MTAZAMO
JF-Expert Member
- Feb 8, 2011
- 19,675
- 33,583
Wakuu,
Kipute cha Kariakoo deby kimekaribia, mimi kama shabiki wa Lunyasi nina maoni yafuatayo kuelekea siku hiyo.
1) Ubora wa Yanga ni Nabi, Nabi amefanikiwa kusumbua makocha wengi kimbinu sababu akili zao huzama kwenye wachezaji hatari kama Mayele kuliko akili ya Nabi. Kwa muda mrefu Nabi anamaliza game kipindi cha pili na makocha wameshindwa kudhibiti hilo.
2) Ubora wa viungo wa Yanga, sehemu ngumu na muhimu Yanga ni kiungo. Plan zote zinaanzia hapo na kufia hapo. Lazima uwe na viungo wenye intensity ya kutosha dakika zote ikibidi sub ili kulinda utimamu wa timu.
3) Fiston Mayele ni mchezaji hatari akiachwa peke yake maeneo hatari. Huyu akiwa maeneo mengine apewe uhuru lakini akiwa kwenye 18 lazima awe na destructive player kama Putin. Akiwa peke yake mpira ukamfikia akiwa kwenye hatari mtaufuata nyavuni.
4) Kama nilivyosema Nabi game ngumu anashinda kipindi cha pili. Sub zake na mabadiliko ya positions uwanjani kipindi cha pili lazima haraka sana yafanyiwe home work na ku switch plan. Makocha wengi wa bongo wakiona 1st half wana droo au wanaongoza wanafikiri wamekamata game kumbe kipindi cha pili Nabi ndio anacheza baada ya kujua strength and weakness za mpinzani.
Hitimisho:
Kocha Robertinho ameifunga Yanga mara mbili na amefanikiwa kwa aina ya soka alilokuwa akitumia huko. Mara nyingi anacheza direct football na double striker! Huu mfumo ni complicated kueleweka kwa mashabiki hasa wa Simba!
Kocha wa Simba ni hatari timu yake ikiwa haina mpira kuliko ikiwa na mpira! Hili imechukua muda wachezaji kumuelewa na sasa wameingia kwenye mfumo.
Kama wachezaji wakifata maelekezo yake vizuri na pia kama kocha mwenyewe akimzidi ujanja Nabi hasa kipindi cha pili basi Simba atashinda goli nyingi.
#nguvumoja