Kuelekea kuadhimisha miaka 10 ya ndoa

Kuelekea kuadhimisha miaka 10 ya ndoa

Foxhound

JF-Expert Member
Joined
Dec 15, 2013
Posts
28,710
Reaction score
76,243
Habari wadau, nikiwa nipo mbioni kuelekea kuadhimisha miaka 10 ya ndoa yangu leo hii nimeona nitoe ujumbe mfupi tu kwa wanaume kama mimi maana watoto wa kiume kwao sio rahisi kuiweza ndoa.

1. Ndoa ni sawa na gereza ambalo tofauti iliyopo kwa gereza la kawaida ni kwamba gereza la ndoa mfungwa huchagua mfungwa wenziwe wa kuishi nae gerezani.

2. Ndoa ni kipimo cha akili kwa maana wenye akili pekee ndio watakaoiweza ndoa kwani wasio na akili mapema sana huamua kujitoa.

3. Ndoa ni kipimo cha uvumilivu, hapa sasa kila mmoja na uwezo wake kwenye kuvumilia mambo yaliyomo ndoani, kuna uvumilivu kwa mambo na aina tofauti. Na wasio wavumilivu huishia ugomvi usiokwisha ikiwemo kupigana na mwisho wa siku kuishindwa ndoa.

4. Lakini pia ndoa ni kipimo cha utu, hapa sasa nataka niweke bayana baadhi ya mambo. Kuoa sio kwa ajili ya kupata watoto tu kwani hata watu wasio na ndoa wanao uwezo wa kupata watoto, isipokuwa utofauti uliopo watoto wanaolelewa na wazazi wao wakiwa ndoani hadi kufikia kuwa wakubwa huwa na makuzi mazuri sana.

Hasa ikichangiwa na wazazi wakiwa ni washika dini ipasavyo na hapa ndio pale ambapo utofauti wa mtoto aliyelelewa na wazazi wake na mtoto aliyelelewa na mzazi mmoja huonekana. Wazazi huweza kusaidiana majukumu mbali mbali ya kimalezi na kadhalika hiyo yote ni katika kuhakikisha watoto wao wanawalea katika misingi iliyo bora, huo ndio utu.

Kuwa na ndoa ni kitu ambacho kila mwanaadamu hutamani kuwa nacho isipokuwa baadhi ya matatizo, makuzi, nyendo na baadhi ya tabia ndio ambazo hupelekea baadhi yetu kuzishindwa ndoa. Kitendo cha kukosa utu ni kama vile kumuachia mwanamke mtoto alee peke yake, au mtoto kulelewa na mama mwengine asiye mama yake wa kumzaa, kitendo ambacho aidha kitapandikiza chuki kwa mtoto dhidi ya baba yake au mama yake.

Mwisho kabisa napenda niseme "Ndoa ni kwa wanaume na sio watoto wa kiume"

Ahsante.

Update
04 APRIL 2024 🎊🎊🎊🎉🎉
 
Kuwa na ndoa ni kitu ambacho kila mwanaadamu hutamani kuwa nacho isipokuwa baadhi ya matatizo, makuzi, nyendo na baadhi ya tabia ndio ambazo hupelekea baadhi yetu kuzishindwa ndoa.

Hapo ndo penye point huko kwingine umetukoromea brother
 
Hapana, kizazi cha sasa hivi wengi wa vijana mnaonekana kila kitu mnawadondoshea mzigo wanawake. Na ndio maana mko na team zenu za kataa ndoa. Mwanaume kama umetimia ndoa ni kitu cha msingi kwa ajili ya kuendeleza kizazi chako.
 
Habari wadau, nikiwa nipo mbioni kuelekea kuadhimisha miaka 10 ya ndoa yangu leo hii nimeona nitoe ujumbe mfupi tu kwa wanaume kama mimi maana watoto wa kiume kwao sio rahisi kuiweza ndoa.
1. Ndoa ni sawa na gereza ambalo tofauti iliyopo kwa gereza la kawaida ni kwamba gereza la ndoa mfungwa huchagua mfungwa wenziwe wa kuishi nae gerezani.
2. Ndoa ni kipimo cha akili kwa maana wenye akili pekee ndio watakaoiweza ndoa kwani wasio na akili mapema sana huamua kujitoa.
3. Ndoa ni kipimo cha uvumilivu, hapa sasa kila mmoja na uwezo wake kwenye kuvumilia mambo yaliyomo ndoani, kuna uvumilivu kwa mambo na aina tofauti. Na wasio wavumilivu huishia ugomvi usiokwisha ikiwemo kupigana na mwisho wa siku kuishindwa ndoa.
4. Lakini pia ndoa ni kipimo cha utu, hapa sasa nataka niweke bayana baadhi ya mambo. Kuoa sio kwa ajili ya kupata watoto tu kwani hata watu wasio na ndoa wanao uwezo wa kupata watoto, isipokuwa utofauti uliopo watoto wanaolelewa na wazazi wao wakiwa ndoani hadi kufikia kuwa wakubwa huwa na makuzi mazuri sana. Hasa ikichangiwa na wazazi wakiwa ni washika dini ipasavyo na hapa ndio pale ambapo utofauti wa mtoto aliyelelewa na wazazi wake na mtoto aliyelelewa na mzazi mmoja huonekana. Wazazi huweza kusaidiana majukumu mbali mbali ya kimalezi na kadhalika hiyo yote ni katika kuhakikisha watoto wao wanawalea katika misingi iliyo bora, huo ndio utu.

Kuwa na ndoa ni kitu ambacho kila mwanaadamu hutamani kuwa nacho isipokuwa baadhi ya matatizo, makuzi, nyendo na baadhi ya tabia ndio ambazo hupelekea baadhi yetu kuzishindwa ndoa. Kitendo cha kukosa utu ni kama vile kumuachia mwanamke mtoto alee peke yake, au mtoto kulelewa na mama mwengine asiye mama yake wa kumzaa, kitendo ambacho aidha kitapandikiza chuki kwa mtoto dhidi ya baba yake au mama yake.
Mwisho kabisa napenda niseme "Ndoa ni kwa wanaume na sio watoto wa kiume"

Ahsante.
ndoa ni makazi ya shetani, anaweka kambi hapo kabisa, kwahiyo maisha yenu yote mnapambana na changamoto moja baada ya nyingine
changamoto zingine zinatoka nje na zingine humohumo ndani
 
Back
Top Bottom