Kuelekea Euro 2016: Timu zipi unazipa nafasi ya kufanya vyema?

Game over na Switzerland wanashinda mechi yao ya kwanza kwa goli 1-0

Tunasubiri mechi kabambe kati ya Switzerland na France.

Hakuna chance kwa Romania na Albania kwenye kundi hili.
 


Diamond yupi, huyu huyu wa kiduku?
 
Diamond yupi, huyu huyu wa kiduku?



Mkuu ni mfumo wa uchezaji wa timu unaitwa hivyo

lol

Ukiangalia huo mfumo, wachezaji wa kiungo namba 6, 7 10 na 8 wanaunda umbo la Diamond.

Namba 6 anacheza kama DM na analinda back four na namba 10 anakuwa kishughulika kama AM ambayo kwa England atakuwa Wayne Rooney akiwasaidia washambuliaji namba 11 na 9.

Ndio maana Wayne Rooney anatumiwa kutafuta nafasi kwa kusaidia kuchukua mipira kutoka eneo lake na kuipeleka kwa washambuliaji wake na wakati huohuo akiweza kufunga kama anapata nafasi.

Namba 8 na 7 Deli Ali na Adam Lallana watakuwa wakilinda shemu ya kati wakiwa nyuma ya namba 11 na 9.

Jamie Vardy ataanzia bench.
 
Ningekuwa Kocha Wa England, Starege Angeanzia Benchi Maana Show Nyingi Mpira Si Kivile.
 


Mkuu kila team siku hizi inacheza mtindo huo. Mpira umekuwa diffensive sana kuliko miaka ya nyuma. Kwa mtindo huo timu itakayokuwa na kiungo mahili na forward inayoweza kupokea mipira na kupenya ndio itakayoshinda. Au magoli yapatikane kwa counter attack
.Kwahiyo usitoe maelezo mengi kama England wanakuja na jipya. La hasha
 

Siipi nafasi sana England kwani hawana uzoefu sana na safari hii wana wadogo wengi.

Kwa ngazi ya klabu kuna mifumo tofauti kama ule wa 4-4-2, 4-2-3-1 na 5-3-2 inategemea na mazingira na aina ya wachezaji ulio nao.

Ila katika ngazi ya timu ya taifa inataka ujuzi sana kwani wale wachezaji wote hodari wanatawanyika na wanakuwa wakichezea nchi zao, hivyoinabidi kujipanga hasa.
 
in fact tutashuhudia game nzuri ila #England akicheza leo kichapo kitamhusu na #russia akizembea atakula nyingi tuu.
 
Mechi inayofuata Wales na Slovakia uwanja wa Nouveau Stade de mjini Bordeaux.

Team News:

Wales (5-3-2). Ward, Gunter, Taylor, Davies, Chester, Williams (c); Ramsey, Edwards, Allen, Bale, J Williams.

Slovakia (4-5-1). Kozacik, Pekarik, Skrtel (c), Durica, Svento, Mak, Kucka, Hrosovsky, Hamsik, Weiss, Duris.

Mwamuzi ni Svein Moen kutoka Norway.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…