Nyanswe Nsame
Senior Member
- Jul 9, 2019
- 166
- 182
Kuelekea kufunguliwa kwa shule nchini elimu ya kujikinga na COVID 19, misaada yatolewa
SHIRIKA lisilo la kiserikali la kutetea Hakiza wanawake na watoto la Kivulini mkoani Mwanza limeanza kampeni maalumu ya kutoa elimu na msaada wa vifaa kinga kwa shule za msingi na Sekondari.
Msaada utatolewa katika shule za msingi zilizopo katika Wilaya za Misungwi, Ilemela, Kishapu na Bunda.
Shirika hilo leo Juni 25, limetoa vifaa kinga mbalimbali vya kujinga na ugonjwa wa homa kali ya mapafu unaosababishwa na kirusi cha Corona, katika shule za msingi.
Nje ya vifaa hivyo, elimu ilitolewa kwa walimu wa baadhi ya shule za msingi na Sekondari za Ilemela namna ya kutengeneza sabuni (Hard Soap) ili waweze kutengeneza shuleni.
Shirika hilo limetoa elimu pamoja na vifaa hivyo ili shule zitakapofunguliwa walimu waweze kuwahudumia na kuwakinga wanafunzi na maambukizi ya ugonjwa huo wa Corona.
Mkurugenzi Mtendaji wa shirika hilo, Yassin Ally, amesema nje za sabuni ya maji zilizotolewa pia watatoa matenki 26 yenye gharama ya Tsh Milioni saba.
Amesema wakati wa rikizo hii ya CORONA kulisababisha watoto kuzagaa mtaani, wengine kufanya kazi za uchuuzi na uchungaji wa mifugo.
Amesema kutokana na hali hiyo imewalazimu kama shirika kuwapa elimu ya ustadi na ujuzi mpya wa saikolojia ya kurudi kufundisha wanafunzi waliorudi na tabia tofauti.
"Katika kuunga mkono Serikali wakati huu wa kufungua shule, tunatoa matenki 26 ya ujazo wa lita 1000 kwa shule 26 za wilaya hizo.
"Matenki 10 yatapelekwa Shule za Wilaya ya Misungwi, manane Shinyanga vijijini na nane mengine yataenda Kishapu ambako kuna changamoto ya maji," amesema Yassin.
Maimuna Kanyamara ni Mkurugenzi wa Shirika la mikono Yetu, amesema wameshirikiana na KIVULINI kutoa misaada hiyo kutokana na shirika lao kujihusisha kwa ukaribu na masuala ya shule.
Amesema wanatoa elimu kwa walimu kutokana na eneo la shule limeonekana kutokuwa na elimu ya kutosha kuhusu ugonjwa hatari wa Corona.
Benatus Kahuru ni Afisa elimu Elimu ya watu wazima Manispaa ya Ilemela, amesema mafunzo hayo yatawasaidia kutoa elimu kwa wanafunzi namna ya kujinga na ugonjwa huo wa Corona.
Manispaa ya Ilemela mwaka jana ilishika nafasi ya pili kati ya shule 185 kwenye mtihani wa Taifa wa darasa saba.
Mwisho