiza, ni uchaguzi uwe wa wazi, huru na unaofuata misingi yote ya kidemokrasia ya CHADEMA.
Hoja ya nani agombee au nani asigombee ni hoja ya kipropaganda iliyoanzia CCM. Wajumbe wa CHADEMA wana akili timamu waachiwe wafanye maamuzi kwa niaba ya wanachama wenzao ambao si wapiga kura.