Kuelekea laini za simu zisizosajiliwa kuzimwa; Ushauri wa namna bora ya kufanya ili kutovunja sheria za nchi

Kuelekea laini za simu zisizosajiliwa kuzimwa; Ushauri wa namna bora ya kufanya ili kutovunja sheria za nchi

Utawala huu wa Magufuli ni rahisi sana kutabiri kitu na kikatokea.
Nilitabiri Babu Seya atatoka ile December 9 2017 ikawa, nilitabiri 2019/2020 watumishi wa umma hawataongezewa hata senti ikawa. Leo narudia tena kutabiri utabiri huu mgumu kuwa line za simu zisizosajiliwa kwa namba ya NIDA kesho tarehe 20 kuelekea tar 21 hazitafungwa.
Kama unabisha tuwekeane dau
Dah let's wait and see mkuu
 
Ni hakika wengi hawajaweza kusajili simu zao na sababu ni NIDA kushindwa na pia tabia ya wananchi kusubiri deadlines.

Nashauri laini hizi zisizimwe bali tozo ya shilingi 1000 iwekwe kwa kila siku itakapochelewa kusajiliwa. Pesa hizo ziende moja kwa moja Serikalini. Pia zoezi la usajili liwe endelevu.
Nitozwe fine kwa kosa lipi ndugu?

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mi nipo hewani mkuu
Utazimiwa soon.
Lakini itatusaidia sana kubana matumizi, haya mabando yalikuwa yanatumalizia sana hela. Tutarudi kwenye internet cafe kama zamani, nusu saa kwa wiki sh 500 tu.
Na nyumbani siyo lazima kila mmmoja awe na simu.
Yale mambo ya kila mtu ana simu nyumbani hadi housegirl na watoto wa form two fyekelea mbali.
Simu hata ya jirani itasaidia.
Binafsi hii kitu ya kukata mtandao wa wasiosajiliwa itanipunguzia matumizi ya sh 2,000 kwa siku ambayo ni kama 60,000 kwa mwezi. Hebu twende mwendo huo kwanza, usawa huu mgumu sana.
Kila changamoto ina faida zake, wazungu wanasema 'a blessing in disguise'!
 
Tarehe 20.
Inaisha saa 23:59.
Uliambiwa usajili laini yako kabla ya tarehe 20 January,leo ni tarehe ngapi,nakwanini uwe hewani hadi saa hizi wakati ni tarehe 20,ingekuwa walisema sajili laini yako kabla ya tarehe 21 wewe ambaye hujasajili usingeshangaa kuwepo hewani hadi saa hizi.
Kuna kitu,siyo bure,endapo upo hewani hadi muda huu,wakati hukutakiwa kuwepo.
KABLA na siyo BAADA.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kama umesajili line yako na bado unasubiri taarifa confirmation au bado hujasajili naona baadhi yetu tumeanza kuonja joto la kuzimiwa mtandao.

Si mimi hata jamaa yangu hapo Dar hapatikani, nimetumia njia mbadala kwa kupitia jamaa wa ofisini kwake ndipo akaniambia yupo ofisini.

Sijaelewa kama ndiyo wamefanya yao au wanatest mitambo, mdau huko ulipo vipi upo hewani?

Kwani tarehe 21 imefika?
Si walisema mwisho ni tarehe 20/1/2020, ina maana leo bado hawajasitisha/funga mawasiliano. Ikifika saa 5.dk 59.sek 59 usiku leo, basi watafunaga kama ni kweli watafanya hivyo.

Kama kwako wamekata, basi wewe uko mbele kwa siku nzima.
 
Usiwe na shaka Ndugu, hawezi kuzifikia zote, hawana uwezo huo, unakumbuka wakati ule waliposema wanafunga simu zote ambazo hazikuwa zimethibitisha IMEI number ?!, wewe endelea na shughuli zako inaweza kuwa ni tatizo la Network.
 
Kwani tarehe 21 imefika?
Si walisema mwisho ni tarehe 20/1/2020, ina maana leo bado hawajasitisha/funga mawasiliano. Ikifika saa 5.dk 59.sek 59 usiku leo, basi watafunaga kama ni kweli watafanya hivyo.

Kama kwako wamekata, basi wewe uko mbele kwa siku nzima.
Unaelewa maana ya KABLA ya tarehe 20?Leo ni 20 au?
 
Mimi nina daiwa shilingi 4900 kwenye nipige tafu..
kiukweli hii nilikuwa nataka nilipe ila nahofia laini yangu kufungwa kwasababu sijasajili kutumia alama za vidole..

Najua kuna wengine wanadaiwa songesha, Wengine M-pawa.. Wengine wamekopa airtel, halotel au tigo
Je laini zao zikifungiwa, nani atawalipa mitandao ya simu fidia?
 
Back
Top Bottom