Kuelekea Euro 2016: Timu zipi unazipa nafasi ya kufanya vyema?

Kuelekea Euro 2016: Timu zipi unazipa nafasi ya kufanya vyema?

Natizama TV Mashabiki wa Wales kwenye viwanja vya nchini kwao Watu wanarushiana Maji Maji ya Beer juu ila sio mtu Kurusha simu yake tehtehteh! mtu anaweza kushangilia akaachia Glass ila sio Smartphone.
Lazima wafurahi..Ndo mara ya kwanza kuingia nusu fainali ya uero. Hawakutegemea kufika huko
 
Haya bana kumbe tz tunaweza kuwa juu ya nigeria na ghana au ivory cost tunafanyiwa figisu figisu

Algeria ya 32, Ivory Cost ya 36, Ghana ya 37, Senegal ya 41, Misri ya 45 na Tunisia ya 47.

Na hata visiwa vya Cape Verde yenye watu 513,9000 ni ya 49!

Hizi timu za Afrika zimo katika 50 bora Duniani.
 
Haya bana kumbe tz tunaweza kuwa juu ya nigeria na ghana au ivory cost tunafanyiwa figisu figisu

Kuna mahali nimetaja figusu ?
Kwa Ulaya ukiacha Ufaransa na Ujerumani kwa sasa
Belgium wana talented players kuliko timu nyingi lakini wanakosa kocha wa kutengeneza timu ya ushindani.Kuna nchi hazina talented players lakini makocha wametengeneza timu za ushindani (Italy,Wales,Iceland,Croatia)
 
Jumatano usiku itakuwa ni usiku wa mgongano wa galasticos wawili Gareth Bale na Cristiano Ronaldo.

Lazima Lyon ichimbike.
 
Belgium watafute kocha kutoka Italy,Germany au Holland atengeneze timu kabla hawa wachezaji hawajazeeka
 
Kuna mahali nimetaja figusu ?
Kwa Ulaya ukiacha Ufaransa na Ujerumani kwa sasa
Belgium wana talented players kuliko timu nyingi lakini wanakosa kocha wa kutengeneza timu ya ushindani.Kuna nchi hazina talented players lakini makocha wametengeneza timu za ushindani (Italy,Wales,Iceland,Croatia)

Ni kweli kabisa mkuu, na hili tatizo wanalo pia Holland ingawa wamekuwa na mameneja wazuri kam Gus Hiddink na LVG.

Ila kwa Belgium ni special case kwasababu hawajawahi kuwa na wachezaji wa kiwango cha juu kabisa ukilinganisha na Germany au France ambao wamecheza kwenye fainali bila kuwa majeruhi.

Lakini wana academy nzuri sana hasa pale Anderlecht walipotoka Lukaku na Hazard na wengine.

Kocha wao wa sasa Wilmots ni kocha mzurio na ndie aliewawezesha Belgium kucheza hii Euro 2016 baada ya WC 2014.

Tungoje tuone Euro 2020 itakayofanyika Belgium kama nchi hiyo itakuwa imefikia kiwango gani cha uchezaji .
 
Belgium watafute kocha kutoka Italy,Germany au Holland atengeneze timu kabla hawa wachezaji hawajazeeka

Belgium wala hawahitaji meneja mgeni kwani huyu walie nae sasa Marc Wimots ni kocha mzuri tu.

Tatizo ambalo Belgium wanalo ni kucheza bila mfumo na mpango Fulani yaani wanapocheza wanaacha nafasi kubwa katikati na timu pinzani wanatumia mwanya huo kama Italy walipowafunga 2-0 kwenye mechi ya makundi.

Lakini wakarekebisha kidogo tatizo hilo na hawakufungwa goli hata moja na Ireland, Sweden wala Hungary.

Hivyo ile nafasi kubwa kati ya mabeki na wachezaji wa kiungo leo imetumiwa vema na Gareth Bale na Aaron Ramsey kumsaidia Hal Robson Kanu na wenzake kuweza kufunga magoli matatu kirahisi.

Belgium wana wachezaji wazuri sana ambao meneja ameshindwa kuwafanya kuwa wachezaji wanaocheza kama timu na kuwa na lengo moja la kucheza kwa kusaidiana kutafuta ushindi na ndio maana Eden Hazard, De Broune, Lukaku na Batshuayi wameonekana si kitu na wachezaji wasioelewana uwanjani.
 
Ni kweli kabisa mkuu, na hili tatizo wanalo pia Holland ingawa wamekuwa na mameneja wazuri kam Gus Hiddink na LVG.

Ila kwa Belgium ni special case kwasababu hawajawahi kuwa na wachezaji wa kiwango cha juu kabisa ukilinganisha na Germany au France ambao wamecheza kwenye fainali bila kuwa majeruhi.

Lakini wana academy nzuri sana hasa pale Anderlecht walipotoka Lukaku na Hazard na wengine.

Kocha wao wa sasa Wilmots ni kocha mzurio na ndie aliewawezesha Belgium kucheza hii Euro 2016 baada ya WC 2014.

Tungoje tuone Euro 2020 itakayofanyika Belgium kama nchi hiyo itakuwa imefikia kiwango gani cha uchezaji .

Holland huwa na kikosi kizuri tatizo lao miaka yote ni defence mbovu na huwa wanatolewa na timu nzuri (Brazil,Argentina,Spain).Wilmots alisifiwa sana kuipeleka timu WC 2014 lakini wakachemsha ,kuipeleka timu Euro 2016 sidhani kama ni mafanikio huu mfumo wa timu 24 tumeona timu nyingi vibonde zimefuzu (Hungary,Ireland,Wales,Iceland,Austria).Alipofikia panatosha hatari ni hawa wachezaji(Cortous,KDB,Hazard,Dembele,Carasco,Vertoghen,Lukaku,Witsel,Batshuayi,Martens)wakizeeka itachukua muda sana kupata wachezaji kama hao.
 
Haya sasa zamu ya Italy kung'olewa imeshawadia. Na wasipoangalia Germany wanaweza wakawaaibisha kabisa kwa kupigwa bao 4.
 
Toka enzi na enzi...rekodi zinaibeba zaidi Italy kuliko Ujerumani.

Wanapokutana kwenye Robo au Nusu iwe Euro au World Cup, Ujerumani hufungwa.

Je leo wataweza kugeuza historia?
 
Italy wakicheza kama walivyocheza mechi za nyuma basi ni lazima wawapige hawa Wajerumani at least kwa 2-0. Italy wanacheza kwa determination kubwa sana na pia wanacheza mpira ambao washabiki wengi tunaupenda, attacking football.

Italy vs German..Timu gani unaipa nafasi leo.
Leo pagumuuuu.
 
Italy wakicheza kama walivyocheza mechi za nyuma basi ni lazima wawapige hawa Wajerumani at least kwa 2-0. Italy wanacheza kwa determination kubwa sana na pia wanacheza mpira ambao washabiki wengi tunaupenda, attacking football.
Ni kweki mdau..Ila German nao idara zote zimekamilika.
 
Back
Top Bottom