Kuelekea hatua ya Makundi Ligi ya Mabingwa Afrika, AS Vita Club dhidi ya Simba SC, Injinia Ngapi?

Kuelekea hatua ya Makundi Ligi ya Mabingwa Afrika, AS Vita Club dhidi ya Simba SC, Injinia Ngapi?

Kuelekea hatua ya makundi ya ligi ya mabingwa Afrika, baada ya kuwakwaruza vilivyo JS Saoura ya Algeria, kwa mikwaruzo mitatu bila majibu, DOZI Kimataifa kuendelea.

..Mwana Kulitaka Mwana Kulipewa

Mabingwa wa Nchi ya Tanzania, Simba SC, Kesho Jumamosi Januari 19' 2019 watakuwa ugenini Kinshasa DRC kukipiga na AS Vita Club katika mechi ya kundi D Ligi ya Mabingwa Afrika, mchezo ambao unatarajiwa kuwa ni mkali na wakusisimua katika dakika zote 90 za mchezo.

Mkuu wa habari wa klabu ya Simba, Haji Manara, De la boss amesema timu imejipanga na wanakwenda kuhahikisha wanapata matokeo mazuri kwa ajili ya Nchi na maslahi ya Simba SC.

..Mfumba Jicho MK 14 Meddie Kagere

Akiwa amecheka na vyavu mara 5 Ligi ya Mabingwa Afrika, na kuwa kinara kwa ufungaji, Meddie Kagere MK 14, Mfumba Jicho ataongoza safu ya ushambuliaji ya Simba SC kuhakikisha mabeki wa AS Vita Club wanakuwa na Tandabelua kwa muda wote wa mchezo.

..Nahodha wa Simba SC John Bocco!

Simba itamkosa nahodha wake John Rafael Bocco kutokana na kusumbuliwa na majeraha aliyoyapata katika mchezo dhidi ya JS Saoura

Kumbuka mchezo huu utashuhudia LIVE na ZBC 2 kuanzia saa moja kamili usiku..!

Kutoka Kiembesamaki, Zanzibar kwa niaba ya JFSimba..ni Ghazwat nakuambia Usikose Ukaambiwa.View attachment 997865View attachment 997866

Kikosi cha Simba kikifanya mazoezi ya mwisho Jana jioni, tayari kuwakabili AS Vita Club katika uwanja wa Stade des Martyrs DRC

View attachment 997867

Sent using Jamii Forums mobile app
Mkuu, injinia anasemaje?
 
kwani as vita wanna point ngapi.na sisi tuna point ngapi?
hyo ni Hatua ya makundi.
USICHANGANYIKIWE

Sent using Jamii Forums mobile app
As vita anà point 3 na magoli 5 tena wapo nafasi ya pili na wana magolì 2 ya kufungwa. Nyie underdog mna point 3 na magoli 3 pia mna maģoli 5 ya kufungwa kwahyo goli difference 2. Mechi ijayo mnaenda kūnyonyolewa tena ugenini (Misri)
 
Hahaaa. Nitoke nini sasa. 💃💃💃💃

Ila Pole eee.
Amakweli jana ndio nimeamini uchawi kwenye soka upo! Yaani Simba utafikiri walifungwa magunia ya mchanga mgongoni au miguuni! Walikua wazito utafikiri hawana mazoezi mwaka mzima. Wakongomani vigagula sana, watakuwa waliroga kupita kiasi, hasa kiungo wetu Chama ndio walimtupia mauchawi yao ya kuuua mtu kabisa, shwaini zao
 
Jana as vita walikuwa wamepiga ile kitu vumbi la congo, half time washamaliza pact moja ya condom

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Amakweli jana ndio nimeamini uchawi kwenye soka upo! Yaani Simba utafikiri walifungwa magunia ya mchanga mgongoni au miguuni! Walikua wazito utafikiri hawana mazoezi mwaka mzima. Wakongomani vigagula sana, watakuwa waliroga kupita kiasi, hasa kiungo wetu Chama ndio walimtupia mauchawi yao ya kuuua mtu kabisa, shwaini zao
Pole sana. Ndio mpira huo na nyie warogeni wakija kwa Mchina.
 
Akikujibu mwambie namsalimia. 😃😃

Ghazwat
Shadeeya naona machungu ya kupapaswa na Stand United kama yaliopoozwa vile na matokea ya Kinshasa eeh? Maana ukizingatia na rangi ya jezi za wale jamaa na sura za wachezaji wake wengine kama kina Makambo basi weye hapo kiroho kwatu, wala huna machungu ya kuchafua rekodi yako kwenye ligi
 
Back
Top Bottom