Tanzania imeandaa Dira Mpya ya Maendeleo ya 2050 ambapo utekelezaji wake utaanza rasmi mwaka 2025/26 baada ya kujadiliwa na kupitishwa na Bunge kabla ya Rais kuidhinisha rasmi.
Kwa Sasa Serikali imezindua rasimu na ambapo zoezi la maboresho linaendelea ikiwemo kutoa maoni.
Sasa Kwa wapanga mipango pamoja na kuweka malengo ya kuwa na GDP ya $ 700bln na per Capita income ya $4700 by 2050 napendekeza pia tuweke kigezo Cha kiushindani na Nchi zingine Ili tuwe tunajipima na wengine.
Tunapoanza utekelezaji wa Hiyo Dira Natamani inapofika mwaka huo au kabla ya mwaka huo basi Tanzania iwe ni Kati ya Nchi 5 Zenye Uchumi mkubwa Barani Afrika ambapo tunatakiwa kutoka nafasi ya 10 tuliyoko Sasa Hadi kufikia nafasi ya 4 na kama.tukishindwa basi tuwe nafasi ya 5.
Tanzania tuna sababu na vigezo vyote vya kufikia nafasi ya 4 Kwa kuanzia na Rasilimali asili zilizopo.
Nafahamu Kila Nchi Ina Mali asili lakini Kwa Tanzania tutakuwa na advantage ya idadi kubwa ya watu.
Kwa Sasa Tanzania ni namba 5 kwa Wingi wa watu hapa Afrika na bila shaka tunaendelea kuwa namba 5 miaka Mingi ijayoa Sasa inatakiwa tutumie Wingi wetu kuwa fursa ya soko na Uchumi Ili tukuze Uchumi wa Nchi yetu.
Kama tumeweza kuingia top 10 Kwa nini tushindwe kuwa namba 4?
View attachment 3174529
Hivyo basi by 2050 ni matumaini yangu kwamba Msimamo wa Ligi ya Uchumi Afrika Mwaka 2050 utakuwa kama ifuatavyo.,
1.Nigeria
2.Egypt
3.Ethiopia
4.Tanzania
5.Algeria
6.South Africa
7.DR Congo
8.Morocco
9.Angola
10..Kenya
11.Ivory Coast
12.Uganda.