Kuelekea laini za simu zisizosajiliwa kuzimwa; Ushauri wa namna bora ya kufanya ili kutovunja sheria za nchi

Kuelekea laini za simu zisizosajiliwa kuzimwa; Ushauri wa namna bora ya kufanya ili kutovunja sheria za nchi

Kituo Cha NIDA kinapokea watu 20,000 kwa siku; halafu mkuu wa kituo hicho anajisifu kwa kutoa namba za utambulisho 800 kwa siku ;
Hesabu rahisi 20000/800 = siku 25
Uzembe wa Hali ya juu.
 
Ila mimi sijatetea suala la muda kutosha ama la, kuwepo kwa deadline ama isiwepo n.k.

Mimi nilimjibu Mleta uzi upande wa uhitaji wa kubadilika na teknolojia.

Nadhani Wenye mamlaka wana jukumu la kuangalia mkwamo wa zoezi upo wapi na wasiwaonee wasio na hatia, kama ni NIDA basi wao ndio wabebeshwe msalaba wao na si Wananchi.

Mabadiliko yanapaswa kwenda na hali na uchumi wa watu.
Kama kuleta dijitali kunamaanisha expensive technology kulinganisha na hali ya uchumi wa watu, then kuintroduce hiyo dijitali ni counterproductive.
Hivi unajua siku hizi bongo kumiliki TV ni kama anasa?
 
Hakuna namba itakayofungiwa kirahis ivyo, ile ni biashara wenye biashara yao hawawez kubali loss kipuuz ivyo, nashangaa watu wamekomaa na ishue ya kufungiwa


Sent from my iPhone using JamiiForums
 
voda Sasa wanakubali kusajilia kwa majina tofauti ila nafikiri wamechachelewa kwa hizi siku mbili zilizobaki wangeanza mwanzo wangezitoa
 
By the way, lengo la kuisajili cad za simu kwa kitambulisho cha NIDA ni nini?
 
Niwaulizeni nyie mnalalamikia NIDA TCRA hivi NIDA wanamiaka ngapi toka waanze kutoa vitambulisho.TCRA nao wana muda gani toka waanze kutuhimiza tukasajili line zetu.

Wasilaumiwe makosa ni yetu wananchi kila jambo tunadharau ata mombo ya msingi tunaleta dharau mie nimejiandikisha miezi ya nyuma huko na famila yangu baada ya muda mchache tumchuka namba.au toka miaka yote mlikua amjafikisha miaka 18 sasa ndio mmefikisha hiyo miaka.

Acheni lawama kwanza TCRA wametuvumia sana Chekini mnavyopanga mafoleni mtasema mnasubiria Mwendo Kasi Kimara.WAZIME LINE MSAJILI ZINGINE MLIYATAKA WENYEWE
 
NIDA kumekuwa na folen ya kufa mtu sio kwa kuwa watu wanataka vitambulisho vya Taifa bali kwa kuwa wanapigania namba zao za simu zisizimwe

Yaan watu hawana mpango na vitambulisho sema tu inabidi wawe nacho kukamilisha usajili

I.e line ya simu ni muhimu kuliko kitambulisho
ikitangazwa kuwa usajili wa line sio muhimu kitambulisho cha NIDA basi folen inaisha fasta
Mkiambiwa Serikali hii ni "Serikali Tegeshi" mnalalamika nyie waimba mapambio.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Je laini yako ikifungwa na ulikuwa unaitumia WhatsApp akaunti yako itaendea kuwepo !!
 
Sijaona wala kusikia Diwani, mbunge na waziri wakilalamika kupanga foleni NIDA muda mrefu
 
Kwa wale wenye wasiwasi na vijana wanaopita mitaani kuwasajilia laini zaidi ya moja unaweza kwenda Mtandao husika ukaomba wakuonyeshe laini zako zote zilizotumia kitambulisho chako ambazo huzitambui wanazicancel nimeona Hayo ktk Mtandao WA airtel
 
Je laini yako ikifungwa na ulikuwa unaitumia WhatsApp akaunti yako itaendea kuwepo !!
WhatsApp kinachotumika ni internet namba yako utambulisho tu ndio maana unaona mtu yupo Ulaya ila anatumia utambulisho wa namba yake ya voda au tigo utashindwa kuiupdate kwa sababu namba za kuverify wanakutumia kwenye namba ya utambulisho
 
Back
Top Bottom