Hatua ya makundi ligi ya mabingwa Afrika kuanza kupigwa Jumamosi ya Januari 12, 2019 kwa wawakilishi wa Tanzania
Simba SC, Mnyama Mkali kuliko wote mwituni, inakapokwaruzana na
JS Saoura ya Algeria katika uwanja wa Taifa jijini Dar es salaam.
Uongozi wa Simba SC umeendelea kuhamasisha wanachama, mashabiki na wadau mbalimbali wa soka kujitokeza kwa wingi uwanja wa Taifa.
Mwenyekiti wa Simba SC, Swedi Mkwabi amewataka mashabiki na wanachama kujitokeza kwa wingi kuipa sapoti timu ili kuweza kupata ushindi, huku akiongeza kuwa wachezaji wako na hali nzuri na morali ya juu kuelekea mchezo huo, huku wakifanya maandalizi ya mwisho.
..Wekundu wa Msimbazi Simba SC
Meddie Kagere, MK 14 na
John Bocco, Nyota hatari hawa wakiwa wamepachika mabao 3 kila mmoja, wataongoza mashambulizi dhidi ya JS Saoura, huku
Cleoutus Chota Chama, Triple C ambaye ni moja ya sajili bora kabisa zenye tija kufanyika nchini akiwa sehemu ya kiungo mshambuliaji, ubunifu wake na uwezo wakufunga umekuwa chachu ya mafanikio kwa Simba.
..Mwana Kulitaka Mwana Kulipewa
Tiketi zimeanza kuuzwa leo katika vituo mbalimbali kwa shilingi 5,000, 10,000 na 100,000
Tiketi ya
Platinum itakupa fursa ya kuchukuliwa katika hoteli ya nyota tano ya
Serena Hotel ambao ni washirika wa Simba SC na kupelekwa uwanja wa Taifa na gari lenye hadhi (Luxury bus) likiongozwa na king'ora cha Traffic kwenda na kurudi hoteli Serena huku ukienjoy na soft drinks, bites bila kusahau jezi halisi mpya ya Simba SC
..This Is Simba SC...SimbaNguvuMoja
View attachment 991213View attachment 991214
Sent using
Jamii Forums mobile app