Kuelekea laini za simu zisizosajiliwa kuzimwa; Ushauri wa namna bora ya kufanya ili kutovunja sheria za nchi

Katika harakati za kusajili line kwa alama za vidole nimekutana na kimbembe cha kutoa hela kwanza ndipo usajili ukamilike.

Cha kushangaza ni kuwa kwenye akaunti yangu kuna zaidi ya mil 1 alafu kiwango cha mwisho kufanya miamala kwa siku ni sh mil 1.

Nyie vodacom naona mmekua wasumbufu. Nawaambia leo ndo mwisho kutumia huduma zenu. Maana sijajua ni kwanini mnalazimisha nitoe hela kwenye akaunti yangu ya M PESA wakati mitandao mingine nimesajili bila usumbufu.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Ni Kama utani vile kesho ndio kesho laini zinakwenda kuzimwa rasmi.Tangazo tulipewa mapema lakini kutokana na changamoto mbalimbali baadhi yetu tukachelewa kujaza fomu.Wengine walijua utani wakadhani nguvu ya soda kwa maneno kumbe sio ni mwendokasi wa vitendo.Kila nikisikia neno NIDA akili inaenda mbio foleni Kama yote,baadhi ya watanzania wanapambana kwa udi na uvumba kuhakikisha wanapata namba za NIDA.Wafanyakazi wa NIDA wanapiga kazi usiku na mchana nao wananchi wakesha usiku kucha kuhakikisha wanapata namba za NIDA Ili wakamilishe usajili wa laini za simu.Mwitikio ni mkubwa muda mchache ni maombi yangu kwa serikali ya jamuhuri ya muungano wa Tanzania tunaomba watuongezee angarau siku 10 ili ambao baadhi yetu taarifa hatujakamilisha tuweze kukamilisha. Tunaiomba serikali ya Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania ituongezee walau hata siku 10 tu.

#Tupande miti kwa wingi mkoa wa Dodoma.Dodoma kuwa kijani kama Morogoro na Mbeya inawezekana.Serikali itoe support kwa kugawa Miche ya miti kwa kila kaya bure.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Niko huku vijijini wakina mama wako na watoto mgongoni wakisajiri line na hakuna network. Ila sisi hatutalia na nida tutalia na tulio wapigia Kura watuongoze
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…