Kuelekea hatua ya Makundi Ligi ya Mabingwa Afrika, Simba SC dhidi ya JS Saoura, Injinia Soma hiyoooo!!

Ghazwat

JF-Expert Member
Joined
Oct 4, 2015
Posts
23,718
Reaction score
66,267
Hatua ya makundi ligi ya mabingwa Afrika kuanza kupigwa Jumamosi ya Januari 12, 2019 kwa wawakilishi wa Tanzania Simba SC, Mnyama Mkali kuliko wote mwituni, inakapokwaruzana na JS Saoura ya Algeria katika uwanja wa Taifa jijini Dar es salaam.

Uongozi wa Simba SC umeendelea kuhamasisha wanachama, mashabiki na wadau mbalimbali wa soka kujitokeza kwa wingi uwanja wa Taifa.

Mwenyekiti wa Simba SC, Swedi Mkwabi amewataka mashabiki na wanachama kujitokeza kwa wingi kuipa sapoti timu ili kuweza kupata ushindi, huku akiongeza kuwa wachezaji wako na hali nzuri na morali ya juu kuelekea mchezo huo, huku wakifanya maandalizi ya mwisho.

..Wekundu wa Msimbazi Simba SC

Meddie Kagere, MK 14 na John Bocco, Nyota hatari hawa wakiwa wamepachika mabao 3 kila mmoja, wataongoza mashambulizi dhidi ya JS Saoura, huku Cleoutus Chota Chama, Triple C ambaye ni moja ya sajili bora kabisa zenye tija kufanyika nchini akiwa sehemu ya kiungo mshambuliaji, ubunifu wake na uwezo wakufunga umekuwa chachu ya mafanikio kwa Simba.

..Mwana Kulitaka Mwana Kulipewa

Tiketi zimeanza kuuzwa leo katika vituo mbalimbali kwa shilingi 5,000, 10,000 na 100,000

Tiketi ya Platinum itakupa fursa ya kuchukuliwa katika hoteli ya nyota tano ya Serena Hotel ambao ni washirika wa Simba SC na kupelekwa uwanja wa Taifa na gari lenye hadhi (Luxury bus) likiongozwa na king'ora cha Traffic kwenda na kurudi hoteli Serena huku ukienjoy na soft drinks, bites bila kusahau jezi halisi mpya ya Simba SC

..This Is Simba SC...SimbaNguvuMoja







Sent using Jamii Forums mobile app
 
Lazima waarabu wakae.. JS Saoura ni kama waarabu wengine waliofungwa na Simba SC

Wale kule ndo wanaogopa waarabu mno![emoji3][emoji3]

Sent using Jamii Forums mobile app
Thomas Ulimwengu ataaaaaa......ngoja niishie hapa Hatakuja Minara asije akalialia ana aaaaaaa ngoja niishie hapa damu zisijeeeeee na ngoja niishie wasijekusema nimewaombea....maba....ngoja niishie hapa maneno ya Rage yasije yakaaaa.......

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Hizi taarabu J1 zitageuka kilio..Ulianza na Mbabane Swallows, Nkana FC na utaendelea kuteseka tu

Hivi siku ile ya mechi na Nkana ulivaa nyekundu ama [emoji3][emoji3][emoji3]

Sent using Jamii Forums mobile app
 
nimeuliza swali.jibu swali...hamchezi knock outs..inabidi mtie goli au mtiwe magoli..
Hakuna maana hilo swali. Yaani unaweka sharti iwe dakika 90 ndo nini?

Sitaki kufungua Mkataba au kupoteza muda kwahilo, Logic kubwa ni kumvua Bingwa Mtetezi Zamalek ardhi ya kwao

Soma hiyoooo Injinia [emoji3][emoji3][emoji3][emoji3][emoji3]

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…