Kuelekea dakika ya tisini: "Maoni ya wanachama yasiposikilizwa, CHADEMA njiani kulia na kusaga meno!"

CHADEMA ikisambaratika CCM itapata ushindi mkubwa wenye kura chache kutokana na wanachi wengi kutoshiriki kupiga kura kwa kuwa hakutakuwa na mgombea mwenye mvuto wa upinzani atakayechuana na mgombea wa ccm. Ccm itazoa hizo hizo kura chache za wanachama wake watakaokwenda kumpigia mgombea wao
 
Vyama 14 hata vikiungana na kuwa na mgombea mmoja asiye na mvuto kwa wananchi ataishia kugeuzwa mbuzi wa hitma na kufanywa kitoweo na CCM iliyofanikiwa kuisambaratisha CHADEMA kimafia
 
sawa! Kwa hiyo ilikuwa ni kuzuga nchi wafadhili kuwa kuna vyama vingi?
 
hivi Lissu si TISS? Kama mbowe atang'ang'ania madaraka tutajua ni TISS kama hao wengine kina mrema, cheyo na lipumba. Nchi ni ya chama kimoja tu CCM, hivyo vingine vilivyoanzishwa ni magumashi tu. Tukapipe kura kwa hiyari tu kama kuna muda wa kuchezea kupanga foleni kwa zoezi hilo feki
 
Saa tano imefika, ajitokeze atoe tamko kama anagombea mitandao ifufurike mapovu na kama hatagombea apewe maua yake kwa kuimarisha demokrasia ndani ya chama
 

Kwani kuwa Tiss ni dhambi?

Au labda malaika wa kuikomboa hii nchi ungedhani ni kina nani au wanapatikana wapi?

Hadi tutakapoachana ni huu ulimbukeni wa kushukuiana wenye kuendekeza utengano uchwara, safari yetu bado sana.

Mbona kwingine Uganda au Kenya huko huu upumbafu haupo?

Au yale yale ya kuelekezana kwa kuhamia?

Tulishasema si nchi, si chama:

"Tutabanana hapa hapa!"
 
Huna hoja zaidi ya uchawa tu
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…