Kuelekea laini za simu zisizosajiliwa kuzimwa; Ushauri wa namna bora ya kufanya ili kutovunja sheria za nchi

Kuelekea laini za simu zisizosajiliwa kuzimwa; Ushauri wa namna bora ya kufanya ili kutovunja sheria za nchi

Kuna wengine ni wa kuonewa huruma,ila wengine wanastahili kufungiwa ni wazembe,kuna watu wanajitiaga wako bize na wengine wanangojea siku za mwisho za zoezi ndio wanaanza kuhangaika
 
Kesho watakuja na tamko lingine
La kuongeza muda tena

Ova

Sent using Jamii Forums mobile app
MH atakuwa amefanya Jambo Jema Sana kama atatoa amri Muda uongezwe. Na itakuwa vema kama atatoa Muda wa kutosha like six months or something ili watu wote waweze kupata namba za NIDA na hivyo kutimiza zoezi la kusajili line zao.
 
Mkuu, hebu kuwa serious, watu tumejaza fomu za kuomba kitambulisho tangu mwezi wa tisa mpka leo sijapata namba , afu unanificha laini , hapo kosa Ni la Nani , wanipe namba au kitambulisho then wafunge kwa uzemve wangu
 
Wengine wanasubili kupewa kesi za utapeli maana matapeli washazipata laini zilizosajiliwa tayari,ee Mungu naomba utunusuru kwenda kisutu.
 
MLIPOAMBIWA MABADILIKO YA KWELI ANAYO JPM,PIA MLIBISHA.

MLIPOAMBIWA JPM HANA URAFIKI,MLIBISHA.

MLIPOAMBIWA JPM ATA- DEAL NA MAFISADI HADI KIELEWEKE MLIBISHA.

MLIPOAMBIWA JPM ATAIRUDISHA TANZANIA KWENYE RIGHT TRACK PIA MLIBISHA,

HAYA WEWE ENDELEA KUPIGA RAMLI

LAKINI NDIO MWISHO WA MATAPELI WA MITANDAO YA SIMU UMEWADIA USIKU WA LEO!

[emoji1241][emoji818]2020 - 2025,JPM[emoji818]

Sent using Jamii Forums mobile app
Kapimwe kalio

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Serikali yangu inabidi ijitathmini kwa kina kuhusu huu usajili kama vipi ipige kimya tu uchaguzi upite ila zoezi limekwama kwa asilimia 50.

Watu hawana hata cheti cha kuzaliwa anapataje kitambulisho cha NIDA wakati wajawazito zahanati za shida watu wanazaliwa vichakani hivi man'gati wangapi na wahadzabe wana vyeti vya kuzaliwa let alone NIDA.

Hili zoezi ni kichekesho serikali ijitathmini imekwama wapi ianze uko chini then haya matamko ya mjini wahakikishe huko vijijini kuko vizuri kwanza.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Wazime tu. Tumechoka kusikia hizo ngonjera za kila siku zinazohusisha maneno matatu ya kuzima, laini na NIDA.
 
Naibu Waziri wa wizara ya mawasiliano na uchukuzi amenukuliwa mjini Kigoma akisema kuwa watu watakao zimiwa laini za simu ni wale ambao hawajajaza fomu za NIDA kabisa lakini Kwa wale walio jaza fomu za NIDA serikali itatumia hekima katika kudili na suala Lao.
Kesho kuna tamko jingine kuonyesha "hekima" waliyonayo wenye nchi.
 
.
By Happiness Tesha, Mwananchi htesha@mwananchi.co.tz
Kigoma. Serikali ya Tanzania imesema itatumia hekima kuwasaidia wananchi walioshindwa kusajili laini za simu kwa sababu ya kukosa kitambulisho cha Taifa na namba licha ya kuanza mchakato wa kupata kitambulisho hicho.

Imesema wananchi hao taarifa zao zipo katika Mamlaka ya Vitambulisho vya Taifa (Nida), huenda wamekosa kitambulisho au namba kwa sababu zilizo nje ya uwezo wao.

Hayo yameelezwa leo Jumapili Januari 19, 2020 na naibu Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Atashasta Nditiye katika mkutano wa ndani wa CCM mkoani Kigoma.

"Serikali itaona jinsi ya kutumia hekima kwa wananchi ambao taarifa zao zipo katika ofisi za Nida kuona namna ya kufanya lakini kwa wengine ambao hawajajaza fomu laini zao zitazimwa,” amesema Nditiye.

Amesema ambao laini zao zitazimwa ni wale waliosajili laini chache na kuacha nyingine licha ya kuwa na kitambulisho hicho.

Amebainisha kuwa usajili wa laini za simu ni endelevu licha ya baadhi ya wananchi kupuuza.


Kesho Jumatatu Januari 20, 2020 laini zote za simu ambazo hazijasajiliwa kwa alama za vidole zitazimwa. Ili uweze kusajili laini ni lazima uwe na kitambulisho cha Taifa au namba ya kitambulisho hicho.


Jr[emoji769]
 
Back
Top Bottom