Kuelekea hatua ya Makundi Ligi ya Mabingwa Afrika, Simba SC dhidi ya JS Saoura, Injinia Soma hiyoooo!!

Kuelekea hatua ya Makundi Ligi ya Mabingwa Afrika, Simba SC dhidi ya JS Saoura, Injinia Soma hiyoooo!!

Hatua ya makundi ligi ya mabingwa Afrika kuanza kupigwa Jumamosi ya Januari 12, 2019 kwa wawakilishi wa Tanzania Simba SC, Mnyama Mkali kuliko wote mwituni, inakapokwaruzana na JS Saoura ya Algeria katika uwanja wa Taifa jijini Dar es salaam.

Uongozi wa Simba SC umeendelea kuhamasisha wanachama, mashabiki na wadau mbalimbali wa soka kujitokeza kwa wingi uwanja wa Taifa.

Mwenyekiti wa Simba SC, Swedi Mkwabi amewataka mashabiki na wanachama kujitokeza kwa wingi kuipa sapoti timu ili kuweza kupata ushindi, huku akiongeza kuwa wachezaji wako na hali nzuri na morali ya juu kuelekea mchezo huo, huku wakifanya maandalizi ya mwisho.

..Wekundu wa Msimbazi Simba SC

Meddie Kagere, MK 14 na John Bocco, Nyota hatari hawa wakiwa wamepachika mabao 3 kila mmoja, wataongoza mashambulizi dhidi ya JS Saoura, huku Cleoutus Chota Chama, Triple C ambaye ni moja ya sajili bora kabisa zenye tija kufanyika nchini akiwa sehemu ya kiungo mshambuliaji, ubunifu wake na uwezo wakufunga umekuwa chachu ya mafanikio kwa Simba.

..Mwana Kulitaka Mwana Kulipewa

Tiketi zimeanza kuuzwa leo katika vituo mbalimbali kwa shilingi 5,000, 10,000 na 100,000

Tiketi ya Platinum itakupa fursa ya kuchukuliwa katika hoteli ya nyota tano ya Serena Hotel ambao ni washirika wa Simba SC na kupelekwa uwanja wa Taifa na gari lenye hadhi (Luxury bus) likiongozwa na king'ora cha Traffic kwenda na kurudi hoteli Serena huku ukienjoy na soft drinks, bites bila kusahau jezi halisi mpya ya Simba SC

..This Is Simba SC...SimbaNguvuMoja





View attachment 991213View attachment 991214

Sent using Jamii Forums mobile app
Kiongozi, mwambieni Haji mnacheza na JS Saoura siyo JS Soura kama alivyo andika kwenye press release.
 
Jumamosi utapata jibu. Itakuwa mwisho wa dharau zenu.
Hahaaah ombaomba fc a.k.a roho mbaya fc...mlianza na mbabane tukatatua marinda ya mashabiki wa ombaomba pamoja na mbabane wenyewe ingawa walioumia sana ni mashabiki wa ombaomba...tukaja nkana tukatatua marinda ya mashabiki wa ombaomba pamoja na nkana wenyewe ingawa walioumia sana ni mashabiki wa ombaomba...kesho tunatatua tena marinda ya waarabu pamoja na washabiki wake😂😂😂😂
 
Dah! Mkuu inawezekana umetawaliwa na ushabiki kuliko ualisia hv hapo kosa langu nn? Nainawezekana unajifanya shabiki kindakindaki wa yanga wakati ujawai ata kuichangia ata buku. Jifunze kuheshimu mawazo ya wenzio.
Kwan ujui simba akisonga mbele anatengeneza nafasi ya nchi kupata wawakilishi wengi kwenye hii michuano?
Mkuu acha kupata taabu kwani darasa fupi umelitoa. Mwenye kuelewa ameelewa.

Yaani anadai kuwa eti hakuna shabiki wa Yanga kama wewe, yeye kwa Yanga ni ndo msajili wa mashabiki na wanachama..?

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Aisee ili uendelee nilazima ujifunze kuwa na wivu wa maendeleo na sio kulogana au kuombeana dua mbaya. Emu wanayanga tujifunze kutoka kwa mikia japo kidogo.
Naona umeanza kushabikia mpira mwaka juzi. Ndio tunajifunza hivi kwa kuishangilia JS Saoura kama wao walivyofanya kwa TP Mazembe.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom