mrangi
JF-Expert Member
- Feb 19, 2014
- 88,759
- 123,368
Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
MH atakuwa amefanya Jambo Jema Sana kama atatoa amri Muda uongezwe. Na itakuwa vema kama atatoa Muda wa kutosha like six months or something ili watu wote waweze kupata namba za NIDA na hivyo kutimiza zoezi la kusajili line zao.
Kapimwe kalioMLIPOAMBIWA MABADILIKO YA KWELI ANAYO JPM,PIA MLIBISHA.
MLIPOAMBIWA JPM HANA URAFIKI,MLIBISHA.
MLIPOAMBIWA JPM ATA- DEAL NA MAFISADI HADI KIELEWEKE MLIBISHA.
MLIPOAMBIWA JPM ATAIRUDISHA TANZANIA KWENYE RIGHT TRACK PIA MLIBISHA,
HAYA WEWE ENDELEA KUPIGA RAMLI
LAKINI NDIO MWISHO WA MATAPELI WA MITANDAO YA SIMU UMEWADIA USIKU WA LEO!
[emoji1241][emoji818]2020 - 2025,JPM[emoji818]
Sent using Jamii Forums mobile app
Jambo hili linaukweli kiasi gani ndugu??Hakuna laini ata moja itafugwa, hizo ni propaganda na vitisho kwa raia.
Jambo hili linaukweli kiasi gani ndugu??
Kesho kuna tamko jingine kuonyesha "hekima" waliyonayo wenye nchi.Naibu Waziri wa wizara ya mawasiliano na uchukuzi amenukuliwa mjini Kigoma akisema kuwa watu watakao zimiwa laini za simu ni wale ambao hawajajaza fomu za NIDA kabisa lakini Kwa wale walio jaza fomu za NIDA serikali itatumia hekima katika kudili na suala Lao.
By Happiness Tesha, Mwananchi htesha@mwananchi.co.tz
Kigoma. Serikali ya Tanzania imesema itatumia hekima kuwasaidia wananchi walioshindwa kusajili laini za simu kwa sababu ya kukosa kitambulisho cha Taifa na namba licha ya kuanza mchakato wa kupata kitambulisho hicho.
Imesema wananchi hao taarifa zao zipo katika Mamlaka ya Vitambulisho vya Taifa (Nida), huenda wamekosa kitambulisho au namba kwa sababu zilizo nje ya uwezo wao.
Hayo yameelezwa leo Jumapili Januari 19, 2020 na naibu Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Atashasta Nditiye katika mkutano wa ndani wa CCM mkoani Kigoma.
"Serikali itaona jinsi ya kutumia hekima kwa wananchi ambao taarifa zao zipo katika ofisi za Nida kuona namna ya kufanya lakini kwa wengine ambao hawajajaza fomu laini zao zitazimwa,” amesema Nditiye.
Amesema ambao laini zao zitazimwa ni wale waliosajili laini chache na kuacha nyingine licha ya kuwa na kitambulisho hicho.
Amebainisha kuwa usajili wa laini za simu ni endelevu licha ya baadhi ya wananchi kupuuza.
Kesho Jumatatu Januari 20, 2020 laini zote za simu ambazo hazijasajiliwa kwa alama za vidole zitazimwa. Ili uweze kusajili laini ni lazima uwe na kitambulisho cha Taifa au namba ya kitambulisho hicho.
Sawa ngoja tuoneLina ukweli baada ya 23:59
😀😀😀😂😂