Kuelekea kuapishwa Biden kuwa Rais wa Marekani raia na askari hawatambuliki wote wamebeba silaha

Kuelekea kuapishwa Biden kuwa Rais wa Marekani raia na askari hawatambuliki wote wamebeba silaha

MakinikiA

JF-Expert Member
Joined
Jun 7, 2017
Posts
5,104
Reaction score
6,827

Armed groups cross the street as they hold a rally in front of a closed Texas State Capitol in Austin, Texas

Vikosi vya usalama viko nje ya majengo mbalimbali ya serikali

Vikundi vidogo vya waandamanaji - baadhi yao wakiwa na silaha - wamekusanyika nje ya majengo ya serikali ya Marekani, ambapo kuna mvutano mkubwa baada ya jengo la Capitol Hill kuvamiwa huko Washington.

Maandamano yanafanyika katika majimbo ya Texas, Oregon, Michigan, Ohio na kwingineko.

Lakini kulikuwa na hali ya utulivu Jumapili, baada ya kuimarishwa kwa ulinzi katika bunge congress la Marekani. FBI imeonya juu ya maandamano yenye silaha kabla ya kuapishwa kwa Biden siku ya Jumatano.


Rais mteule Joe Biden atachukua madaraka wiki mbili baada ya waandamanaji wafuasi wa Bw Trump kushambulia Jengo la Capitol la Washington mnamo Januari 6, na kusababisha vifo vya watu watano akiwemo afisa wa polisi.

Miji mingi imejiandaa kwa maandamano yanayoweza kuwa na vurugu mwishoni mwa wiki, huku vikosi vya usalama vikiwa vimeimarisha ulinzi.

Machapisho ya kwenye mitandao yanayomuunga mkono Trump na yaliitisha maandamano yenye silaha siku ya Jumapili, lakini wanamgambo wengine waliwaambia wafuasi wao wasihudhurie, wakidai ni jambo lililopangwa na askari kama mtego.

Kufikia sasa, ni idadi ya watu wachache tu ndio wamekusanyika katika baadhi ya miji , na kuacha barabara zinazozunguka majengo mengi ya serikali kuwa hazina watu.

Members of the Boogaloo Bois protest against the election of President-elect Joe Biden, outside the Michigan State Capitol in Lansing, Michigan

Wanachama wa Boogaloo Bois wakiwa nje ya jengo la serikali la Michigan huko Lansing
Jarida la New York Times liliripoti kuwa zaidi ya washiriki 20 wa vuguvugu la Boogaloo Bois walikuwa miongoni mwa waandamanaji wenye silaha ambao walikusanyika katika jengo la serikali huko Columbus, Ohio.

Lakini wanaume ambao ni wanachama wa kundi lenye msimamo mkali ambalo linataka kuipindua serikali ya Marekani - wanasema walipanga kwa muda mrefu kuwa na maandamano ya silaha.

Wakati huohuo huko Michigan, watu zaidi ya ishirini wakiwa wamebeba bunduki - waliandamana nje ya jengo la serikali huko Lansing, huku polisi wakiwatazama tu.

"Sikuja hapa kufanya vurugu na natumani hakuna mtu atakayejitokeza kuwa mkali," mwandamanaji mmoja aliliambia shirika la habari la Reuters.
Kundi lingine dogo la waandamanaji kama kumi hivi wakiwa na bunduki, walisimama nje ya Jumba la Texas huko Austin.
 
Ingekuwa Tanzania hii basi tungetukanwa Sana na wana harakati na matamko kibao kutoka kwenye balozi na umoja wa ulaya Ila kwasababu ni marekani watu watasifia tu utasikia mtu anasema hii ndio democrasia sasa.
 
Hili jambo si la kufurahia kwa nchi za Africa zinazokandamiza haki za wananchi wao hata kidogo - Chama cha Biden kina msimamo hatari sana juu ya hawa madikteta uchwara toka Africa

Wajiandae !!
 
Ingekuwa Tanzania hii basi tungetukanwa Sana na wana harakati na matamko kibao kutoka kwenye balozi na umoja wa ulaya Ila kwasababu ni marekani watu watasifia tu utasikia mtu anasema hii ndio democrasia sasa.
Beggars cannot be choosers, mkitaka wasiwe na sauti juu yenu kataeni na misaada yao basi tujue moja.
 
Hili jambo si la kufurahia kwa nchi za Africa zinazokandamiza haki za wananchi wao hata kidogo - Chama cha Biden kina msimamo hatari sana juu ya hawa madikteta uchwara toka Africa

Wajiandae !!
America as a country has a lot of internal problems to avail their savvy to,
As the matter of fact, Biden will start with cleaning up the mess Trump made.
 
America as a country has a lot of internal problems to avail their savvy to,
As the matter of fact, Biden will start with cleaning up the mess Trump made.
Biden atakuwa na kazi ngumu ya kurekebisha mambo ya hovyo yaliyofanywa na utawala wa Trump, sawa na itakavyokuwa kwa yule atakayechukua madaraka mwaka 2025 Tanzania.
 
Usishangae huu uzi ukakosa wachangiaji.
Maana Kuna wajinga wanaamini marekani ni malaika
Angalau America Countrywide ina taasisi zenye nguvu na zimaongozwa na watu wanaojitambua na kuheshimu miiko ya ajira zao. Ingelikuwa kama kwetu hapa Trump angekatalia madarakani, na pengine angeshaapishwa. Lakini ona vyombo hivyo viko dhidi ya Rais alieko madarakani.

Odhis *
 
Hii habari ingekuwa imeletwa inahusu nchi za Africa yangemwagwa matusi ya kiswahili na ya kizungu hapa,lakini kwasababu ni U.S akuna tusi hata moja.
Kwangu ni kukomaa kwa demokrasi ya hali ya juu sana.

yaani watu wanaruhusiwa kuandamana hata na siraha bila bughudha yoyote hali mradi hawafanyi fujo.

Kwa nchi za kiafrica na za kikomonist dhubutu hata kupeperusha jani angani ni shida kubwa sana.
 
Trump angeomba a,b,c za kung'ang'ania madaraka hata wikihow tu.
 
Back
Top Bottom