Kuelekea Euro 2016: Timu zipi unazipa nafasi ya kufanya vyema?

Kuelekea Euro 2016: Timu zipi unazipa nafasi ya kufanya vyema?

nitashangiliaje timu ya Rubaman na Piers Morgan? basi Final sishangilii timu nitakuwa Refa.

Piers Morgan anatafutaga kicks za nguvu. Arsenal wakicheza vizuri yupo upande wa Wenger wakiboronga tu unamsikia anakuja negative. Sijui alisemaje England walivyotolewa na Wales kwenda Semi final?
 
Wamecheza kwa nguvu dakika zote 90 au ukuona walivuoanza game. Dakika ya 15 mpaka 30 wajerumani walishambulia mkaona ile ndio game, no. Germany walikuwa na possession kwasababu France wanacheza defensive game na hiyo ndio trending football 2016. Mlikuwa mnaangalia mashati meupe tu lakini France deserved to win the game. Griezmann peke yake kapiga 7 shots on target, then what more do you want?
Pagan wewe ni noma sasa nasubiri prediction yako kuhusu final
 
Mark Clattenburg akipewa kuwa refa Final sitizami mpira jamaa anavigezo gani hata haya Mashindano anapewa nafasi? na yule refa wa Man U mwembamba? bora Michael Oliver.

Mark Clattenburg ndiye refa bowa wa nchi yenu tangia Howard Webb astafu

Wampe tuu Final apulize kipyenga
 
Portugal anaweza kushinda hili kombe. Ingawaje hawajacheza vizuri tokea mwanzo timu yao inaweza kuforce draw ikabeba kwa penati.Hawa France nyuma sio wazuri kihivyo wanaweza kwenda usingizini CR7 akawagonga kwa vichwa.

Katika mechi zote za Portugal naona ya jana ndio walicheza vizuri, ila hata wafaransa na wao wapo wapo tuu

Naona timu yeyote inaweza kuchukua ubingwa huu
 
Katika mechi zote za Portugal naona ya jana ndio walicheza vizuri, ila hata wafaransa na wao wapo wapo tuu

Naona timu yeyote inaweza kuchukua ubingwa huu
True na hasa toka Sanchez aanze kucheza kati pale.
 
Mark Clattenburg akipewa kuwa refa Final sitizami mpira jamaa anavigezo gani hata haya Mashindano anapewa nafasi? na yule refa wa Man U mwembamba? bora Michael Oliver.
Mbaya wako kapewa,tayari ndo imetanganzwa kuwa Mark Clattenburg ndo atakaekuwa refa hapo stade de France,Portugal v/s France
 
Kombe kwa France hili hakuna namna
Kwa tunayoifahamu les bleus na maajabu yake wala hata hatushangazwi na kipigo alichopewa ujerumani jana.

Ni hali ya kawaida sana france kuziangusha timu ambazo ni heavy favorites michuano inapofanyikia aridhi ya nyumbani, na tena mara nyingi anakuwaga wa kawaida sana yaani kma kuna star basi anakuwepo mmoja au wawili na hutoa matokeo ya kushangaza.

Ukirudi nyuma mwaka 1998 kwenye michuano ya kombe la dunia iliyofanyikia ufaransa, hatua za awali ufaransa walifanya vizuri sana ila kwenye mtoano hadi wanafika fainali.. 16 bora walipita kwa goli la dhaabu dhidi ya paraguay, hatua ya robo fainali walipita kwa matuta dhidi ya italy na hata nusu fainali walimtoa kwa mbinde crotia na ushindi wenyewe ilikuwa ni kwa kutoka nyuma hatimae kushinda 2-1.. hivyo basi unaweza kuona hata kufika kwao fainali ilikuwa ni kwa kusua sua tu.


Sasa game ya fainali ilienda kutengeneza maajabu yake ambayo hadi leo wabrazili bado hawajaamini 100% kilichotokea. Timu bingwa mtetezi iliyokuwa na wachezaji tishio kama Bebeto,Rivaldo,Carlos,Denlson,Ronaldo dhidi ya vijana wadogo wakiwa chini ya Aime jacque akina Pires,Petit,Marcel Desailly,Trezguet,Bixente Lizarazu,Your Djokeaff na mfalme Zizzou.

Hadi dakika 90 zimamalizika bingwa mtetezi alikufa 3-0 pamoja na dominance ya ball possession za kufa mtu na kucheza dhidi ya timu pungufu kwanzia dk ya 68 baada ya red card ya marcel dessailly. star wetu alikuwa ni mmoja tu kipindi hicho lakini aliichachafya timu nzima ya brazil kila aliposhika mpira YAZIDI.

Na hata mwaka 2000 kwenye michuano kma hii hii, game ya nusu fainal dhidi ys ureno pamoja na ureno kutangulia kupata bao lakini bado walipelekwa nje kwa goli la dhaabu.

Same situation happened in the final game against italy, up to 90" the whole world had already written france off, only last 13 seconds in the injury time were enough for Slyvio Woltord to send the tie into extra time ambapo David Trezguet kabla hata dakika nne hazijasha alipeleka msiba wa kihistoria kwa wataliano.


SASA UNAWEZA KUONA JINSI GANI UFARANSA ILIVYOKUWA NI TIMU YENYE BAHATI KWENYE MICHUANO MIKUBWA WANAPOFIKA HATUA ZA MWISHO JAPO NA UWEZO NAO UNACHANGIA, MWAKA PEKEE ULIYOKUWA NA GUNDU KWAO NI 2006.

PAMOJA NA HAYO KUELEKEA FINAL DHIDI YA PORTUGAL KWA UWEZO WA KITIMU NA SABABU ZA KIMAZINGIRA NAONA KAMA UFARANSA ANAENDA KUKAMILISHA TU RATIBA NA KUKABIDHIWA UBINGWA WAKE.

SITEGEMEI KUONA UPINZANI MKALI WOWOTE KUTOKA KWA PORTUGAL... SANA WATACHEZA MIPIRA YA KUVIZIA VIZIA TU HASA MIPIRA YA JUU..
 
Utabiri wangu naipa ureno ingawa timu zangu zilikuwa Wales, German na France , kwanini Ureno

#Michuano hii tumeshuhudia uwepo wa timu mpya kabisa katika big tournament kama Wales, Iceland ... na mwisho wa siku zikafanya vizuri sana

#Tumeshuhudia German kufuta uteja kwa Italy (na good penati kutoka kwa brother Zaza [emoji41] joke )

#Tumeshuhudia France kuifunga German kwa mara ya kwanza kwenye big tournament tangia mwaka 1958

#Tumeshuhudia best looser timu pekee inayoshinda kwa ngekewa kufika final

Ingawa wengi hawaipi nafasi Ureno ila mimi naweka bet yangu kwao

Hizi ni tabiri zangu

Game itaisha ndani ya dakika 90+
Kadi za njano nyingi
2 red cards
Girroud atakosa magoli ya wazi
Ureno 3 - France 1
- mpaka half time France ataongoza
- Ureno watasawazisha kupitia beki
-goli la ushindi litafungwa dakika ya 92 counter attack

#TeamFrance tusameheane wacha tu #CR7 achukue kombe
 
Back
Top Bottom