Kuelekea laini za simu zisizosajiliwa kuzimwa; Ushauri wa namna bora ya kufanya ili kutovunja sheria za nchi

Wazimage tu,mimi ndo hata sijui unapita njia gani hadi kupata hiko wanachoita kitambulisho.

Sisemi sikihitaji lah,tatizo njia wanayotaka kuitumia ya kushurutishana kufunga biashara na kwenda kusimama foleni siku mbili kisa card ya taifa ndo unaonitia ukakasi,narudia acha wanifungie na jioni hii voda wamenisisitiza kama sms ya mwisho inavyoonekana hapa but sitahangaika mpaka mfumo wa kutoa hivyo vitambulisho uboreshwe

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Na TSH 1000 unaikata kwa njia gani???hivi unawajua wabongo au unawasikilizia.basic solution ni kufunga line za simu,akili ndio zitukae sawa.
 
Wanazima line za simu,Mwananchi wakati wa kujiandikisha kaweka namba yake ya simu hapo.

Kesho namba inatoka NIDA, watampata vipi mwananchi kumpa taarifa za namba yake .
Inachekesha sana!!!

Sent from my Redmi Note 5 using Tapatalk
 
Ni kweli tutazoea tu kwa sababu hakuna namna. Lakini tukichukulia mfano wa kutoka kwenye mfumo wa analogia na kulazimika kununua hivi ving'amuzi wananchi tumezoea katika hali yenye urahisi au ugumu wa maisha?
 
Zinazimwa kuokoa pesa zinazopotea kununulia mabando ya kuangalizia shilawadu kwenye youtube na mawasap. Pesa nyingi sana inapotelea kwenye ujinga. Zima zote tuokoe gharama.
Mkuu wewe ndiye mshauri wa makonda nini,maana kwa akili yake inavyotafsiri ni kwamba wale wote tusiokuwa na vitambulisho wala # za nida tulikuwa tumekalia umbea ndo maana tumepitwa na mambo ya msingi kama haya.

Sent from my Redmi Note 5 using Tapatalk
 
Ving'amuzi vya tv ni habari tofauti na hii ya NIDA. Ving'amuzi havikuwa na masharti ya NIDA. Analogia ilizimwa, watu wakanunua ving'amuzi, basi.

Hata hii ya kusajili simu nashangaa hivi wataalam wa tehama huko NIDA wameshindwa kupata taarifa kutoka databases zote zilizopo? Kwa mfano, TCRA wameshindwa ku merge data zilizoko TRA (leseni za udereva na TIN), Tume ya Uchaguzi (kitambulisho cha mpiga kura) na RITA (vyeti vya kuzaliwa), halafu kati ya hivyo yule ambaye taarifa zake hazijakamilika ndiye wamtumie ujumbe kuwa fika kituo fulani (wanazo GPS na locations zote za wenye simu wanazijua), wameshindwa nini?
Kwa utaratibu huo ni watu wachache tu wangehitajika kwenda kujiandikisha, hasa wale wasiokuwa na vyeti vya kuzaliwa.

Tunasomesha watu TEHAMA kwa faida gani kama kitu kidogo kama hiki kinawashinda?
 
Hapana, ninyi msiokuwa na vitambulisho vya NIDA mkizimiwa simu mtakuwa mmesaidiwa kubana matumizi. Hebu imagine kupitisha mwezi mzima bila kununua bando, ni pesa ngapi unaokoa. Zidisha mara watu milioni kumi.
 
Hapana, ninyi msiokuwa na vitambulisho vya NIDA mkizimiwa simu mtakuwa mmesaidiwa kubana matumizi. Hebu imagine kupitisha mwezi mzima bila kununua bando, ni pesa ngapi unaokoa. Zidisha mara watu milioni kumi.
Unaongea as if kichwa umekifungia kabatini au umekisahau kwenye daladala,unajua line zangu kupitia miamala ya pesa ni sh ngapi serikali inapata na tupo wangapi tupo ktk Hali hiyo?

Usichukulie vitu kiwepesi kiasi hiko.

Sent from my Redmi Note 5 using Tapatalk
 
Sisi tunashangilia kupata fursa ya kubana matumizi yeye anasema nini? Hizo simu zifungwe.
Kufungiwa simu ni sawa na teja kupelekwa sober house, ambako supply ya unga inakatwa hadi anakaa sawa. Na sisi hii itatusaidia kufuta uteja wa kijinga wa airtime na mabando.
 
Wewe unajali pesa ambazo serikali inapata au zile ambazo wewe unapata?
Furahia hii nafasi ya kusaidiwa kuondoa uteja wa airtime na mabando. Ni kama tunapelekwa sober house, tutarudi na akili tofauti kabisa, tutagundua kuwa maisha bila wasapu na youtube yanawezekana.
Tuwashukuru TCRA kwa kutuokoa dhidi ya uteja huu unaoleta umasikini.

Nyumba ina baba mama na watoto na simu zao zote zina mabando, kutwa kubofya tuuuuuu! Bora zizimwe.
Kama ni miamala tutatumia fahari huduma zimejaa kila kona.
 
..............Dah imebidi nicheke,mkuu wewe Muha nini?

Sawa point tatu chukuwa wewe ndugu yangu.

Sent from my Redmi Note 5 using Tapatalk
 
Imebaki saa nne jamani, bado nahaha kesho itakuaje bila mawasiliano jamani ndugu zangu mweeeeeh

Ngoja nielekee NIDA

Piga ndulu uwiiiii!

Jamani TCRA waliamshe dudeeeee
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…